Hii mwanzilishi wa hii idea katika siasa za TZ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii mwanzilishi wa hii idea katika siasa za TZ?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Kapwani, Jun 22, 2010.

 1. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #1
  Jun 22, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wana JF nina swali linaloniumiza kichwa sana hapa...hii mnafahamu ni nani aliyeanzisha ideas hizi 2
  1) Rais kuchangiwa kuchukua fomu
  2) Kutangaza nia ya kugombea mwaka 2010

  Rais kuchangiwa fedha kwangu mimi naona haya mambo hayana maana .....kama kundi la watu linadhani kuwa JK anafaa basi wasubiri kumpigia kura October....dhana ya michango huja pale ambapo mtu anahitaji kusaidiwa ili afanikishe suala fulani. Je ni kweli JK hana hela iyo....kumchangia huku unajua kuwa ana uwezo si unafiki huo??? si gia za wanaofacilitate kukumbukwa JK akipita October hata kama hawana uwezo wa kuongoza? Je rais kama mwanadamu hataweza kuwapendelea hawa waliomchangia kwa mfano UDOM nakuwaacha UDSM au SUA kwa sababu hawakumchangia? MIMI NINGEKUWA JK NINGEKATAA KUTOKA SIKU YA KWANZA WAZO LA KUCHANGIWA KWA SABABU LINAWEZA KUKUWEKA KARIBU NA
  WANAFIKI ZAIDI KULIKO WATU WENYE UPEO. NINGESHAURI WATU WOTE WANAONIUNGA MKONO WAJITOKEZE KUPIGA KURA NA HIZO FEDHA WAZIPELEKE KWENYE CHARITY ORGANIZATIONS AMBAKO NDIO HALISI WANAHITAJI MICHANGO

  Suala la kutangaza nia halionyeshi ubaya ukiliangalia juu....lakini ukifakari kwa undani unagundua kuwa kuchafuka kwa hali ya hewa kwingi kumeletwa na watangaza nia....watu hawa na wapambe wao wameacha shughuli zao za msingi na kukalia kutangaza nia....wamesababisha tension kubwa kwa wabunge wetu hata bunge la bajeti sasa limegeuka mahali pa wabunge wa sasa kutolea machungu yao dhidi ya hao watu...tension kila mahali....kamati zinaundwa kujadili migogoro hii WATU WANAACHA KAZI ZA MSINGI WANA DEAL NA WATANGAZA NIA
  katika nchi maskini kama hii baadhi ya taratibu kama hizi lazima zichunguzwe madhara yake kabla ya kuziweka....siasa ni chakula....jamani kama wagombea ubunge wangesubiri tu July wakachukua fomu ingekuwaje? Na ninani mwanzilishi wa ideas hizi?

  Mix with yours
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Jun 22, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Politics is supposed to be the second-oldest profession. I have come to realize that it bears a very close resemblance to the first.
   
 3. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #3
  Jun 22, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  As a result of engineering, many useful products were created from a chaos of facts; however, it is politics that created chaos.
   
 4. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #4
  Jun 23, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Jun 23, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kwapani,
  Mkuu unaweza kunambia ni kiasi gani cha fedha kinatakiwa kwa mgombea kufanya kampeni za uchaguzi Tanzania nzima?.. labda nitakuelewa unachotaka kusema, kinyume cha hapo tuichambue hiyo Demokrasia ya vyama vingi inayokuja na mengi yasiyowezekana kwetu..Nakumbuka wakati wa Nyerere tulikuwa na demokrasia yayetu ya kuchagua vichwa vya watu kwa alama ya jembe au nyumba. Hapakuwa na gharama kubwa zaidi ya hotuba za Wabunge tena basi mkutano unaweza kuwa mmoja tu..kama wana kijiji wako hawakufahamu huwezi kushinda.. Na hakika sisi Wakerewe hatujawahi pata Mbunge makini toka tupate uhuru zaidi ya mzee wetu Msonge..
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  ==>> prostitution..
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,200
  Trophy Points: 280
  Kwa nini wanaotaka kumchangia KJ kuchukua fomu, kwa mapenzi yao, bila kulazimishwa, wasiweze kumchangia?

  Tanzania ni nchi huru, na kumchangia mtu si lazima awe hajiwezi, kuna watu wanawanunulia nguo wazazi wao kwa kuonyesha moyo wa ahsante tu, wakati wazazi wenyewe huenda wana uwezo kuliko watoto. Kama unataka ku question track record ya Kikwete naweza kukuunga mkono, lakini unapotaka kukataza watu, watu wazima, watu wenye hiyari yao, hawakushurutishwa, kumchangia mtu wanayempenda wao, naanza kukuogopa kuliko hata huyo Kikwete mwenyewe.

  Maana sijui kesho utasema nini, watanzania wote wapige kura against Kikwete na wasipopiga utawafuata majumbani mwao?

  Tuna uhuru wa kujihusisha na vikundi vya kisiasa tunavyotaka.Kama una matatizo na siasa za Kikwete tuambie hapa, wengi hatumpendi huyu rais kwa mengi tu na tunaweza kukuuunga mkono.


  Kuhusu kutangaza nia ya kugombea 2010 mimi naona alitakiwa kutangaza mapema sana ili tujue wazi mapema, maana kuna washashi kipindi kile alivyoanguka anguka Mwanza walishaanza kumzushia kwamba ni one term president, mimi nikawauliza in bongo?
  Lakini katika hili la kutumia haki yake ya kikatiba kuchukua fomu, na watu fulani kutaka kuonyesha kumuunga mkono kwa kumlipia ada za fomu, mimi kamwe siwezi kukuunga mkono.
   
 8. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135

  Mkuu hapa tuko pamoja and I think michango hii ilitakiwa iwe ni kusaidia kampeni na si kuchukulia form which to me sounds as missalocation of resources.
   
 9. W

  WildCard JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mtake msitake wapo watu wanaridhika na kunufaika sana na utendaji wa JK. Mnapojaribu kuwabeza, kuwakejeli na kudhani wanapotoka mnapoteza muda wenu tu. Wambieni mnaodhani wanafaa zaidi ya JK wajitokeze, muwachangie, washinde, watuongoze. Vinginevyo kujadili mapenzi na hisia za watu wengine ni kutwanga maji kwenye kinu. Hata hivyo mnabaki na haki yenu ya msingi kutoa maoni.
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,200
  Trophy Points: 280
  Mimi sina tatizo na kumbeza na kumkejeli JK, kama kuna watu wameridhika na utendaji wake kuna wengine hatujaridhika nao.Different strokes for different folks.

  Tatizo langu linakuja pale watu wanapotaka kumbeza JK kwa non-issues, kama vile wameishiwa na issues za kweli za kumbezea. Eti mtu anakuja kuhoji uhalali wa JK kuchangiwa, si ndiyo demokrasia yenyewe hiyo mliyokuwa mnalilia? Au demokrasia wachangiwe wapinzani tu, akichangiwa JK si demokrasia?

  Nikiona watu wanataka kumsema JK kwa non issues naona wanaharibu ujumbe wa wale wanaoweza kumbeza JK on the merit.Mwishowe watafanya wote tuonekane wale wale tu, walalamishi wa upinzani ambao hawana shukurani.

  Folks, kama hamuwezi kufanya homework na kuja na solid criticism kuhusu Kikwete bora kaeni kimya, ama sivyo kwa criticism zingine zisizo kichwa wala miguu, badala ya kumuangusha JK, mtakuwa mnampandisha chati bure tu.
   
 11. K

  Kapwani JF-Expert Member

  #11
  Jun 23, 2010
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu hapa wala hatujadili mapenzi na hisia za watu kwani hata hivyo hazitusadii kwa namna yoyote ile. Mimi nilijaribu kuweka haya mambo na perceived impacts zake. Nadhani sina tatizo na watu kumpenda kiongozi wao.
  Mimi hata kama ningekuwa na mgombea yangu nisingemshauri afanyiwe mbwembwe hizi ambazo mkuu anafanyiwa kwa sababu naona madhara yake baadae. Hofu yangu ni jambo hili kufanywa na watu wanaotaka kunufaika baadae kisiasa au kiuchumi...nina amini aliyewaoganaizi watoto wa maandazi huenda anatarajia apate nini baadae ...sasa wanafiki watatumia loop hole hizi ila waje walipwe vyeo ambavyo hawana uwezo navyo....
  mix with yours
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,200
  Trophy Points: 280
  1. Huwezi ku prove kwamba wanataka kunufaika kisiasa na kiuchumi.
  2.Kama unaweza kuprove miongozo ya campaign inasemaje kuhusu hilo, kama halina miongozo inayofaa unafanya kazi gani kuhakikisha hili linatokea?

  Ni lazima tujifunze kuheshimu utawala wa sheria na kuachana na mambo ya speculations. Hata kama unayoyasema yana ukweli, huwezi kuwashinda kama hakuna sheria inayokataza, cha kufanya wasiliana na mbunge wako (most probably wa CCM) uangalie uwezekano wa kutunga sheria inayokataza haya mambo

  Au kama vipi fanya ingia bungeni mwenyewe.Kulialia kwa kitu ambacho hakikatazwi kisheria na wala huwezi kuprove madai yako ni upuuzi.

  Huwezi ku run nchi kwa morals ambazo hazina misingi iliyo well defined.Next thing utasema nini, wanaochangia kampeni ya CCM wote wana ajenda ya kutafuta ulaji?
   
Loading...