Hii mistari kwenye nyimbo za hiphop haileti maana

magnifico

JF-Expert Member
Jan 14, 2013
9,903
21,199
Bila shaka umeshawahi kusikia mstari fulani kwenye wimbo fulani wa miondoko ya Hip hop ambao ukiutafakari unakua hauna maana au hauusiani kabisa na maudhui ya wimbo husika.

Mimi nimewahi kukutana na hizi:

1."Good life ndio mi nataka muulize Kanye West Lamborgin Mess Barcelona".

Izzo bizness - Tummoghele.

Sijaona muunganiko hapo, Labda wenzangu mnieleweshe

2."Mama alikua na happy coz sikupata kasoro, Najua haujui wapi ilikua mji kasoro"

Stamima - mr boniventure

kwenye intro jamaa anajitapa kabisa "It's moro town baby..Home sweet home".. Au tuseme alikua anakumbushia?

3."Tatu bila kubali matokeo punguza hasira, hadi mechi inaisha hawagusa hata mpira".

Tmk wanaume halisi - Tatu bila.

Kwamba wakifunga goli mpira kati wanaanzisha wenyewe? Au walikua wanacheza pool table wanapiga WASH tu au sio?

4."Wasanii kurogana, siku hizi ishakuwa fasheni"

Izzo bizness - Mr. christmass.

Tuseme ni kweli ila ina mahusiano gani na Mr. christmass?
 
Wasanii wa Zamani walikuwa na uwezo mkubwa mno wa ku-stick kwenye Mada usika wimbo mzima wenye verse tatu bila kuchanganya Mada Ila watoto wa siku hizi Wimbo mwanzo mwisho anajisifia tu hujui Hata main concept ya wimbo.

Mtu kama Jay Moe,Professa Jay,MwanaFA,Fid Q etc wa Zamani anakupa story ile ile kwenye verse zote tatu bila kutoka nje ya Mada wala kujisifia kiboyaboya.

Kwa miaka hii Mtu kama Songa sioni mwingine mwenye uwezo huo.
 
Wasanii wengi wa hip-hop huwa wanaongea vingi visivyoleta maana, cos wanajua mashabiki wao wengi vilaza kama wao. They would say whatever long as it rhymes. Notorious B.I.G anazo nyingi sana kwenye nyimbo zake, Nas, Prof J, Masta Ace, Navio, etc.

Binafsi naamini Lil Wayne anamshinda Bjggie Smalls, cheki hii; "b!tch n!ggas go behind your back, like nun-chucks/ and that's effed up". When a nun-chuck goes behind your back, it's for protecting YOU, period.
 
hahaha acha hizo, Vipi hii ya Diamond "Na Mbuzi wa kutaga".?
 
Back
Top Bottom