Hii miradi siyo ya Hayati Magufuli, ni ya nchi. Waziri Makamba kuwa makini sana

hizi nchi zetu za dunia ya tatu zina shida sana, hao wenye nchi zao (kama kweli wapo km unavyodai) ni heri wangejikita kutengeneza taasisi imara watasaidia sana badala ya kuweka mtu mmoja ainyooshe nchi haitasaidia chochote maana mtu hadumu km tulivyoona ila taasisi zipo milele,
Umesema vyema brother.
 
Hahahahaha..halooo ooohh..daawaa imeanzaa kuwaingiaa sasa..yaan mnazungukaa tuu..ukwel ni kwamba ndani ya mioyo tenu mnakubali sana JPM..ila ndo hvyoo yaan kawaumiza sana ambao mlikuwa hamna vyeti halisi..mliokuwa majambazi na majizi...
JPM was a real man..mutu na nusu
Hata JPM mwenyewe alikuwa na matatizo ya vyeti FEKI kwa ile PhD yake na kwa UWIZI ndiyo kaweka rekodi. Tsh 2.4 Trillion kwa miaka 2016-18. CAG alipohoji akafukuzwa kazi
 
Vijana mlioingia siasa 2015 ni kama mtoa mada
Jifunze kwanza kabla ya kuandika
Wanaokulipa ni kama wewe wageni kwenye ccm
Hii nchi kubwa Fatma
 
Miradi mingapi anasimamia January
Januaru mradi mmoja ila mtoa mada anasema miradi kana kuambiwa Januari ninwaziri Mkuu
 
Yaani unasema ungewa wewe ungeipiga chini Sgr na bwawa la umeme..Kama nani?yaani hera zote zilizoteketa utwambie kwa kuwa miradi ilianzishwa na magufuri basi iachwe..harafu sisi tukuangalie tu ..wewe kama nani?
Pole sana unakumbuka mwalimu pia kuna siku alijenga viwanda katika taifa lako?,aliweka nidhamu kwa watumishi kama alivyodai,akapambana na rushwa na umasikini lakini leo hii mko wapi? napokueleza kupiga chini,I mean to retreat.Eti sgr sijui bwawa la umeme.Wewe unaweza kuendesha hiyo SGR unayolilia.Hivi Magufuri aliporetreat katika project ya mwendokasi kuna siku ulikuja kuuliza alifanya kama nani?

Anyway,kama unauliza ntafanya kama nani,jibu ni jepesi ntafanya kama mimi.
 
Nachojua January ni very smart. Na akisimamia project anaisimamia Kwa uweledi mkubwa (refer mifuko ya plastic). Hii habari ya kufanya mambo Kwa haraka na mihemko saa zingine ni hasara Kwa Taifa. January atafanya vyema na mambo yatakuwa sawa.
 
Nachojua January ni very smart. Na akisimamia project anaisimamia Kwa uweledi mkubwa (refer mifuko ya plastic). Hii habari ya kufanya mambo Kwa haraka na mihemko saa zingine ni hasara Kwa Taifa. January atafanya vyema na mambo yatakuwa sawa.
Umekaririshwa? Na ndo maana unadanganywa kuwa hakuna crane ya kunena tone 26 , na Wakati site zipo zinazo beba hadi tone 50
 
Suala la kuwa ni serekali ya majizi ya kura, wala sihitaji ww udhibitishe hilo, maana hivyo ndivyo ilivyo regdless unakubali hukubali.

Tuje kwenye hayo maelezo yako ya kutaka kusifia mtu na sio mifumo. Tuanze na reli ya SGR, hiyo reli kipande cha Dar-Moro alisema itakamilika Nov 2019, je mpaka anafariki hicho kipande kilikuwa kimekamilika ambapo ni ni mwaka na zaidi? Unatarajia muujiza gani kwa wale ambao walikuwa sio sehemu ya maamuzi yake. Mgao wa maji, yeye angekuwepo angefanyaje iwapo hakuna mvua, na hakuna water reserve yoyote kukabiliana na hali hii? Alipoingia madarakani 2016 kulikuwa na ukame mkali na mgao wa maji ulikuwepo pia, yeye alifanya miujiza gani?

Unapotosha kuwa malori yalikuwa yamefichwa sasa yamerejea kwa kasi, ni kwamba hiyo SGR ilikuwa inafanya kazi hayo malori yakaaondoka, na sasa hayupo treni imesimama ndio malori yamerudi ama? Unasema hujui kama SGR itaisha, yeye alikopa zaidi ya 15y+, mbona hakumaliza hiyo SGR & SG respectively?

Unasema Tony Blair alikuja hapa nchini kutushauri, kwahiyo alikuja kutushauri tuwe na mgao wa maji na umeme!? Toka lini ushauri ukawa shuruti kwa viongozi wetu? Au unadhani wote ni hamnazo kwa kuchomekea sababu zisizo na kichwa wala miguu?

Arrogance kwenye taasisi za serikali imerudi tena, kwani iliwahi kuondoka au uhuru wa vyombo vya habari tu uliminywa kuripoti habari hizo negative? Kama kuna tofauti, basi ni ndogo sana kwa yeye kutokuwepo. Kwani hatukuona watu wakitekwa na kuuwawa, bila kupata majibu ya mambo hayo? Tulishuhudia chaguzi za kishenzi na kihayawani chini ya tume ya uchaguzi, au hiyo tume ya uchaguzi sio taasisi ya umma? Huenda unachanganya ufanisi na hofu+ maigizo. Bei ya mafuta ya kula na petroli yalipanda maradufu wakati wake, ajira kulikuwa hakuna nk. Au ni ubora gani unaongelea?

Gazeti la financial times limeanza kutusifu tena, kwani likitusifu sasa kuna ubaya gani kama wanaona utawala wa kishenzi umeondoka? Isitoshe gazeti la Financial Times lina madhara gani hapa nchini wakati halina hata wasomaji? Mbona magazeti ya uhuru, habari leo nk yanayochwapwa hapa nchini na kusomwa hadi sasa, yanasifia kwamba mambo ni mazuri toka utawala huu uingie? Je tukuamini ww na sio hayo magazeti ya serikali yanayosema mambo ni mazuri? Kama kweli unasema mambo ni mabaya hadi unashangaa financial times kuisifia nchi yetu, mbona kinachoandikwa na magazeti ya ccm na serikali kusifia hali ni nzuri hakikushangazi?

Wakati anapora na kunajisi chaguzi, huku akiharibu mifumo ya kuhoji mliona anafanya kitu cha maana. Hatimaye amefariki akiwa ameua mifumo ya kuhoji,mambo yanazidi kuharibika kwa kasi na hakuna mwenye uwezo tena wa kuhoji, badala ya kujiuliza tumefikaje hapa, mnaanza kuchomekea sababu za uongo ili kumsafisha mtu muovu! Unashangaa rais muovu kusemwa, kwani alikuwa mtu muadilifu, Nape si alitolewa bastola hadharani akiwa waziri, alichukua hatua gani kama alikuwa kiongozi mzuri? Je ni kiongozi au binadamu gani asiyesemwa? Au kwako yeye alikuwa Mungu? Kama alikuwa hataki kuambiwa ukweli, ulitegemea watu wasimsungumze huko pembeni? Huu ujinga wa kutotaja kuambiwa ukweli naona kauacha kwa wengine, Ndugai naye kaambiwa ukweli anaanza vitisho vya ulevi wa madaraka.

Tunaposema tunataka katiba mpya tunamaanisha, bila kuwa na mifumo bora. Kama kungekuwa na katiba bora yale mazuri yake yangebaki, na uchafu wake asingepata nafasi ya kuufanya. Lakini badala yake, mazuri yake yametoweka, na uchafu aliopandikiza ndio umechukua nafasi. Amka dai katiba mpya itakayolinda mifumo, na sio kuamini mtu anayeweza kufanya mazuri machache na maovu mengi.
Hoja zako ni dhaifu mno Wala hakuna haja ya kuzijibu
 
Back
Top Bottom