Hii mikoba jamani! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii mikoba jamani!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by PSYCHOLOGY, May 10, 2011.

 1. P

  PSYCHOLOGY Senior Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: Feb 10, 2011
  Messages: 177
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari members JF...!
  Naomba kujulishwa kwa yeyote alie ona ukweli wa hii mikoba ya akina mama/baba utakuta mtu/me au ke ameubeba mkoba utadhani anasafiri kumbe anaenda kazini tena atakuepo huko kazini kwake kwa masaa kumi au tisa.
  Najiuliza hua inabeba nini?
  Maana kuna hospitali moja hapa mjini alikuepo dada mmoja kila siku anakuja home mkoba wake umejaa mashuka nets mikate maziwa... Hivyo hivyo kwa baba mwingine. Mbali na mikoba ya laptop...
  Si kwamba nawachukia...kama ni uzito wa mikoba wanabeba wenyewe.
  Nawakilisha!
   
 2. d

  digodigo Senior Member

  #2
  May 10, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kama ni wanaume wanabeba documents mbalimbali muhimu kama id, diary,notebooks na vitu vingine vinavyomsaidia kazini na kwa upande wa kina mama ni kama manukato,tissue papers (anything might happen) kanga mobile phones,pochi nk
   
 3. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  ...siku moja nlimshangaa dada mmoja ameingia kwenye dala dala ana mkoba wake mkubwa...mbaya zaidi akaniwekea kichwani kwangu...nikawa napenda nipate thawab za kumbebea mzigo wake.
  Tena alikua dada wa kimjin mjin...sikujua kwanin amenibebesha!
   
 4. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Hujaeleweka maalim, yani alikuwekea kichwani na wewe ukakausha tu?
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Inabeba mahitaji ya mbebaji!!!
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  May 10, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mikoba inashughuli nyingi; usione imebebwa tu... Ooh!

  Kwa mfano kwa kina mama ukiacha vitu muhimu kama vile Khanga, pamoja na zile kinga zao za mzunguko wa kila mwezi, utakuta pia kuna uturi, podari, sare za kazini... Wapo wanaobeba kwa nia njema kama vile viji zawadi vya watoto wakati wakitoka kazini au matembezini.... Usishangae kukuta ndani ya mkoba kumefichwa visheti, kaimati, sikirimu au ramba ramba na bagia.... Ukipekua sana utakuta tooth pick... vipande vya toilet paper na wakati mwingine hubeba biashara ndogondogo za kuuziana maofisini.

  Wale wanaobeba vipodozi hawa wako wengi tu na ikifika wakati utashangaa kwani hata kama yuko ofisini hujisahau kabisa akidhani yuko chumbani kwake jinsi anavyojiremba na na kujipodoa inafurahisha anapokosa kioo cha kujiangalia utamuona akitumia kompyuta bila shaka... au atakuuliza vipi XP nipo poa eeh!?

  Kuna mshairi mmoja ameandika haya:

  Mkoba wa mkononi, kwa kina mama hadaa
  ukimuona njiani, mbwembwezake ni balaa
  Akiufungua ndani, wallahi utashangaa

  Wale wendao kazini, yanini kuuchukua
  Nauli imkononi, imevunyangwa sawia
  Mkoba wa kazigani, mahangasha kujitia

  Akijapita mahali, alivyoukumbatia
  Utadhani muna mali, aogopa kuibiwa
  Kumbe muna miambili, na wanja kujipodoa

  Harusini kiwaona, kilamtu pekepeke
  Ni aina kwa aina, kwa kila mtu na wake
  Aringa na kujiona, ati ni mzuri wake

  Ata kama ana begi, safari akimbilia
  Na huku ana mashungi, mwilini yaning'inia
  Ni lazima handbegi, nayo kijipachikia

  Hebu siri nambieni, enyi mnaoibeba
  Mikoba ya mkononi, kwa nini mna mahaba
  Ijapo mwendasokoni,kununua ngogo miba

  Ukweli nielezeni, wala msifiche kitu
  Mkoba wa mkononi, ni lazima kila mtu
  Uutundike kwapani, japo ndani hakuna kitu

  Tamati sasa naona, Kalamu naweka chini
  Kina mama wasichana,na mtie akilini
  Kama hakuna la maana, mkoba wacha nyumbani.
   
 7. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #7
  May 12, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Hujanielewa wapi?
  Nilketi kiti cha m2 mmoja..nae dada huyo kaingia na hilo koba lake...kwa kua kulikua na abiria wengi...nae hakuweza kulibeba uzuri...ndipo akaliegesha juu ya kichwa changu...nikatulia tuli!
  Au ww hujawahi kupanda dala dala iliojaa?
   
 8. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #8
  May 12, 2011
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  ....nimecheka karibu mbavu kupasuka/kuvundika!!!!
  Hee hee hee...nimependa hayo mashairi.
   
Loading...