Hii migogoro ya Amani kwanini Inashamiri sana Bara la Africa na Asia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii migogoro ya Amani kwanini Inashamiri sana Bara la Africa na Asia?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Zipuwawa, Dec 7, 2010.

 1. Zipuwawa

  Zipuwawa JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2010
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 3,052
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 145
  Ni muda mrefu sana nimekuwa nikijiuliza kwanini migogoro mingi inaikumba Bara la Africa na Asia kwa sana, watu kuuana na wengine kuachwa vilema kwa vita vya kila siku.Ukiangalia Asia kama Lebanon,Izrael, Syria na nyingine nyingi kila siku ni mizozo isiyoisha.
  ukija Africa ndio limekuwa takataka za nchi za magharibi kujipenyeza na kujikuta kila siku tupo kwenye machafuko mfano angalia Congo, Ruanda,Burundi,Zimbabwe,Namibia na kwingineko.

  Kwanini Bara la ulaya wao muda mwingi wanajikita kwenye maendeleo wakati sehemu nyingine zinafanywa sehemu za Vita na wao kujiita kama Wasuluhishi wakubwa? Ni lini Waafrica watajua nini Kisa cha Migogoro yao? Au ndio hakuna wa kumshika mwenzie mkono?

  Leo hii Obama anapinga matokeo ya Rais Wa Ivory Coast na nchi nyingi za maghalibi....je nini wanachofaidika nacho?
  [​IMG]
  Afisa mmoja wa ikulu ya White House amesema rais Obama anamzingatia kuwa Bwana Ouattara ndiye aliyeshinda uchaguzi huo kihalali.
  Rais wa zamani wa Afrika Kusini,Thabo Mbeki, anatarajiwa kuwasilisha ripoti kwa umoja wa Afrika baada ya siku mbili za kujarbu kusuluhisha mgogoro huo nchini Ivory Coast.
  Jumuiya ya kiuchumi kwa mataifa ya Afrika magaribi ECOWAS ambayo pia imemtangaza bwana Ouattara kuwa mshindi, inatarajiwa kuandaa mkutano maalum hivi leo Jumanne nchini Nigeria.
  Jana Jumatatu, umoja wa mataifa ulisema unawaondoa japo kwa muda yapata wafanyikazi wake 500 wanaotoa huduma zisizokuwa za lazima kutoka nchini Ivory Coast kutokana na mzozo huo.

  Hili la Ivory Coast ni miongoni mwa machache yanayojiri Barani Africa. Wakati Asia kila siku watu wanaishi kwa hofu wasijue lini watakuja kuishi kwa Amani wakatio wao ulaya ni
  furaha kila siku ukikuta wapo kwenye matatizo ya amani si kama yetu.
   
Loading...