Hii michango itayochangishwa si sababu ya Royal Tour, hawa vijana wa Kiholanzi wanaujua Mlima Kilimanjaro tangu enzi na enzi

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,125
4,168
Raia wa Uholanzi zaidi ya 40 wameanzisha mbio za baiskeli kuzunguka mlima Kilimanjaro kilometa 400 kwa ajili ya kuchangisha fedha kusaidia sekta ya afya nchini.

Mbio hizo za baiskeli zijulikanazo kwa jina la ‘Africa Classic’ zimeratibiwa na Shirika la Amref Netherlands kwa kushirikiana na Amref Tanzania na zinalenga kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia huduma za afya.

Akizungumza leo Jumapili Juni 12, 2022 katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa bodi ya Amref Health Africa, Anthony Chamungwana amesema mbio hizo za kuendesha baiskeli zilianza rasmi mwaka jana ambapo wamekuwa wakifanya kila mwaka kwa ajili ya kuchangisha fedha kusaidia sekta ya Afya Tanzania na mafanikio makubwa yameonekana.

uholanzi.JPG
 
Back
Top Bottom