Hii methali ina maana gani?

Farolito

JF-Expert Member
Sep 10, 2018
11,634
26,369
Wakuu,
IDD Mubarak!

Nini maana ya methali 'Mkaidi hafaidi mpaka Siku ya Idd'?

Ahsante.
 
Ina maana kuwa mtoto mtii kwa mzazi atapewa vinono kila vitakapopatikana lakini mwenye kiburi atakula siku za sikukuu tu. Mama anaweza kuficha kitu kizuri ili ampe mtoto mtii kwake. Lakini mtoto mkaidi atakula vinono siku za sherehe tu maana hapo kunakuwa Hamna namna ya kumnyima.

Methali hii hutumika kumsema mtu jeuri ili ajue kwa ujeuri wake huenda akakosa mazuri mengi.
 
Asante kwa ufafanuzi mkuu
 
OK kwahio ukamilifu wake ni "Mtoto mkaidi hafaidi mpaka Siku Idd"
Asante
Alitakiwa kuanza na nomino ya mtoto mkaidi ......

Nadhani siku hizi hawafundishi methali. Ni aibu sana.
 
Ina maana kuwa mtoto mtii kwa mzazi atapewa vinono kila vitakapopatikana lakini mwenye kiburi atakula siku za sikukuu tu. Mama anaweza kuficha kitu kizuri ili ampe mtoto mtii kwake. Lakini mtoto mkaidi atakula vinono siku za sherehe tu maana hapo kunakuwa Hamna namna ya kumnyima.

Methali hii hutumika kumsema mtu jeuri ili ajue kwa ujeuri wake huenda akakosa mazuri mengi.
Asante kaka
 
Back
Top Bottom