Hii maneno niiweke fungu gani ? Ni kudhalilishwa/nyanyaso/vituko au hakuna jibu sahihi ? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii maneno niiweke fungu gani ? Ni kudhalilishwa/nyanyaso/vituko au hakuna jibu sahihi ?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Judgement, Dec 14, 2011.

 1. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Ilikua ni siku ya Jumamosi tupo harusini na muda husika niuzungumzao ni tulipokua ukumbini, harusi ambayo mmoja ya mdau mwenzangu kazini alikua anaoa.
  Mimi na mama ya boma yangu (wife) ni miongoni mwa wageni waalikwa, shughuli iliendeshwa vizuri kwa mujibu wa ratiba ilivyoainisha tulikunywa tukala kama ilivyo ada.
  Ukafika wakati wa muziki mimi nilim'nyanyua wife nikacheza nae takriban nyimbo mbili, wife alikua akicheza kwa style zake za kawaida kama nilivyozizoea sikuona kipya tukarudi kukaa vitini kuendelea na vinywaji huku tukiwaangalia waalikwa wenzetu wakiendelea na miserebuko, ghafla akatutokea mdau mwenzangu wa kazini ambae na wf wangu anam'fahamu (kwa taarifa huyu kijana yeye bado hajaoa) japo kwa marika mimi na yeye hatupishani sana.
  Huyu mdau akaniomba akacheze na shemejie, na kwa dunia ya leo ya (global, dotcom,twiter e.c.t) si rahisi kulikataa suala kama hilo! Nikam'ruhusu wakachezenae, ambapo eneo walilokua wakicheze ni mbele ya meza tuliokua tumekaa nilichokishuhudia hapo sikuamini macho yangu vizuri ni kwamba wife wangu alikua anakata MAUNO ya nguvu! MAUNO ya ukweli ! MAUNO ambayo sijapatapo kuyaona hapo kabla, MAUNO! alikua anakatika kama umuanavyo "funza wa chooni" au kuzidi! tangu nimuoe sikuwahi kujua kama mama ya boma ni mkali wa kucheza kivile. Sio siri kisukari changu kilipanda ghafla nikijiuliza kama wife wangu ni mkatikaji kivile mbona hata siku 1 hajawahi kunikatia mie mumewe? Na iweje mikatiko ile akakatikiwe mdau ? Mdau ambae hata kuoa hajaoa? Hata wife anaelewa hivyo? Aidha iwe ameoa au bado still sioni reason yeyote ile mdau au nje ya mdau atakaekua na right ya kuchezewa MIUNO ile tofauti ya mie MUEKEZAJI !
  Nilitamani nikawakatize kabla nyimbo ile haijaisha lakini namshukuru Mungu nilifanikiwa kulidhibiti hilo, na wimbo ule ulipokwisha sikuhitaji tena kuendelea kuwepo ukumbini pale, nilimwambia tuondoke kidogo akataka kuleta ubishi na aliponiona sitanii naelekea kutoka huku nikimuacha akanifata, njia nzima tukiwa garini ni ukimya ndiyo ulitawala.
  Tulipofika home ndipo nikaiweka agenda mezani nikitaka maelezo toshelevu dhidi ya kadhia nzima ya kile kisicho cha kawaida nilichokiona ukumbini (MAUNO YA HATARI KWA MDAU) Jibu alilonipa namnukuu "Wewe ndiyo hua hunichezeshi kuendana na bit za nyimbo! Hua unacheza slow-slow namie ndiyo inabidi niende slow! Yule jamaa yako alikua ananichezesha kwa kasi ya bit ya nyimbo na ndiyo maana namie nikawa naenda kasi"
  Wadau je? Hizo ni sababu toshelevu kweli kwa wife wangu kumuonesha maufundi na maujuzi ya MAUNO shemeji yake? Hapa kweli mtaniambia mambo ya "inferiority cmplx?" sijanyanyaswa/sijadhalilishwa hapa? Au kuna "behind the curtain" between mdau with my wf?
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hata mimi nilitaka kukupa jibu alilokupa mkeo.Yani yeye anacheza na wewe vile unavyoonyesha unataka, kama hukuwahi kumtaka akatike kabla, wala hukuwahi kumuuliza kama shughuli anaiweza basi sioni kosa lake. Though alitakiwa ajidhibiti kidogo hapo ukumbini, kosa la kutokukuchezea wewe sio lake maana pengine hata hujawahi kuonyesha kwamba uko interested na mauno yake.

  Anza sasa kumchezesha ili siku nyingine asije akadata na wadau kwa kukosa uwanja kwako.
   
 3. m

  mzabzab JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2011
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 6,981
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  tulizana bana...wewe wewe mwenyewe ulishasema unakisukari kweli miondoko ya vijana utayaweza?
  kubaliana na maelezo ya wife na siku hiyo watu wanataka kujimwanga na ku-enjoy so atizo nini. potezea tuu
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  alikua anakuonyesha talents acha wivu
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  H ha ha ha, unaleta miondoko ya 80's kwenye twita na fesibuku?
  Afu inawezekana huwa unamboa sababu hujui kucheza ila hawezi kukukatalia sababu wewe ni mumewe.
  Kachukue twisheni ya kudansi somewhere
   
 6. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #6
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  Una mke mzuri sana, mkweli! Kazi ni kwako, badilika baba. Washa king'amuzi, muambie akufundishe jinsi ya kucheza nae. Japo nna wasiwasi kuwa maybe huoni mauno yake wakati ukidance nae? Afu uwe unampeleka club mara moja moja, manake kudance na mauno kwenye harusi naona kama sio vile, kuna hadi babu wa bi harusi hakawii kudhani mamaa ya boma yake mekatika center bolt,lol
   
 7. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #7
  Dec 14, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  jibu alilokupa mkeo ni sahihi kabisa, ingawa pengine alitakiwa acheze kwa kiasi (maana kwa vyovyote lazima ajue utaona wivu) tena una bahati ya kupata mke muwazi
  badala ya kujiuliza kama mkeo kakudharau au la ingia mzigoni, jifunze nyimbo za aina mbalimbali, miondoko yake
  badala ya kucheza kwa style mlizozizoea, tena unaweza muomba akufundishe au nendeni mara moja moja sehemu za starehe mkajifunze mitindo mpya.

  :kev::msela:
   
 8. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #8
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  LIZZY ! Comments zako nimezipima na kuzidurusu twicely! Evenif unaonesha uko fair but there some minor elements unaonesha kama unampa wf pande kubwa la haki than me! Bt ningejua gender yako (Lizzy) ingenisaidia kuelewa vema kama uko fair 100% au una fever upande wa gender yako.
   
 9. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #9
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Mzabzab ! Ile miuno mtu wangu ungeiona mmh! Hata "under the Net" sijaiona! ol to ol yaonekana wewe uko gendar tofauti na mimi mlalamikaji! Ungekua na gendar kama yangu lazima ungekunja uso ktk hili.
   
 10. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #10
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  BADILI TABIA! Ushauri wako ni wa kiume! 100%
   
 11. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #11
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  KONGOSHO! umeongea NENO!
   
 12. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #12
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  MTM ! "TALENTS" sina tatizo na hilo, basi talents si zianzie kitandani? Rejea "charity begin at home" au?
   
 13. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #13
  Dec 14, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  ubaba na mfumo dume umetuzidi wanaume mnooo, bado ktk karne hii tunambana mno mwanamke na ku ignore hisia zake. mkiwa home unataka akuogope na kukunyenyeea km mungu. sikiliza miuu achana na mambo ya kizamani ndoa lzm iwe funny bana mimi nikiwa room na wife mziki ukipigwa ntacheza freely ntamvuta tutacheza mzuka ukimpanda atakatika vilivyo, hiyo ikemfanya awe huru kwenye sherehe tukicheza mpaka watu wanapenda. so kamanda kuna mwenzio alikwenda kumpick wife wake kazini kwao jioni wakati anamsubiri reception alipogeuka kulia aangalie ofisi ile vizuri macho yalipenya kwenye kioo kwa mbali akamuona wife wake akikatika sebene na wadada wawili mithili ya stage show ya kofi olomide. jamaa hasira zikampanda akaondoka, wife alipokuja reception hola jamaa hayupo alipompigia jamaa likatia endelea kucheza mziki. ugomvi uliendelea wiki mbili mpaka yule dada alipoamua kumpasulia jamaa kwamba yeye ni mpenzi wa muziki km home ni tv tuu tena supersport taarifa ya habari sijui cnn yeye ata refresh vipi? jamani hawa wenzetu wana mahitaji yaoctusi ignore sababu eticni mkeo. communication imekuwa tabu mnoo! ni amri tuu, kukunjiana sura. endelea kumchekesha kuongea naye kimahaba. chunguzeni wake za watu makazini mara nyingi utakuta ana ukaribu sana na ka bachelor flani utani mwingi vicheko anajua akirudi home ni amri tuu
   
 14. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #14
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sasa kaka hapa unalia wivu au unaonauchungu kua wewe huja sakatiwa hilo buno wakati wewe ndio mdau? tatizo nadhani hujakaa na mkeo mkaulizana yeye anapenda vp na wewe unapenda azungushe vp, mkishajuana isingekupa shida, lakini usijali nnaimani huo sio mualiko wa mwisho,mkienda sikunyengine au niseme kuanzia sasa mabuno yote hayo yako mwambie aanze kukumwagia mauno kuanzia kwenye sita kwa sita,kosa lako kaka japo utakata mda wote huo unalala nae unaamka nae hujui kama mambo anayaweza?
   
 15. sister

  sister JF-Expert Member

  #15
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 9,028
  Likes Received: 3,940
  Trophy Points: 280
  binafsi nadhani bidada alibidi akuambie apendacho cz uwez jua kila kitu anachopenda mpenzi wako, mlishahudhuria harusi nyingi nadhani na kama unavyomchezesha apendi basi angesema mume wangu nichezeshe hivi, hafu kwenye harusi c sehemu ya kukata mauno pale watu mnabidi muwe wastaarabu unacheza kama hautaki vile. tatizo tulikuwa nalo uwa atupendi kuulizana na wapenzi wetu vitu tuvipendavyo uwa tunajaribu kutafuta tu wenyewe kwamba mpenzio anapenda nin na sio kila kitu unaweza kujua. na wew kaka usione aibu kumwambia mkeo kama unapenda viuno kwenye mambo fulani. binafsi uwa namuuliza mpenzi wangu anachopenda na achotaka nimfanyie tukiwa kwenye mambo fulani. LOL
   
 16. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #16
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  CHIMUNGURU! Thanks mkuu mwenzangu! Comments yako umefikiri na yakufanyia kazi.
   
 17. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #17
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  SISTER! Hakika ushauri wako umetulia!
   
 18. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #18
  Dec 14, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Hapa kuna mambo yafuatayo;mosi-tatizo ni la mkeo,yaani iwe iwavyo mwanamke yoyote ambae ni mchumba/girlfriend/mke wa mtu lazima ajiheshimu anapofanya lolote,namna alivyokatika sio sahihi hata kama hakunachoendelea baina yao,sio kila jambo anafanyiwa kila mtu au kila mahali.Pili-wewe ni tatizo,kwanini unachukulia mambo kinegative sana?Kwanini usifikirie kuwa yale mauno alikua anakuonesha wewe badala ya mdau japokua hakutumia njia sahihi?
   
 19. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #19
  Dec 14, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  ARABIAN FALCON! Sihitaji ziada ya details kufahamu kwamba una uwezo/upeo wa kupambanua issues!
   
 20. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #20
  Dec 14, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Pole sana mkuu,
  Hukua na haja ya kutoa povu kihivyo,
  Pale,ungeonyesha maujuzi tu,walipomaliza ungeenda kuunga pale nawe ukampeleka kwa speed anayotaka na mamnjonjo kibao mpaka unamfunika mdau,
  Yani ungemfanya afurahi zaidi na wivu wako usingeonekana kbs,
  Jitahidi kuwa muwazi na punguza ubabe ili awe huru kujieleza kwako ni vp anapenda hata huko kwa bed uoneshwe mauno,
  Nampongeza bidada kwa kuvunja ukimya na kumwaga radhi hadharan uone coz inawezekana huko hm unakuwa serious mda wote na hapati nafasi ya kujiexpess km alivyofanya ukumbini.
   
Loading...