Hii maana yake nini? Mwaka jana na juzi mtaani kwetu maendeleo yako kasi sana...

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,569
15,298
Katikati na mwishoni mwa awamu ya JPM

1: Ninashangaa kuona mtaani watu wanajenga nyumba hadi wanahamia bila kupumzika.

2: Jamaa wamefungua mahardware,maduka ya madawa, salooni kali, Bucha, Bar, carwash na nyumba za kulala wageni.

3: Vituo vya bodaboda viwili vikubwa ambavyo miaka mitatu iliyopita zilikuwa kama boda mbili tu na mwisho saa mbili.

4: Miaka mitatu iliyopita hakukuwa na kituo cha mafuta, leo viko vinne karibukaribu.

5: Shule za chekechea za kisasa kama nne hivi, na moja imefufuliwa hivi karibuni.

6: Mama ntilie, wauza samaki, kijiwe cha kahawa, maduka ya vyakula vya mifugo, welding ,magenge ya nyanya na maduka ya vitu vya nyumbani nayo yanamushroom kila kukicha.

Je, tukichukua hii kama sample, mipango ya hayati JPM ilikuwa inaanza kutunufaisha watanzania kidogo kidogo.
Je, yajayo yalikuwa yanaanza kufurahisha?

Ukiangalia Google map ya 2015 na ukipiga picha ariel view kwa drobe/hericopter au ndege utashangaa mabadiliko makubwa sana hasa miaka hii ya mwishomwisho.

Wakuu ni juhudi zetu tu au ndio matunda ya mikakati ya uchumi ya Hayati JPM
 
Kweli mkuu.

Viwanda vya kufyatua tofali vilivyo activr kabisa zaidi ya vitano. Trna kimoja kimeanza Muda sio mrefu uwanja mzima umejaa tofali na vifuso vinapishana tu kuelekea site.
 
Ukitaka kuelewa tafuta connection au conect dot kati ya mmoja ya hao watu na consiparacy ayko ya hayati nenda kamuulize hivi serikali mipango hii imekuwezeshaje wewe kufika hapa.
 
Katikati na mwishoni mwa awamu ya JPM

1: Ninashangaa kuona mtaani watu wanajenga nyumba hadi wanahamia bila kupumzika.

2: Jamaa wamefungua mahardware,maduka ya madawa, salooni kali, Bucha, Bar, carwash na nyumba za kulala wageni.

3: Vituo vya bodaboda viwili vikubwa ambavyo miaka mitatu iliyopita zilikuwa kama boda mbili tu na mwisho saa mbili.

4: Miaka mitatu iliyopita hakukuwa na kituo cha mafuta, leo viko vinne karibukaribu.

5: Shule za chekechea za kisasa kama nne hivi, na moja imefufuliwa hivi karibuni.

6: Mama ntilie, wauza samaki, kijiwe cha kahawa, maduka ya vyakula vya mifugo, welding ,magenge ya nyanya na maduka ya vitu vya nyumbani nayo yanamushroom kila kukicha.

Je? Tukichukua hii kama sample, mipango ya hayati JPM ilikuwa inaanza kutunufaisha watanzania kidogo kidogo.
Je, Yajayo yalikuwa yanaanza kufurahisha?

Ukiangalia Google map ya 2015 na ukipiga picha ariel view kwa drobe/hericopter au ndege utashangaa mabadiliko makubwa sana hasa miaka hii ya mwishomwisho.

Wakuu ni juhudi zetu tu au ndio matunda ya mikakati ya uchumi ya Hayati JPM
Siku zote hata ubane vipi kuna watu huwezi wagusa au wana mbinu mbadala. Mfano kipindi kile wakati watu wanalalamika vyuma kukaza 2018/2019 hapa mtaani kuna jamaa kanunua kiwanja kilichokaa kwa miaka kadhaa baada ya kukosa wateja 50 mill. Alikaa miezi mitatu baada ya kununua kashusha ghorofa bila ya kusimama hadi imekamilika na fence hadi maua ya bustani.
 
Back
Top Bottom