Hii lugha ya kuwa nchi ilikuwa imefika pabaya inakera na ni ya kejeli

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,818
5,007
Habari wakuu!

Bila shaka kila MTU amekuwa akisikia lugha hii ya kwamba nchi yetu ilikuwa imefika pabaya. miongoni mwa watu wanaopenda kuongea hivi yumo pia Rais wetu na viongozi mbalimbali.

Cha kushangaza na cha kujiuliza ni watu gani hao walioifikisha nchi yetu kwenye hali mbaya? wako wapi, nchini, nje ya nchi, au wamekwishafariki?

Nasema lugha hii inakera na ni ya kejeli kwa sababu wanaotumia lugha hiyo ndio kikosi kile kile kilichokuwa serikalini, kilichobadilika ni kubadilishana nyadhifa lakini bado ni wale wale.

ndio maana Leo utasikia nchi ilikuwa imefika pabaya lakini kesho utamsikia huyohuyo kuwa atawalinda wale walioifikisha nchi pabaya.

ccm tuache usanii
 
Ni mpuuzi mwenzao atakayeamini upuuzi wao
we lizaboni pia ni mpuuzi thread zako ni za kimaandazi maandazi za lowasssa bavicha

lakini thread kama zile za kumpinga makonda kuzuia biashara zisifanyike kila jumamosi mpaka saa 4 asubuhi huji!!!!!!!
 
Ila huyo sio LIZABONI hebu angalia tena ID yake!
 
Habari wakuu!

Bila shaka kila MTU amekuwa akisikia lugha hii ya kwamba nchi yetu ilikuwa imefika pabaya. miongoni mwa watu wanaopenda kuongea hivi yumo pia Rais wetu na viongozi mbalimbali.

Cha kushangaza na cha kujiuliza ni watu gani hao walioifikisha nchi yetu kwenye hali mbaya? wako wapi, nchini, nje ya nchi, au wamekwishafariki?

Nasema lugha hii inakera na ni ya kejeli kwa sababu wanaotumia lugha hiyo ndio kikosi kile kile kilichokuwa serikalini, kilichobadilika ni kubadilishana nyadhifa lakini bado ni wale wale.

ndio maana Leo utasikia nchi ilikuwa imefika pabaya lakini kesho utamsikia huyohuyo kuwa atawalinda wale walioifikisha nchi pabaya.

ccm tuache usanii
Nchi hii kwa sasa ipo pabaya kuliko ilipowahi kuwa. Jumlisha na LUGUMI na kuhonga wabunge.
 
Mkuu anaongelea thinking yetu ya kitanzania kwa kipindi chote cha uhuru wetu.

Njia mpya ya magari ya mwendo kasi inajengwa halafu mtu anapitisha gari lake sehemu asiyotakiwa.

Viti vya uwanja wa taifa vinajengwa kwa fedha nyingi halafu mpumbavu mmoja anang'oa kiti na kukirusha uwanjani.

Elimu hewa, wanafunzi hewa, wafanyakazi hewa, meli hewa, ni utamaduni mbovu tuliokubali kuwa ndio unaotufaa.

Ni mchanganyiko wa mambo mengi sana ambayo sisi wenyewe tunaona ndio maisha halisi kumbe ni kielelezo cha udhaifu wetu wa kujitakia.
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom