Hii kitu kweli au ni utapeli naomba anayejua anijuze

Salaam wana jf
Nimekuta kwa email yangu upande wa "spam" nimetumiwa ujumbe wa kushinda pesa (paund GB) hizo halafu ikinielekeza kuzidai kwa kutoa maelezo binafsi na details za kibenki nk
Angalia picha attached chiniView attachment 1937684View attachment 1937688View attachment 1937685View attachment 1937687
Hii maujinga ya zamani sana aisee toka watu tunajifunza kutumia email miaka ya 1998 brother, wanaijeria wamepiga sana wajinga.

Achana na huo upuuzi hakuna hela ya burebure kihivyo hapo Yani unashindaje game ambayo haujawahi kucheza? Hapo wanakumwagia mtama utakula utafika mlangoni wanafunga mlango wanakutumia kwanza dola 200 halafu wanakuambia ukipata confirm ili waweze kutuma nyingine, ukiconfirn wanakuambia Sasa inabidi ulipie fee fulani hapo unakuwa overtaken na hiyo transaction unatoa dola 1000 bila kujua ili wakutumie mzigo wote hapo ndio unaliwa 😃😃

Hao jamaa huwa wanakuambia utume pesa kidogo sana ambapo utaidharau kama unahisi wewe ndio mwenye bahati sana na unajifanya msori. Ila what they do wanatumia email zaidi ya milioni moja kwa siku so wanapata hela sana kwa huo utapeli maana out of 5 million people lazima watu laki moja wanaingia mkenge. Uliza wanaijeria aisee ogopa sana na Kuna wazee wa kadi za viza noma.
 
....Umeukuta Ujumbe kwenye upande wa 'Spam' halafu bado unajiuliza kama ni 'Spam'?? Ulienda Shule kufanya nini??
Kwan nini maana ya spam
Mbona sometime hata jumbe za jf huwa naziona humo kwani kitu kuwa spam ndiyo kiwe scam au?
 
Asante kunijuza nimewaelewa kiufupi ni utapeli
Tusichoke kuelimishana
 
Back
Top Bottom