Hii ' Kero ' ya Mwenye Nyumba naipata tu peke yangu au tupo wengi tunaotaabika nayo?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,871
Mama mwenye Nyumba wangu simwelewi kwani kutokana na Vyuma Kukaza kwa sasa nimemwambia nitampa Kodi yake baada ya muda kama wa Wiki mbili zijazo hivyo awe tu mvumilivu Kwangu lakini kuna ‘ Kajitabia ‘ kamezuka hivi karibuni ambako kananitatiza.

Tokea juzi hadi leo kila nikimsalimia tu iwe ni asubuhi au usiku akishamaliza kuniitikia tu anaingia ndani na kuweka Wimbo wa Tshala Muana ule aliourudia wa Hayari Fredy Ndala Kasheba wa ‘ Dezo Dezo ‘ halafu kila ukifika ule mstari usemao ‘ unapenda dezo dezo……kodi ya Watu hulipi…..’ anaurudia rudia sana huku anasonya ‘ msonyo ‘ mrefu wa Tegeta Nyuki hadi Mbagala Kizuiani.

Natamani sana nimuulize Kulikoni kila nikimsalimia anauweka huo Wimbo lakini naogopa asije niongezea Kodi au hata kunidai kwa nguvu halafu akanijazia Inzi ( akanitangazia kwa Watu hapa ) ikawa noma Kwangu hivyo nimebaki tu kuumia kimoyo moyo.

Je hii adha naipata Mimi tu peke yangu kama Mpangaji au kuna Wapangaji wengine huko mliko nanyi pengine yanawakumba makubwa zaidi ya hayo ninayopata Mimi? Tafadhali na Wewe weka Wimbo ambao lazima tu Mwenye Nyumba wako ukiwa umemkwaza au umemuudhi hasa kwa kutomuwahishia Kodi yake huwa anakuwekea

Nawasilisha.
 
Mi wakwangu alikuwa na tabia siku tatu kabla ya tarehe ya kulipa,anaanza kununa hataki story na mtu.Ukimlipa tu jioni ya siku hiyo atatoa na karedio msikilize wote BBC wakati huo cheko mpaka jino la mwisho
 
Acha utoto. Kwani nyumba zote za kupanga hapa mjini znamilikiwa na huyo landlord wako ?
 
Mama mwenye Nyumba wangu simwelewi kwani kutokana na Vyuma Kukaza kwa sasa nimemwambia nitampa Kodi yake baada ya muda kama wa Wiki mbili zijazo hivyo awe tu mvumilivu Kwangu lakini kuna ‘ Kajitabia ‘ kamezuka hivi karibuni ambako kananitatiza.

Tokea juzi hadi leo kila nikimsalimia tu iwe ni asubuhi au usiku akishamaliza kuniitikia tu anaingia ndani na kuweka Wimbo wa Tshala Muana ule aliourudia wa Hayari Fredy Ndala Kasheba wa ‘ Dezo Dezo ‘ halafu kila ukifika ule mstari usemao ‘ unapenda dezo dezo……kodi ya Watu hulipi…..’ anaurudia rudia sana huku anasonya ‘ msonyo ‘ mrefu wa Tegeta Nyuki hadi Mbagala Kizuiani.

Natamani sana nimuulize Kulikoni kila nikimsalimia anauweka huo Wimbo lakini naogopa asije niongezea Kodi au hata kunidai kwa nguvu halafu akanijazia Inzi ( akanitangazia kwa Watu hapa ) ikawa noma Kwangu hivyo nimebaki tu kuumia kimoyo moyo.

Je hii adha naipata Mimi tu peke yangu kama Mpangaji au kuna Wapangaji wengine huko mliko nanyi pengine yanawakumba makubwa zaidi ya hayo ninayopata Mimi? Tafadhali na Wewe weka Wimbo ambao lazima tu Mwenye Nyumba wako ukiwa umemkwaza au umemuudhi hasa kwa kutomuwahishia Kodi yake huwa anakuwekea

Nawasilisha.
Bado tu unaishi kwenye nyumba za kupanga??
 
Mkuu unamawazo kama yangu, huyu jamaa nilijua yupo kwake na mambo mengine mengi

Ni lini labda niliwahi kukuambia kuwa Mimi ni Tajiri? Halafu kuna faida gani labda ambayo utaipata kama ukijua ama Mimi ni maisha bora au duni? Ukiwa humu JF changia tu mada na acha kutaka kuyajua sana maisha ya Watu na kuna uwezekano pia siku ukija kuyajua maisha halisi ya yule unayemdharau au kumdhihaki ukaja kushangaa, kuona aibu na kujiona ni Mpumbavu wa Kiwango chenye Ubora wake.

Uandishi wangu humu JF hasa katika ' threads ' huwa unaegamia katika ' technique ' ya Kiuandishi ya ' anecdote ' ambayo mara nyingi kama nataka kutuma ujumbe fulani ili kuifanya mada iwe nzito, iibue hisia na Watu wachangie hulazimika kujiweka Mimi kama ' main character ' ili kuichangamsha.

Nimekudharau na nimekupuuza mno tu!

Cc: Daudi Mchambuzi
 
Tatizo lako wewe una hasira na hutaki waende tofauti na Mawazo yako. Mm sijasema wewe ulitangaza humu lkn kibinadamu kulingana na mbembwe za humu kuna picha mm binafsi napata.
Punguza jaziba
 
Ni lini labda niliwahi kukuambia kuwa Mimi ni Tajiri? Halafu kuna faida gani labda ambayo utaipata kama ukijua ama Mimi ni maisha bora au duni? Ukiwa humu JF changia tu mada na acha kutaka kuyajua sana maisha ya Watu na kuna uwezekano pia siku ukija kuyajua maisha halisi ya yule unayemdharau au kumdhihaki ukaja kushangaa, kuona aibu na kujiona ni Mpumbavu wa Kiwango chenye Ubora wake.

Uandishi wangu humu JF hasa katika ' threads ' huwa unaegamia katika ' technique ' ya Kiuandishi ya ' anecdote ' ambayo mara nyingi kama nataka kutuma ujumbe fulani ili kuifanya mada iwe nzito, iibue hisia na Watu wachangie hulazimika kujiweka Mimi kama ' main character ' ili kuichangamsha.

Nimekudharau na nimekupuuza mno tu!

Cc: Daudi Mchambuzi
Kimsingi hata mm nilisha kudharau kitambo sana
 
Back
Top Bottom