Hii kero umewahi kuikuta kwa wafanyabiashara? Hivi nao watalalamika biashara ngumu?

Cosovo

JF-Expert Member
Jul 8, 2018
375
1,000
Kuna wafanyabiashara na wajasiriamali wanachekesha mnoo,na utawakuta wanalalamika kuwa biashara ngumu

Inakuaje unaenda kwa mfanyabiashara anayeuza bidhaa fulani ,halafu una sh 10000 (Elfu kumi noti) akuuzie bidhaa ambayo ni sh 200,300,500,700,au 1500 halafu ukishachukua bidhaa na kutoa noti tajwa unampa kwa mshangao anakurudishia hela yako kisa hana chenji

Pia cha kushangaza zaidi hajishughulishi kutafuta chenji badala yake anataka wewe mnunuzi ndo utafute chenji uje ununue bidhaa hiyo

Je ni halali mfanyabiashara kugoma kukuzia bidhaa kisa una hela kubwa?

Je watu kama hao watalalamika kuwa hawajauza leo hata senti ?

Je umewahi kukutana na wafanyabiashara kama hao? Ulichukua hatua gani au uliwaza nini kichwani

Wengine wanasema wafanyabiashara kama hao huwa wanakataa kwa sababu wanahisi unatafuta chenji maana haiwezekani utoe noti ya sh elfu kumi ununue wembe ya sh 100,utakuwa unatafuta chenji

Lakini hata kama lakini si unatafuta hela ,kwa nini ulete bidhaa sokoni?

Unazungumziaje wafanyabiashara wa hivyo
 
Baraja

JF-Expert Member
Dec 28, 2015
1,435
2,000
Wewe mwenyewe vaa kiatu cha muuza karanga za 200@ au muuza machungwa ya 100 na unataka chungwa moja unatoa elfu 5 au 10.

Mfikirie konda wa daladala asubuhi anapewa elfu 10 nne za watu tofauti akate sh 1200 katika elfu 40
 
RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
44,488
2,000
Ifikie mahali tueleweshane maana sahihi ya mfanyabiashara. Mfanyabiashara anaejijua anauza vitu vya TSH 200,300,500 na anajua ana wateja wengi huamka asubuhi na kupitia chenji benki kabla hajaanza biashara. Wahindi wengi wanafanya hivi.
 
mkaamweusi

JF-Expert Member
Feb 19, 2013
546
1,000
Nakuibia tu hii siri.

Chumaulete wengi, hutumia hiyo mbinu kumwibia Mfanyabiashara.

Yaani unamchosha akili, aumize kichwa kupanga chenji ya tsh9900,

Ghafla anaingia mwingine anajifanya ana haraka na kitu fulani, mwisho wa siku unajikuta unazidisha chenji.

Binafsi ukija na 5000 unataka vocha ya 1000 kama chenji sina nakwambia kanunue kwa jirani.

Remember;Unatumia energy kubwa kuzunguka kuomba chenji afu upate faida ya sh 50 au 100.Mfanya biashara smart yupo makini ni wapi apoteze energy yake.
 
Torque vs HP

JF-Expert Member
Jan 7, 2021
1,776

Kwanini ufanye biashara ya faida ya sh. 50 au 100 kama hutaki purukushani hizo?
 
Mother Confessor

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
18,394
2,000
Kuna wafanyabiashara na wajasiriamali wanachekesha mnoo,na utawakuta wanalalamika kuwa biashara ngumu

Inakuaje unaenda kwa mfanyabiashara anayeuza bidhaa fulani ,halafu una sh 10000 (Elfu kumi noti) akuuzie bidhaa ambayo ni sh 200,300,500,700,au 1500 halafu ukishachukua bidhaa na kutoa noti tajwa unampa kwa mshangao anakurudishia hela yako kisa hana chenji

Pia cha kushangaza zaidi hajishughulishi kutafuta chenji badala yake anataka wewe mnunuzi ndo utafute chenji uje ununue bidhaa hiyo

Je ni halali mfanyabiashara kugoma kukuzia bidhaa kisa una hela kubwa?

Je watu kama hao watalalamika kuwa hawajauza leo hata senti ?

Je umewahi kukutana na wafanyabiashara kama hao? Ulichukua hatua gani au uliwaza nini kichwani

Wengine wanasema wafanyabiashara kama hao huwa wanakataa kwa sababu wanahisi unatafuta chenji maana haiwezekani utoe noti ya sh elfu kumi ununue wembe ya sh 100,utakuwa unatafuta chenji

Lakini hata kama lakini si unatafuta hela ,kwa nini ulete bidhaa sokoni?

Unazungumziaje wafanyabiashara wa hivyo
Umenikumbusha jana wakati naenda zangu kinyerezi kutokea kimanga,mdada kapanda daladala imeanza kuondoka kituo cha mbele akatoa noti ya 10,000 anamwambia konda nashuka bima hivyo tafuta chenji mapema na hapo anatakiwa kukata 300 tuu,hahahah yaani nilimuona konda alivyosawajika kumshusha hawezi kilichofuata ni kumpa chenji za mia mia 😂😂hadi yule dada akasema hee ndo unanikomoa...nilimuonea hadi huruma maana aliyakumbatia yale machenji duh kama mkimbizi...😂😂
 
TANMO

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
10,212
2,000
Binafsi pia huona ni dharau kununua kitu cha 100 halafu unatoa 10k.. Hata ikinitokea Nina uhitaji Wa bidhaa ya pesa ndogo na Nina pesa kubwa humpa taarifa muuzaji mapema kabla hajanipatia ninachohitaji..

Unamwambia kabisa nataka maji ya mia tano Ila Nina elfu kumi, je utakuwa na chenji? Na mara nyingi ukimuuliza kistaarabu huwa hawalalamiki, shida ni pale unaagiza maji, unayafungua kabisa kisha ndiyo unatoa elfu kumi..

Na hili suala siyo TZ pekee, Hata nchi nyingine nimewahi shuhudia huu utata wa kutoa pesa kubwa kwa manunuzi ya kitu cha pesa ndogo, na watu kugombezana kabisa..
 
Mtoto halali na hela

JF-Expert Member
Aug 10, 2012
33,697
2,000
Kuna neno zuri "pambana" ina maana jipange andaa chenji ya kutosha hata wiki ili kum retain mteja asikukatie tamaa

Hilo ni jukumu lako kuwa na chenji hata wakija wateja buku 1! Tatizo biashara tunazifanya kimazoea. Nenda supermarket kama discount centre uone kama kuna huo ujinga
Nimejifunza nikifungua yangu hamtakosa chenji
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom