Hii kauli ya vijana wajiajiri inakera sana

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,236
9,841
HII KAULI YA KUWAAMBIA VIJANA WAJIAJIRI INAWAKERA SANA.

Na Thadei Ole Mushi.

Mzee Mangula Shikamoo!!! Mwenye number ya Mzee Mangula Mpeni huu Ujumbe wa kutaka vijana wajiajiri. Mwambieni kuwa:-

Kiongozi anayepokea Mshahara kila Mwezi, Posho kila Siku, anawekewa mafuta ya gari, analipiwa malazi na marupurupu mengine. Akishakula akashiba anapanda jukwaani anamwambia kijana wa mlalahoi, aliyeifilisi familia yake ili apate ada ya kusoma, hana hata cent mfukoni baba yake na mama yake wanakomaa na wadogo zake ambao bado wapo shule KAJIAJIRI hili kwa Kifupi ni Tusi.

Mtaala wetu unahitaji marekebisho makubwa sana cha kushangaza hakuna kiongozi anayejali. Vyuo vingi vya Ufundi tumevifanya kuwa vyuo vikuu. Kwenye Soko la ajira wanaoteseka zaidi ni wahitimu wa vyuo vikuu.

Tunatoa mabilioni ya Shilingi kama mikopo ya vyuo vikuu kwa vijana ambao hatuna uwezo wa kuwaajiri. Huu ni upotevu wa fedha.... Yaani ni fedha tunachimbia chini.

Tukiendelea kudharau masomo ya Ufundi, fani mbalimbali, Kilimo na Ufugaji tutakuja kupigana Siku za Usoni. Mtaala wetu utambue fursa zilizopo nchini.... Tunapoteza muda mwingi sana kujifunza mambo yasiyokuwa na msaada kwenye maisha yetu.

Hawa viongozi wanataka watu wajiajiri watuambie watoto wao wamejiajiri wapi ili wakajifunze wengine. Huo mtaji wa kujiajiri wameupatia wapi ili nao wakajiandikishe kuchukua....

Shule zetu hazifundishi Kilimo wala Ufugaji, wanafundisha matundu ya Panzi na ukuaji wa chura. Shule zetu hazifundishi Uvuvi zinafundisha mkoloni alituuzaje utumwani, shule zetu hazifundishi Ufundi (Uchomeleaji, uchoraji, Ususi, Upishi, Ujenzi nk.) Zenyewe zimokomaa kuelezea Mzungu alivyotupora ardhi yenye Rutuba.....

Wizarani yupo Profesa anaendelea kuhudhuria maafali mbalimbali na kuelezea mabilioni yanayomwagwa na JPM kwenye Elimu kwa ajili ya Elimu Bure. Vijana waliohitimu vyuo vikuu lazima tukubali kuwa na mjadala wa kitaifa.... Namuona waziri wenu Mavunde akicheza Bao....

Kuwa na watu wengi nchini bila ajira au watu wasioweza kujikimu ni Tatizo kubwa. Vijana wanajenga chuki na viongozi wao sana kutokana na tatizo hili.

Miaka Saba msingi, Miaka Sita Sekondari, miaka Mitatu chuo kikuu jumla miaka 16 huko kote hukufundishwa kujiajiri unamaliza chuo wanataka mtende miujiza kwa kujiajiri. Tuache kutaniana na hawa vijana viongozi wanapaswa kuwaomba msamaha.

Ngoja nirudi jalalani nisiseme sana.

Ole Mushi
 
Tungeaanza kwa kusema nafasi za serikalini wawe wanafanya kazi kwa miaka mitano mitano then wanaaenda kujiajiri kupisha wengine waingie.....
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom