Hii kauli ya Rais Magufuli "Wafugaji walishe popote nchini" sio uchochezi? Hivi wakulima watapata haki zao kweli?

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,868
Rais Magufuli aruhusu wafugaji kulisha popote nchini

Pia, Rais Magufuli amewata wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi kushirikiana na Wizara za Kilimo, Maliasili na Utalii, Mifugo na Uvuvi na Tamisemi kupanga mipango bora ya ardhi ili kuhakikisha hapatokei migogoro.

Rais Magufuli alitoa kauli na maelekezo hayo jana alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Mwandoya na Meatu wilayani Meatu mkoani Simiyu katika siku ya pili ya ziara yake mkoani humo ambayo inahitimishwa leo.

Alisema haoni sababu ya wafugaji wala wakulima kunyanyasika wakati wanahitajika na mchango wao ni mkubwa katika nchi.

"Nataka kila mkuu wa mkoa na wilaya watenge mazingira ya kuwasaidia wakulima, wafugaji na wavuvi, hakuna sababu ya kusema eti warudi huko huko walikotoka, unawezaje kusema huwahitaji wafugaji wakati ng`ombe unahitaji, unasemaje wafugaji huwataki wakati nyama unahitaji," alisema Rais Magufuli na kuongeza:

"Sisi sote tunategemeana, naomba kuwekwe mazingira mazuri ya kuwawezesha kutekeleza majukumu yao bila kuathiri upande mwingine."

Pia Rais Magufuli aliwataka wafugaji hao kufuga kisasa na kuhakikisha wanaitumia nafasi hiyo ili kuwaletea maendeleo.

“Serikali yangu inapenda wafugaji, lakini ni lazima tukubali ufugaji wa sasa ni lazima tubadilike, wakati tunapata uhuru tulikuwa na ng`ombe milioni tisa, lakini mpaka sasa tuna ng`ombe milioni 30.5, wakati tunapata uhuru watu tulikuwa milioni 10, leo tuko milioni 55 bado hujahesabu mbuzi, kondoo, kuku, lakini ukubwa wa ardhi bado uko vile vile," alisema Rais Magufuli.

"Mifugo inaongezeka, watu tunaongezeka, 'activities' (shughuli) nazo zinaongezeka, lakini ardhi tuliyonayo ni hiyo hiyo, haipanuki, yale maeneo yaliyokuwa ya maji, ya mito bado ni yale yale, maeneo tuliyokuwa tumeyaweka kwa ajili ya uhifadhi wetu bado yapo na mengine tunayavamia, hiyo ndio changamoto ya kuangalia kama taifa, kwamba tunalimaje, tunafugaje na tunatunzaje wanyama wetu wa porini."

"Suala la kuwa na ng`ombe elfu tano unakuwa unazunguka nao imepitwa na wakati, unaenda kuchunga katika mashamba ya watu, imepitwa na wakati, sisemi mpunguze idadi ya ng`ombe isipokuwa niwaombe wachungaji tuanze kufuga kisasa."

Rais Magufuli pia aliwataka wafugaji ambao wana maeneo yao makubwa mahali wanapoishi wafuge idadi yoyote ya ng`ombe wanayohitaji, huku akiwataka kutumia ng`ombe walionao kujiletea maendeleo.

"Ukiwa na ng`ombe wengi, vuna wachache jenga hata nyumba ya bati, chimba hata bwawa la maji yako," alisema.

Aliwaomba viongozi, wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi kwa kushirikiana na Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Ardhi na Tamisemi, wajitahidi kutatua migogoro kwa usalama kila mahali palipo na migogoro hiyo.

"Nimekuwa nikisikiliza matamshi mengine yakitolewa na baadhi ya viongozi wanasema hawa wafugaji warudi kwao, kwao ni wapi, kwao ni Tanzania. Kwa hiyo mchungaji ana haki ya kwenda mahali popote kwa sababu ni Watanzania. Lakini ni lazima mzingatie sheria pia," alisema Rais Magufuli.

"Serikali hii inawapenda sana wafugaji, lakini tushirikiane na mamlaka zilizopo ili tufuge vizuri, serikali inawapenda sana wakulima, ni lazima tushirikiane na mamlaka katika kupanga matumizi bora ya ardhi yetu. Mimi huwa nasikitika sana ninaposikia wakulima na wafugaji wanapigana mpaka wanauana."

Kwa upande wake, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina, alisema lengo la serikali ni kuhakikisha inatatua changamoto za wafugaji zilizopo.

“Tunataka kila Mtanzania anayefuga, mifugo isiwe misalaba, tuna mifugo mingi, tuna maeneo mengi ya malisho kama tutayapangilia vizuri,” alisema Mpina.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka, alisema wamepanga namna ya kuboresha sekta ya ufugaji ikiwamo kujenga kiwanda cha nyama.

Chanzo: Nipashe
 
Alipokuwa anasema yeye ni kichaa hakuyasema hayo kwa bahati mbaya, hayo aliyasema akimaanisha kabisa lakini cha kushangaza na kusikitisha watetezi na mashabiki wa kichaa wanaleta propaganda kuwa hakumaanisha kama yeye ni kichaa pure, ukichaa wa mtu siyo lazima aokote makopo, wengine ni vichaa lakini wako ofisi za umma kama jenny muro, bashite, gumbuzi, mnyet n.k
 
woyoooo! upele umefika kwa mkunaji..

Kachaa kapewa rungu.!!

Mifugo yangu ya urithi naifungulia kwenye shamba pori LA jirani yangu Baba Ubaya...ila lina nyoka wengi balaa
 
Back
Top Bottom