Hii kauli ya Makamu wa Rais ina maana gani?

Ukali wa wanajeshi wetu sijawahi kuuona popote, ina maana wote waliotangulia walikuwa na busara hawajawahi kuvurugwa na yeyote toka tupate uhuru?
Wanajeshi halisi walikuwa akina marehemu hans pope, angalao walijaribu japo walisalitiwa
 
Mh. Dr. Isidori Mpango hakupaswa kutoa maneno hayo kwa Waziri wa Ulinzi kwa uwazi namna hii ambapo maneno haya wameyapata hawa wanajeshi.

Hii sio sahihi kabisa inakuwa kama vile anamchonganisha Tax na Maafande! Pia itawafanya Maafande wasimheshimu hiyu Waziri wao na itamfanya Tax asijiamini atakapokuwa na hao Maafande.

Generally, Makamu wa Rais katereza kwa hilo andiko!!!
Siku ya kiapo tunatamani Rais atoe neno Kwa nchi juu ya hali halisi ili angalau kujenga matumaini mapya kwa wananchi.Maana wananchi wengi wanakuwa kama wana maswali mengi na majibu machache.Mbolea bei juu,petrol juu,mafuta ya Kula juu,nk nk.Hao viongozi wengine sio lazima waongee.Mambo ya kutwambia eti Fereshi hakujua kuwa anakuja Dodoma kula kiapo cha kuwa AG ,
 
Umechanganywa na rangiiiii au majina?
Ameongoza na kuratibu shughuli za kamati nyeti ndani ya SADC. Amekuwa katibu EAC and SADC Kwa nyakati tofauti na kahudumu muda mrefu. Amekuwa katibu wa wizara pia.

Unadhani nafasi hizo hazitoshi kuonesha kwamba yuko vizuri? Kwa mfumo wa nchi yetu kupewa hizo nafasi tayari inaonesha kwamba yuko vizuri huyo mama.
 
AJIUZULU TU...../
YEYE PAMOJA NA RAISI WAKE MIMI KUSEMA KWEELI SIWAELEWI KABISA
takataka yaani trash
Kama wewe umwelewi sisi tunamwelewa , na tunamuunga mkono na tutamtii(kauli ya cdf chato).Kazi iendelee
Mama tupo naye sana tu.."atake asitake"
 
Kwa jinsi TZ ilivyo usiseme jeshi halijaingizwa siasa. Huoni akina Makamba, Mkuchika, Komba, Lowasa, na wengine akina kikwete,, Kinana, watu kibao walitoka CCM kuingizwa jeshini na wakarudi CCM?

Angalia wanajeshi kibao wakistaafu wanapewa vyeo vya CCM, usiseme jeshi halipo kisiasa sema jeshi lipo kisiasa za CCM lakini nao wangeruhusu ex military akistaafu ajiunge na upinzani wa CCM mbona mngekoma mapema sana CCM???

Maana ingekuwa kuna wafuasi wa vyama vingine pia kama walivyokomesha Ile uchaguzi wa 2015 walimnyoosha jiwe mpaka akawachukia
Very good answer, now the question is, walipelekwa kufanya nini? Makamisaa wa nini Yani purpose ya kuwatoa makada na kuwapeleka jeshini wakapata mavyeo then wakarudi kwenye siasa ilikuwa nini?

Ukisema 1992 ndio walirudishwa nakataa maana akina Lowassa na mzee Mkuchika na hao wengine walifanya kazi na Nyerere na walikuwa Mawaziri toka enzi hizo walipotoka jeshini especially baada ya Vita ya Kagera so hawakukaa sana huko jeshini so nakataa hiyo hoja yako kwamba walirudishwa 1992.

Siasa ipo kwenye jeshi letu na no siasa ya CCM tukubaliane tu mzee.
Someni historia vijana.
Mjue tulikotoka.
Muwajue na akina Col Moses Nnauye.
Tatizo kubwa humu watoto wengi na historia hata ya jeshi hawaijui.
Tukirudi nyuma zaidi kwa akina Nyirenda, Kavana ndo tunawaacha kabisa.
 
Mh. Dr. Isidori Mpango hakupaswa kutoa maneno hayo kwa Waziri wa Ulinzi kwa uwazi namna hii ambapo maneno haya wameyapata hawa wanajeshi.

Hii sio sahihi kabisa inakuwa kama vile anamchonganisha Tax na Maafande! Pia itawafanya Maafande wasimheshimu hiyu Waziri wao na itamfanya Tax asijiamini atakapokuwa na hao Maafande.

Generally, Makamu wa Rais katereza kwa hilo andiko!!!😆😆😆
Kwani maafande hawakushirishwa uteuzi? Hiyo kazi ya uwaziri Raisi aliishusha hadhi kwenye hotuba aliposema kazi ya waziri sio sijui mabunduki na na kuendesha vifaru au. Misuli! !! Kutetea kuwa ni kazi ndogo hata mwanamke aweza kufanya kazi ya waziri wa Ulinzi! !!

Wanawake huwa hawapangwi jeshini shift za usiku wala hakuna commandoo mwanamke JWTZ. Waziri wa Ulinzi Mwanaume alikuwa akiwekwa makusudi kuwa anatakiwa kuwa on duty masaa 24 akiitwa usiku wa manane kwenye kikao anatakiwa kuinuka haraka kwa spidi ya mwewe kwenda. SASA mama akiistuliwa usiku wa manane hadi avae nguo mia apake lipstick ajipodoe si kutakuwa kumekucha
 
Wanajeshi wenyewe wameridhika wengi vitambi vitupu, hamna jeshi hapa
Ukiwaona wembamba hao ujue ni kuruta mpya na muda si mrefu anachomoa kazi na kurudi kitaa...
Maana hata vyeo vya kukupa kitambi ni mishimise...
Vita Sasa hivi ni vifaa sio vitambi
 
Ameongoza na kuratibu shughuli za kamati nyeti ndani ya SADC. Amekuwa katibu EAC and SADC Kwa nyakati tofauti na kahudumu muda mrefu. Amekuwa katibu wa wizara pia.

Unadhani nafasi hizo hazitoshi kuonesha kwamba yuko vizuri? Kwa mfumo wa nchi yetu kupewa hizo nafasi tayari inaonesha kwamba yuko vizuri huyo mama.
Kwa CV hiyo wizara ya Mambo ya nje ndiko kungemfaa zaidi sio Ulinzi
 
JWTZ yetu ni Jeshi la kistaarabu sana.
Moja ya Taasisi ambazo hazijaingizwa siasa kama vyombo vingine vya usalama
Nina hadithi nyingi za kwasimulia juu ya umahiri wa Jeshi letu lakini kama hata wao wanaandika katika Daily Order, IMEZUILIWA.
Waziri raia katika MOD inabidi aelewe nafasi yake la sivyo anajikuta redundant.
Yalimpata waziri Maokola Majogo enzi za Mkapa.
Ikabidi aombe poo!
mh mkuu acha siasa.
 
Ukali wa wanajeshi wetu sijawahi kuuona popote, ina maana wote waliotangulia walikuwa na busara hawajawahi kuvurugwa na yeyote toka tupate uhuru?
True maana hata huyo kuandikwa sijui kuchorwa alikua wala hajulikani kama yupo
 
Hatupo hapa kuthibitisha kila hoja maana nyingine unapewa kama hints na ukisoma vizuri nilichoandika haihitaji kuendelea kuniquote na kusema haubishi

Mengine huwa tunayachukua halafu unajiongeza ukiona hauna majibu basi chukulia umepewa info isiyo ya ukweli. Ila kwa mwenye akili hapo anajua info hiyo anaipata wapi.

Otherwise alamsiki jomba.
Kinachofanya nihoji ni kuwa kama vituo vyote vya kambini (tanzania nzima) wewe ulipataje hizi habari ?

na inawezekanaje jiwe awe na chuki na askari ambao ndio wanamlinda na kulinda mamlaka yake na mbona aliwaongezea mishahara
 
Wanajeshi wenyewe wameridhika wengi vitambi vitupu, hamna jeshi hapa
Ukiwaona wembamba hao ujue ni kuruta mpya na muda si mrefu anachomoa kazi na kurudi kitaa...
Maana hata vyeo vya kukupa kitambi ni mishimise...
Kwa wananchi wanaotokea mikoa ya mipakani wanaona umuhimu na kazi za askari jeshi

na kingine kitendo cha uwepo tu wa jeshi ni kazi tosha na kingine unajua kuwa askari wa jwtz wapo msumbiji kuhakikisha magaidi hawavuki mpaka na kuja kufanya uharibifu tz ?
 
Back
Top Bottom