Hii kauli ya Makamu wa Rais ifanyiwe kazi haraka

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,983
11,404
Nimemsikia makamu wa rais akisema kuwa kuna watoto wa shule wanajiuza kwenye clab za usiku, hili jambo sio la kupuuzwa hata kidogo, wazazi wanatumia fedha nyingi kuwalea watoto na kuwagharamia ki masomo halafu wakafanye biashara za hovyo hapana.

nilitegemea kabla ya kauli hiyo tayari watoto kadhaa wawe wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano, hizo kumbi zina camera za usalama uongozi wa chuo husika waende kutizama na kubaini wanafunzi tajwa. najua mkuu huyu aliyasema hayo akiwa na ukweli usiokuwa na shaka kwani anavyo vyanzo mbalimbali vya habari yaani ndio mwenye dola na dola ina mkono mrefu.

ni wakati sasa wizara husika iweke kanuni kuwa chuo kidahili wasichana kulingana na uwezo wa mabweni waliyonayo ili watoto wa kike wote wakae bweni tena chini ya uangalizi wa matron. Haingii akilini chuo chenye uwezo wa kuwapatia malazi wanafunzi elfu mbili kudahili wanafunzi elfu sita hapana hizo ni tamaa za fedha hakuna sababu chuo kudahili wanafunzi wengi zaidi ya uwezo wake.

Mwanafunzi akae nje ya chuo kwa sababu maalumu, labda awe ananyonyesha au ni mke wa mtu, mfano wanafunzi wa masters anaweza kuwa ni mama mtu mzima mwenye familia huyo anaweza kaa nje ya chuo.

Zipo clab za usiku hutuma magari kusomba mabinti wa chuo kuwapeleka kwenye disco na dansi za usiku hili lipigwe marufuku, miaka ya nyuma madisco ya wanafunzi yalikuwa yakifanyika maeneo ya chuo sasa hili la akina sumaye kuwakusanya watoto katika kumbi za usiku kwa kisingizio cha mafahali hapana hatuwezi kubaliana nayo lazima maadili yazingatiwe.

Ukweli ni kuwa sasa hivi watoto wanaanza shule wakiwa wadogo muda mwingine mtoto anaanza darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka mitatu na anarushwa darasa hivyo upo uwezekanao akahitimu chuo kikuu akiwa binti mdogo na asiyejitambua.

Tuliwahi sikia sintofahamu ya mwanafunzi aliyekuwa akiishi na hawara kibaka bwenini tena asiyekuwa mwanachuo. Hivyo hii kauli ya makamu wa rais lazima ifanyiwe kazi na kutolewa ufafanuzi.
 
Mkuu hili tatizo ni kubwa na ambalo hakuna anayeweza kuliongelea wala kilisimamia kulizuia. Kumbuka jamii yetu imekosa maadili kabisa. Siyo viongozi, siyo law enforcers hakuna hata mmoja. Kumbuka kuwa hawa wadada wa vyuo wanaojiuza wateja wao wakubwa ni viongozi wetu. Wabunge, Mawaziri, Wakurugenzi, Askari polisi wote hawa ndio consumers wa hawa dadapoa wa vyuo. Hapao unategemea nini? Hakuna chochote kinachoweza kufanyika badala yake utasikia ni Makamu wa Rais katumia lugha ya uzalilishaji kwa wanavyuo wa kike. Wanaofanya hivyo wanalinda biashara isifungwe wakakosa sehemu ya kununua bidhaa. Kama siyo maadili kumomonyoka katika jamii yetu kusingekuwa na wazee kutembea au kuoa wanawake lika la watoto wao wa kuzaa. Haya yanafanyika hakuna wa kukemea, na hao hao vingozi ndo wanayafanya hayo japokuwa sheria zipo lakini wasimamizi ndo wavunja sheria. oooops!
 
Mimi nikafikiri unazungumzia wale wa shule ya msingi na sekondari, kumbe wa chuo? Japokuwa mimi binafsi kutokana na imani yangu na pia utashi sikubaliani na suala la disco, ila mtoa mada naona kama umechanganya madesa. Hayo ya Sumaye na watoto wanaojiuza vina uhusiano gani? Na pia unafikiri kila mwanachuo anayeenda club anajiuza? Na pia unafikiri pia kukaa darasani peke yake na kusoma tu bila kupata exposure ya mambo mengine ya maisha itamjengea mazingara bora mhitimu wa chuo? Alichosema VP kina mantiki na kinasikitisha sana. Si vizuri kwa wanachuo au watu wa kawaida kujiuza. Ila uandikaji wako upo kimhemko zaidi
 
Nimemsikia makamu wa rais akisema kuwa kuna watoto wa shule wanajiuza kwenye clab za usiku, hili jambo sio la kupuuzwa hata kidogo, wazazi wanatumia fedha nyingi kuwalea watoto na kuwagharamia ki masomo halafu wakafanye biashara za hovyo hapana.

nilitegemea kabla ya kauli hiyo tayari watoto kadhaa wawe wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano, hizo kumbi zina camera za usalama uongozi wa chuo husika waende kutizama na kubaini wanafunzi tajwa. najua mkuu huyu aliyasema hayo akiwa na ukweli usiokuwa na shaka kwani anavyo vyanzo mbalimbali vya habari yaani ndio mwenye dola na dola ina mkono mrefu.

ni wakati sasa wizara husika iweke kanuni kuwa chuo kidahili wasichana kulingana na uwezo wa mabweni waliyonayo ili watoto wa kike wote wakae bweni tena chini ya uangalizi wa matron. Haingii akilini chuo chenye uwezo wa kuwapatia malazi wanafunzi elfu mbili kudahili wanafunzi elfu sita hapana hizo ni tamaa za fedha hakuna sababu chuo kudahili wanafunzi wengi zaidi ya uwezo wake.

Mwanafunzi akae nje ya chuo kwa sababu maalumu, labda awe ananyonyesha au ni mke wa mtu, mfano wanafunzi wa masters anaweza kuwa ni mama mtu mzima mwenye familia huyo anaweza kaa nje ya chuo.

Zipo clab za usiku hutuma magari kusomba mabinti wa chuo kuwapeleka kwenye disco na dansi za usiku hili lipigwe marufuku, miaka ya nyuma madisco ya wanafunzi yalikuwa yakifanyika maeneo ya chuo sasa hili la akina sumaye kuwakusanya watoto katika kumbi za usiku kwa kisingizio cha mafahali hapana hatuwezi kubaliana nayo lazima maadili yazingatiwe.

Ukweli ni kuwa sasa hivi watoto wanaanza shule wakiwa wadogo muda mwingine mtoto anaanza darasa la kwanza akiwa na umri wa miaka mitatu na anarushwa darasa hivyo upo uwezekanao akahitimu chuo kikuu akiwa binti mdogo na asiyejitambua.

Tuliwahi sikia sintofahamu ya mwanafunzi aliyekuwa akiishi na hawara kibaka bwenini tena asiyekuwa mwanachuo. Hivyo hii kauli ya makamu wa rais lazima ifanyiwe kazi na kutolewa ufafanuzi.
Classless point.......mwanafunzi wa chuo aanze kulindwa? Mawazo haya wapelekee primary huko. Tatizo ni mtoto mwenyewe
 
Back
Top Bottom