Hii kauli ya Askofu Dkt Fredrick Shoo kwa Rais Magufuli imenistua!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,975
Kuna kauli ambazo zikisemwa na mtu ambaye ni makini kwa yale anayoyasema lazima utazichambua kwa makini kama unafahamu vizuri umuhimu wake.

Watumishi wa Mungu ni tofauti na wanasiasa. Kuanzia kwa Mwenyezi Mungu mpaka kwa mitume wake kila neno walilokuwa wanalisema lilikuwa lina ujumbe mahsusi lakini kikubwa zaidi lilitamkwa kwa umakini sana. Wanasiasa wengi hutamka tu neno lolote bila kuwa makini na kwa sababu hii ni kupoteza muda kuanza kujadili kauli za wanasiasa wengi.

Kwa mantiki hii ndio maana jamii inategemea hata watumishi wa Mungu wafanye kama Mwenyezi Mungu na Mitume wake walivyofanya katika kuwasilisha ujumbe kwa jamii.

Kikubwa zaidi, Mungu na mitume wake hawakuwa wanafiki na kwa mantiki hii hata watumishi wa Mungu lazima wawe sio wanafiki.

Baada ya Maaskofu kukutana na Rais Magufuli nilikuwa na hamu ya kutaka kujua watakachokitamka kwa jamii hasa kwa kuchunguza kila neno.

Katika maneno yote Maaskofu waliyosema, haya maneno ya Askofu Dkt. Shoo yalinistua kidogo hasa kutokana na nafasi yake kama Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Dkt. Shoo alisikika akisema, ‘’Nimeshukuru mno, nimerudi moyo wangu una furaha na amani. Mungu akubariki sana, Aksante sana Mweshimiwa, asante sana’’.

Askofu Shoo pia akasema, ''Kwamba Rais wetu, ambaye mimi nasema sio kwa bahati mbaya amekuwa Rais wa nchi hii. Yeye anayo madaraka na Mungu amependa awepo hapo, kilichopo ni kushirikiana naye na Watanzania tushirikiane naye''.

Haya ni maneno machache lakini kwa watu wenye fikra pana watajua kuwa yamebeba ujumbe mahsusi na maswali mengi.

Moja ya swali la kujiuliza ni Askofu ana maana gani anaposema, ’’nimerudi moyo wangu una furaha na amani’’

Je, alienda Ikulu kuonana na Rais akiwa hana furaha na amani moyoni?

Je, ni kitu gani kimemfanya awe na furaha na amani baada ya kukutana na Rais Magufuli?

Je, kama hakuwa na furaha na amani kabla ya kukutana na Rais, kwa nini hakuwa na furaha na amani?

Je, Kitu gani kilimfanya akawa hana furaha na amani?

Pia Askofu Shoo ana maana gani anaposema, Rais Magufuli amekuwa Rais wa Tanzania sio kwa bahati mbaya?

Je, kuna Marais wengine walikuwa Marais wa nchi kwa bahati mbaya? Ni kina?

Ni bahati mbaya maswali ya aina hii hakuweza kuulizwa baada ya kutamka hasa ikichukuliwa kuwa kila neno analotamka mtumishi wa Mungu limebeba ujumbe muhimu katika jamii lakini haitakuwa vibaya kama nitapata majibu hapa jukwaani kama ilivyo kauli mbiu ya Jamiiforums inayosema, ‘’ The Home of Great Thinkers. Where we Dare to Talk Openly’’!

Video yenye maneno aliyosema Askofu Dkt Fredrick Shoo.
 
Kuna kauli ambazo zikisemwa na mtu ambaye ni makini kwa yale anayoyasema lazima utazichambua kwa makini kama unafahamu vizuri umuhimu wake.

Watumishi wa Mungu ni tofauti na wanasiasa. Kuanzia kwa Mwenyezi Mungu mpaka kwa mitume wake kila neno walilokuwa wanalisema lilikuwa lina ujumbe mahsusi lakini kikubwa zaidi lilitamkwa kwa umakini sana. Wanasiasa wengi hutamka tu neno lolote bila kuwa makini na kwa sababu hii ni kupoteza muda kuanza kujadili kauli za wanasiasa wengi.

Kwa mantiki hii ndio maana jamii inategemea hata watumishi wa Mungu wafanye kama Mwenyezi Mungu na Mitume wake walivyofanya katika kuwasilisha ujumbe kwa jamii.

Baada ya Maaskofu kukutana na Rais Magufuli nilikuwa na hamu ya kutaka kujua watakachokitamka kwa jamii hasa kwa kuchunguza kila neno.

Katika maneno yote Maaskofu waliyosema, haya maneno ya Askofu Dkt. Shoo yalinistua kidogo hasa kutokana na nafasi yake kama Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Dkt. Shoo alisikika akisema, ‘’Nimeshukuru mno, nimerudi moyo wangu una furaha na amani. Mungu akubariki sana, Aksante sana Mweshimiwa, asante sana’’.

Haya ni maneno machache lakini yamebeba ujumbe na maswali mengi.

Askofu ana maana gani anaposema’’ nimerudi moyo wangu una furaha na amani’’

Je, alienda Ikulu kuonana na Rais akiwa hana furaha na amani moyoni?

Je, ni kitu gani kimemfanya awe na furaha na amani baada ya kukutana na Rais Magufuli?

Je, kama hakuwa na furaha na amani kabla ya kukutana na Rais, kwa nini hakuwa na furaha na amani?

Je, Kitu gani kilimfanya akawa hana furaha na amani?

Ni bahati mbaya maswali ya aina hii hakuweza kuulizwa baada ya kutamka hasa ikichukuliwa kuwa kila neno analotamka mtumishi wa Mungu limebeba ujumbe muhimu katika jamii lakini haitakuwa vibaya kama nitapata majibu hapa jukwaani kama ilivyo kauli mbiu ya Jamiiforums inayosema, ‘’ The Home of Great Thinkers. Where we Dare to Talk Openly’’!

Video yenye maneno aliyosema Askofu Dkt Fredrick Shoo.

Kwa kifupi Dr. Shoo ana furaha kutokana na dhana aliyokuwa akiifikiria kuwa huenda Mh Rais anapigana na kanisa na hasa KKT.
Na baada ya MAZUNGUMZO amekuta sivyo alivyokuwa akifikiria. Na ndo maana akasema anaondoka Ikuluni akiwa na moyo ulio na amani.!
 
Mkuu;
Neno KUPIGANA limebeba hoja nzito sana hasa katika mazingira ya iamani za dini! Naomba unisaidie kunielimisha zaida unaposema dhana ya Rais Magufuli ana PIGANA na kanisa.
 
Kwa kifupi Dr. Shoo ana furaha kutokana na dhana aliyokuwa akiifikiria kuwa huenda Mh Rais anapigana na kanisa na hasa KKT.
Na baada ya MAZUNGUMZO amekuta sivyo alivyokuwa akifikiria. Na ndo maana akasema anaondoka Ikuluni akiwa na moyo ulio na amani.!
Moyo wa mtu ni kichaka matendo na maneno tofauti.
 
Back
Top Bottom