Hii kasumba ya Serikali kukamata mali za wafanyabiashara wakidaiwa kificha bidhaa inapoadimika sokoni, Je ni suluhisho?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Nianze kwa kusema wazi!
Inchi yetu ipo kwenye mfumo wa "SOKO HURIA"
Inakuwaje kila Mara bidhaa inapoadimika Serikali inakimbilia kukamata Mali za wafanya biashara kwa (kupoka) kisa mtaani zimeadimika? ikumbukwe wafanya biashara Hawa wanazimiliki bidhaa hizo kihalali na wamelipia ushuru Sasa serikali inatumia sheria gani kuwapora?

Tupo kwenye Soko HURIA, Kila mfanyabiashara anahaki ya kuamua mda gani auze bidhaa yake Kama kazipata kihalali!
Kama serikali inataka ku-control si itafte namna ya kukaa chini na hao wafanyabiashara kidemocrasia?

Kama serikali inataka Ku-control bidhaa si Kuna maghara ya Serikali kwanini wasikisanye bidhaa ya kutosha ili ku-balance Soko HURIA?

TULIONA KWENYE SUKARI, SANITIZER NA SASA KWENYE MAFUTA!
Kwanini serikali inatumia njia ya kizamani Sana ya KUTAIFISHA NA KUFUNGIA WATU ambao hawana hatia kwasababu Mali wamezipata kihalali na Kodi wakalipia inakuwaje uwapangie mda wa kuuza?

Mtu anafunga stock either kasafili kaamua kufunga store yanini kumfilisi bidhaa zake halali?

AU Wataalam tusaidiane Hapa, je, Ni SURUHISHO kuwakamata wafanya biashara wanaoficha Mali zaowakati tuko kwenye SOKO HURIA?
 
Nchi Lazima Iwe Na Udhibiti Wa Kila Kitu
Ukisema Soko Huria Haina Maana Wafanye Watakavyo
PopoteUlimwengu Mambo Mengi Sana Hufanyiwa Udhibiti
Hivi,nani alisema wakulima wavune mahindi then wahifadhi waje wayauze msimu wa kiangazi kwa bei kubwa?
 
Nchi Lazima Iwe Na Udhibiti Wa Kila Kitu
Ukisema Soko Huria Haina Maana Wafanye Watakavyo
PopoteUlimwengu Mambo Mengi Sana Hufanyiwa Udhibiti
Ila kwny mambo ya msingi kama kutoa ajira mnajifanya ooh serikali haiwezi kuajiri kila mtu,private sector ndio kazi yake hio kuu.
 
Nchi Lazima Iwe Na Udhibiti Wa Kila Kitu
Ukisema Soko Huria Haina Maana Wafanye Watakavyo
PopoteUlimwengu Mambo Mengi Sana Hufanyiwa Udhibiti
Unadhibiti nini? yaani uchukue Kodi halafu iseme unadhibiti Mali ya uliyemkata kodi kubwa? unataka auze Mali kwa hasara wakati Kodi yako umechukua?
 
inategemea unaliza akili gan Kwan?
Yani uchukue shehena nyingi ya mafuta halafu uipaki kwamba hutaki kuiuza umekuja kufanya biashara au kukomoa wananchi na kuichonganisha serikali.

Huu upuuzi hata nchi zilizoendelea hazifanyi, kukata kodi isiwe sababu ya wewe kujipangia la kufanya na ndo maana kuna msimamizi ambae ni serikali.
 
Wakati nachukua shehena Kuna makubaliano yoyote yakunipangia tarehe za kuuza?
 
Ila ukifuatilia mambo ya wafanya biashara kila wanapotaka kutuumiza serikali ikaingilia unagundua wafanya biashara hawana huruma kabisa kwa raia
 
Wakati nachukua shehena Kuna makubaliano yoyote yakunipangia tarehe za kuuza?
Nawakati unayahodhi ili yaadimike upandishe bei unufaishe tumbo lako wakati sisi walaji/watumiaji tunaumia Kuna makubaliano yeyote ulingia na serikali kuufanya huu wizi?
 
Ila ukifuatilia mambo ya wafanya biashara kila wanapotaka kutuumiza serikali ikaingilia unagundua wafanya biashara hawana huruma kabisa kwa raia
Tatizo siyo wafanyabiashara Ni mfumo! Kama mfanyabiashara anaagiza mzigo kwa bei juu! na ukamkata Kodi ya bei kubwa! Mara ghafla unamtangazia kushusha bei! yaan bidhaa hiyo auze kwa bei ya chini HATA UNGEKUWA NI WEWE UTAUZA?
mfano Bidhaa iko sokoni kwa 2500! unaagiza kwa 2000 mzigo, unalipia ushuru wa bei hiyo, stock ikiwa haijaisha unatangaziwa! Bei elekezi ya kuuza kwa 2000 kutoka kwenye 2500 ya Awali Je UTAUZA? Ikumbukwe usafili na Wafanyakazi mshahara n.k JE UTAUZA?
msiwe mnashsbikia biashara kichaa
 
Nawakati unayahodhi ili yaadimike upandishe bei unufaishe tumbo lako wakati sisi walaji/watumiaji tunaumia Kuna makubaliano yeyote ulingia na serikali kuufanya huu wizi?
mfano Bidhaa iko sokoni kwa 2500! unaagiza mzigo kwa 2000 , unalipia ushuru wa bei hiyo, stock ikiwa haijaisha unatangaziwa! Bei elekezi ya kuuza mzigo wako kwa 2000 kutoka kwenye 2500 ya Awali uliyotarsjia, na risiti utoe Je UTAUZA kwa hasara? Ikumbukwe usafili na Wafanyakazi mshahara n.k JE UTAUZA?
msiwe mnashsbikia biashara kichaa
 
mfano Bidhaa iko sokoni kwa 2500! unaagiza kwa 2000 mzigo, unalipia ushuru wa bei hiyo, stock ikiwa haijaisha unatangaziwa! Bei elekezi ya kuuza kwa 2000 kutoka kwenye 2500 ya Awali Je UTAUZA? Ikumbukwe usafili na Wafanyakazi mshahara n.k JE UTAUZA?
msiwe mnashsbikia biashara kichaa
Unakumbuka mafuta yalivyoshuka chini ya dola moja kwa pipa na bei Tanzania haikushuka? Wafanyabiashara walikuwa na stock kwenye maghala waliachiwa wauze kwa bei ya zamani ili wasipate hasara ndio wakaagiza shehene nyengine wakashusha na bei,na Kwavile mafuta nje ni bei rahisi waliagiza mengi,na soko la dunia bei huwa inabadilika mara nyingi kila baada ya miezi mitatu iwe ni kushuka au kupanda, hii Ni janja ya kutaka kupandisha bei wanufaike,
 
Tatizo siyo wafanyabiashara Ni mfumo! Kama mfanyabiashara anaagiza mzigo kwa bei juu! na ukamkata Kodi ya bei kubwa! Mara ghafla unamtangazia kushusha bei! yaan bidhaa hiyo auze kwa bei ya chini HATA UNGEKUWA NI WEWE UTAUZA?
mfano Bidhaa iko sokoni kwa 2500! unaagiza kwa 2000 mzigo, unalipia ushuru wa bei hiyo, stock ikiwa haijaisha unatangaziwa! Bei elekezi ya kuuza kwa 2000 kutoka kwenye 2500 ya Awali Je UTAUZA? Ikumbukwe usafili na Wafanyakazi mshahara n.k JE UTAUZA?
msiwe mnashsbikia biashara kichaa
Wala hili halihitaji mifano mingi utachanganya tu watu. Kwani hao wauza mafuta wananunua wapi mafuta, si kwenye soko la dunia ambako bei ilifika -something/barrel? Sasa stock uliyoichukua bei ikiwa -something/barrel unalazimishaje uiuze bei sawa na stock ya kipindi bei ni 40-60USD/barrel?
Sijui una maslahi gani katika hili ila wafanya biashara wengi ni walafi sana hua hawana huruma kwa mteja. As long as kwao wanatengeneza faida kubwa hua hawajali factor zingine
 
Back
Top Bottom