Kwa watakaopenda kukumbushwa: JPM alitwambia mara kadhaa "TUSIFIKIRI NA WALA KUJIDAGANYA KUWA ATI TUNAPENDWA SANA" na aliongezea "THERE IS NO FREE LUNCH "under the sky.Kama nimekosea nisahihisheni. Serikali ya Marekani haijatoa rambirambi rasmi kwetu kufuatia kifo Cha Rais Magufuli.
Lakini Marekani inajisogeza Sana kwa mama wakidai kutaka kutupa 'misaada' ya kupambanana korona. Tusiwaonee aibu! Tuwaambie hatuhitaji msaada wa kupambana na korona! Kama Wana Nia ya kutupa msaada watupe pesa zitusaidie kumalizia SGR na mradi wa Stigler's George.
Wakapambane na korona huko kwao maana wao tatizo Ni kubwa kuliko kwetu! Hawa mabeberu hawana aibu.
Marekani ni taifa la ki-NARCISSIST. Lina kicheko cha MAMBA kwa kila mahusiano na mataifa madogo hasa ya Afrika. Ni kiongozi aliyejaa ubinafsi tu ndie anayeweza kudhani kuwa kuna tija kwa mahusiano ya kimkakati na Marekani. Hata Baba wa taifa aliipa mtazamo wenye tahadhari kubwa sana Marekani.
Kilicho wazi ni kwamba; kujisogeza karibu sana na Marekani ni kujiua wewe mwenyewe taratibu na mwisho wa siku Marekani yenyewe inakupa kisogo.