Hii kamata kamata ya watumiaji wa mtandao natolea angalizo hapa.

Shukrani A. Ngonyani

JF-Expert Member
Feb 23, 2014
1,182
2,015
Ni dhahiri isilenge kuwashughulikia wanyonge tu. Isilenge kuwashughulikia wanao kosoa watawala tu.

Isitumike kama tishio dhidi ya wanaohoji mwenendo wa serikali na watawala.

Isitumike kama nyenzo ya kuwaziba midomo wenye mtazamo hasi dhidi ya aina ya demokrasia tuliyonayo kwa sasa.

Ilenge hasa kuweka mizania ya haki na usawa baina ya makundi yote.

Nitajisikia faraja sana na wanaowatukana viongozi waandamizi wa vyama vya upinzani nao wakapelekwa mahakamani na kuhukumiwa.

Karibu ktk mjadala!
 
Watakuja Nyumbu wa Pale ulevi karibu na Mnazi Mmoja kukuporomoshea Matusi
 
Mtu yeyote akajihisi ametukanwa bila kujali ni kwenye mtandao au vinginevyo, ana haki ya kumfungulia mashtaka mtusi wake.
 
Back
Top Bottom