Hii kali: Foleni toka Tazara mpaka External Mabibo

frema120

JF-Expert Member
Jan 1, 2012
5,099
1,338
Nimepita toka Tazara mpaka nimemaliza hapa Mabibo hostel ni foleni ya maana, poleni wote mlio kwenye foleni hiyo.

Askari saidieni tatizo hili, kama mataa ya Tabata hakuna maelewano.
 
Heri yako....cc wa posta tangu saa 11 tupo barabarani.na ndio.kwaaanza salenda bridge
 
Jiji Hili lipo Zigizaga ,bora watu wa mikoani waanze kuwekewa utaratibu wa kuomba Viza kuingia Dar ili wasiokuwa na shughuli maalumu wabaki hukohuko ndiyo wanatuletea foleni hawa
 
Askari wamalizeje na mvua hii usiku huu?
Sisi wepesi sana kusahau.
Kukiwa na askari barabarani tunapiga kelele wasiwepo, wakikaa pembeni tunawahitaji.
Tatizo pia tunaendesha kama hatutumii akili,
unaona njia mbele haiendi ila kuliko umruhusu anaetoka kulia kuja kushoto apite unaona bora ubane asikatishe yani wote mkwame mfunge njia.
 
Au wanaamua kuifanya single lane iwe three lane bila kujali watumiaji wengine!
 
Back
Top Bottom