Hii janja janja ya Boeing iripotiwe na media kubwa duniani

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Sep 30, 2015
1,527
3,810
Wanabodi,

Swala la Boeing kutuuzia ndege za bei ndogo kwa bei kubwa ni kinyume na maadili ya kibiashara, swala hili likivaliwa njuga linaweza kuathiri kabisa reputation ya Boeing.

Kama ni kweli Boeing wameshiriki, tunatakiwa kuhakikisha kwamba media kubwa kama BBC nk wanajua na wanaripoti (kwa kiingereza). Ikiripotiwa italeta shock kubwa sana kibiashara hivyo watachukua hatua

Kwasababu CCM ni sikio la kufa, sisi tuwashe moto Boeing utawaka mpaka CCM.
 
Mkuu hata mimi tangu jana nimepata wazo kama hili kuwa mashirika makubwa ya habari kama BBC nina imani yatawahoji viongozi wa hii kampuni na kuwataka watoe ufafanuzi.

Nina imani swala hili sasa hivi litavuka mipaka maana bila shaka waandishi watakuwa wameanza kulifuatilia.

Soon BBC,VOA,DW,n.k wanaweza kuliriopti.
 
Na liripotiwe sasa..

Maana wao wenyewe Boeing wapo kimya kama vile hakuna kinachoendelea..

Tumechoka kuibiwa.
 
Labda Mungu atasaidia warudishe change Kama BAE na issue ya rada
 
Mkuu hata mimi tangu jana nimepata wazo kama hili kuwa mashirika makubwa ya habari kama BBC nina imani yatawahoji viongozi wa hii kampuni na kuwataka watoe ufafanuzi.

Nina imani swala hili sasa hivi litavuka mipaka maana bila shaka waandishi watakuwa wameanza kulifuatilia.

Soon BBC,VOA,DW,n.k wanaweza kuliriopti.
Hivi umewahi sikia BBC,VOA au DW wakiziponda nchi zao kwa lolote? Wewe hujui mashirika ya kimataifa ya habari linapokuja swala la maslahi ya nchi zao.Huwa kitu kimoja na nchi zao.Unafikiria mashirika hayo ni kama vigazeti uchwara vya Tanzania?

Habari ya shirika kubwa kama boeing haiwezi tinga vyombo vya kimataifa kisa eti mbunge wa ujiji eneo lenye funza wengi kaongea!!!
 
Wanabodi,

Swala la Boeing kutuuzia ndege za bei ndogo kwa bei kubwa ni kinyume na maadili ya kibiashara, swala hili likivaliwa njuga linaweza kuathiri kabisa reputation ya Boeing.

Kama ni kweli Boeing wameshiriki, tunatakiwa kuhakikisha kwamba media kubwa kama BBC nk wanajua na wanaripoti (kwa kiingereza). Ikiripotiwa italeta shock kubwa sana kibiashara hivyo watachukua hatua

Kwasababu CCM ni sikio la kufa, sisi tuwashe moto Boeing utawaka mpaka CCM.
Tuwafungulie kesi ICC hao Boeing haiwezekani wanatumia uwezo wao wa kifedha kurubuni nchi masikini, watu wana njaa halafu wao wanataka kutuuzia ndege.
 
Naripotia Fox News kutoka Afghanistan, nawashangaa ndugu zangu huko Tanzania jinsi mnavyolishwa matango poli na huyo mwanasiasa mchumia tumbo!
 
Mbona ile ishu ya Rada na ile kampuni kubwa ya Uingereza ilijadiliwa tena ikafika na kujadiliwa na bunge la uingereza??

Hakuna kinachoshindikana mkuu.... Wenzetu hakuna janja janja ...
Kweli mzee,wenzetu sio wanafiki kama sisi ukweli wanaweka wazi mfano yule mama wa Uingereza bi Clare Short kuhusu rada
 
Mbona ile ishu ya Rada na ile kampuni kubwa ya Uingereza ilijadiliwa tena ikafika na kujadiliwa na bunge la uingereza??

Hakuna kinachoshindikana mkuu.... Wenzetu hakuna janja janja ...
Wazungu waliziikana pesa za rushwa ya rada wakaamua kufumuana ya tukose wote.Lile swala halikuanzia tanzania lilianzia kwao huko huko.Halikuanzishwa na mbunge wala mtanzania yeyote huku tulikuja kudakia tu
 
Hivi umewahi sikia BBC,VOA au DW wakiziponda nchi zao kwa lolote? Wewe hujui mashirika ya kimataifa ya habari linapokuja swala la maslahi ya nchi zao.Huwa kitu kimoja na nchi zao.Unafikiria mashirika hayo ni kama vigazeti uchwara vya Tanzania?

Habari ya shirika kubwa kama boeing haiwezi tinga vyombo vya kimataifa kisa eti mbunge wa ujiji eneo lenye funza wengi kaongea!!!
Acha uongo mbona RADA wali ripoti hao hao BBC na vyombo vingine?
 
Hivi umewahi sikia BBC,VOA au DW wakiziponda nchi zao kwa lolote? Wewe hujui mashirika ya kimataifa ya habari linapokuja swala la maslahi ya nchi zao.Huwa kitu kimoja na nchi zao.Unafikiria mashirika hayo ni kama vigazeti uchwara vya Tanzania?

Habari ya shirika kubwa kama boeing haiwezi tinga vyombo vya kimataifa kisa eti mbunge wa ujiji eneo lenye funza wengi kaongea!!!
Ishu ya Radar na hii benki ya escrow mbona walizivalia njuga.
 
Hivi umewahi sikia BBC,VOA au DW wakiziponda nchi zao kwa lolote? Wewe hujui mashirika ya kimataifa ya habari linapokuja swala la maslahi ya nchi zao.Huwa kitu kimoja na nchi zao.Unafikiria mashirika hayo ni kama vigazeti uchwara vya Tanzania?

Habari ya shirika kubwa kama boeing haiwezi tinga vyombo vya kimataifa kisa eti mbunge wa ujiji eneo lenye funza wengi kaongea!!!
Jadili hoja wewe,mbona suala la rada lilipigiwa kelele?

Pia wanasiasa na vyama wanatakiwa wawe na international alliance na waandishi wa kimataifa,niliona zitto akisema ana connection na waandishi wa habari za kiuchunguzi wa kimataifa
 
Mimi naamini suala hili kama ni la kweli (Ukweli utajulikana tu) halitaweza kutatuliwa na watanzania. Imeshakuwa ni desturi yetu kufanya mambo ya ovyo ovyo kisha na sisi wananchi tusiojitambua tunashabikia kijinga jinga. Kwani suala la Rada lilikuwaje? Hatukuwasikia mawaziri wa wakati huo wakisema hata tukila nyasi ni lazima rada inunuliwe? Lakini kama mnavyokumbuka, kashfa hii ilifika katika Bunge la Uingereza, na suala hili lilichunguzwa kikamilifu huko na kisha tukarudishiwa chenji yetu. Hiyo ilikuwa ni aibu kubwa, lakini ndivyo tulivyo. Hatujitambui. Sasa hata kwa hili nalo, kuna watu wanaojitambua. Wakipata habari hizi watafuatilia na pengine tutapata chenji kwa mara nyingine.
 
Mkuu hata mimi tangu jana nimepata wazo kama hili kuwa mashirika makubwa ya habari kama BBC nina imani yatawahoji viongozi wa hii kampuni na kuwataka watoe ufafanuzi.

Nina imani swala hili sasa hivi litavuka mipaka maana bila shaka waandishi watakuwa wameanza kulifuatilia.

Soon BBC,VOA,DW,n.k wanaweza kuliriopti.
Kama wewe umepata wazo hilo unafikiri vyombo hivyo havina wawakilishi nchini? Vyombo hivi vinajua website halisi ya boeing na haitoi taarifa hizo. Laiti kama taarifa zitolewazo zingekuwa zinashabihiana na za Zito wangemuita kufanya ufafanuzi. Sasa hivi huu umekuwa ni mchezo wa humu jf kuvutia muda tu. Kila mmoja anajifungulia kijiwe kuhusu ndege nasi tunaingia tunatupia mawili matatu siku inaenda.
 
Back
Top Bottom