kyanyangwe
JF-Expert Member
- Oct 31, 2018
- 1,147
- 2,746
- Thread starter
- #41
Vipi,hiyo kazi ulipata boss?Ila hizi interview hizi, some years back nikiwa huko Mtwara maisha yamekaba kila idara, jamaa yangu akanitumia job advert from NGO moja inahitaji watu kwa fani mbalimbali. Nikaona one of the vacancy posts ni eneo langu la kujidai, faster nikatengeneza CV ili iendane na hitaji lao,then nikawatumia pamoja na cover letter. Yaani the same day jamaa waka acknowledge kupokea maombi yangu na kuambiwa nikipita mchujo nitaitwa na kama sitaitwa ndo nijue sikubahatika. Basi bwana nikakaa miezi miwani ikapita nikajua ndo ntolee hiyo nimekosa but ghafla nikapigiwa simu na kuambiwa nicheki email kwani natakiwa kwa interview. Kucheki email kumbe kweli bwana imetumwa two days ago nami nilikuwa sijacheki. Nikatafuta nauli nikafunga safari to Dar, nikafika wakanielekeza nikafika kwenye ofisi yao. Baada ya nusu saa nitaitwa kwenye ukbumbi kuna watu 5 wazungu 2 wengine wabongo wenzetu, aisee walinikaanga kwa maswali for more than two hours. Mwisho wakanishukuru na kuniambia niingie chumba kingine, nikapelekwa kwenye computer nikapewa karatasi yenye maswali ya kujadili issues mbalimbali kama conflicts management, funds management etc kwa muda wa robo saa nikimaliza niisevu hiyo kazi kwa format fulani na jina fulani and then niitume kwenda email niliyopewa pale. Nikakomaa nikamaliza na kuipa jina, nikaisevu na kutuma. Baada ya kumaliza yote nikapelekwa idara ya fedha nikaambiwa jazi hii fomu aisee sikuamini wale jamaa wakanilipa night allowance mbili za Dar kwa rate ya 100,000 enzi hizo per night. Pia nikaulizwa una tiketi ya Bus, nikachomoa tiketi nikawapa wakanirudishia nauli ya kuja na kurudi, yaani sikuamini kabisa!!