Hii inawezekanaje, mwanaume ufunge ndoa na mtu alafu usifanye nae tendo la ndoa?

Mahondaw

JF-Expert Member
Apr 9, 2013
61,944
156,095
Jamani Jamani Jamani hivi kuna ukweli hapa au ndo kufanya mtu ni poyoyo tena mtoto mdogo kabisa kiasi kwamba upeo wakufikiri ni mdogo sana!
Nihivi, eti wewe mwanaume ulimpa binti mimba! Kwa madai yako eti sawa ulimpa mimba lakini hukuwa na mpango naye. Wewe mwanaume bado unaishi kwenu na huyo binti ulimpachika huo mzigo ukiwa kwenu sasa mimba pembe la ng'ombe bana haifichiki ng'o siku ya siku likabumbuluka binti kabanwa mzigo wa nani kakutaja.

Wakati huo wazazi wako wewe mwanaume ni wana dini sanaa na mbaya zaidi wazazi wako ni viongozi wa kanisa hawataki kuaibika mtaani. So ndugu wa binti wakaja kwenu kutoa taarifa kwa wazazi wako kuwa wazee kijana wenu keshaharibu binti yetu hukoo. Wazee wako wakasema ahaa hamna tatizo mlete huyo aje akae hapa kwetu na kijana mwenzie. Binti kaletwa hapo wazazi wakafanya mpango wakamwita padri kawafungisha ndoa ndo mkeo huyo kuanzia mpeane mimba leo padri kahalalisha tu.

Sasa yawezekanaje useme huyo binti eti humpendi ni kwakua wazazi tu waliamua kumleta kwenu na kawafungisha ndoa ila hayupo moyoni mwako? Wakati huo na Pete yake ya ndoa unayo kabisa kidoleni kwako? Inawezekanaje mnaishi nyumba moja useme eti hufanyi nae mapenzi analea mtoto tu eti mnalala vyumba tofauti kwani nyumba ni kubwa?

Inawezekanaje binti yupo kwenu kama mkeo huu mwaka wa Tatu sasa eti hamshiriki tendo la ndoa inamaana akibanwa na nyegezi kona inakuaje? Akikufata unakimbiaaaa! Unampigaa! Ama veepee imekaaje hii? Nawewe haja zako unamalizia wapee? Au ndo unamega kisela ila tamaa zako tyu?

Chakushangaza mwanaume unapatikana muda na masaa yote huyo mwanamke mwingine akikwambia kuchati masaa yoyote yale we freshe tu kuongea usiku wa manane we freshe tu akikuhitaji kwake hata miezi we fresh tu akihitaji chochote kile wee fresh tu akihitaji miamala we fresh tu Kaka miamala.

Chakushangaza zaidi na zaidi sasa wewe mwanaume leo hii umesimamia ukucha eti unataka kuoa tena kwa madai huyo mtarajiwa ndo chaguo lako la moyo na si yule ilhali yule ushafungishwa nae ndoa tena ya kikristo? Umuweke wapi kwa wazazi wa nani? Kwa ndugu wanani ilhali kwenu wanamjua kabisa mkeo na mbaya zaidi yupo kwenu? Nahii juzi tu huyo mkeo kaona sms zote unazochati na huyo unaedai ndo chaguo lako kachukua namba yake kamtafuta kumwambia naomba uachane na mume wangu huyo uliemuagiza mikate na pedi (ni baadhi tu ya vitu ulivyoagizwa huyo mwanamke wakumoyo)

Ofcourse you are so lovely, sexy,sweet, patient understanding a man of focus, mpole, mission town ful kujituma kusaka katika pesa, genius genius genius in all aspects of life ila dah! Man so sorry your situation is very complicated kwakweli! Kweli hii inaingia akilini kama wewe ndo mwanamke huyo mtarajiwa na wewe mwanamke wa kupewa mimba tu unakaaje sehemu kama hiyo ukiwa na akili timamu? Nawewe mwanaume niaje hapa?

Maoni yako tafadhali.

NAWASILISHA
 
Freshe tyu

Freshe ipi sasa kukubali kulala tofauti na mumeo wee unahangaika na mikojo ya mtoto yeye yuko kwingine anachati na mwanamke mwingine?? Au yeye kasafiri hata Mwezi yupo tyu huko kwa mwanamke mwenzio??
 
Freshe ipi sasa kukubali kulala tofauti na mumeo wee unahangaika na mikojo ya mtoto yeye yuko kwingine anachati na mwanamke mwingine?? Au yeye kasafiri hata Mwezi yupo tyu huko kwa mwanamke mwenzio??

Huyo kashakudondokea, maamuzi ni juu yako!
 
Hakuna formula sahihi ya kumtafsiri mtu. Huyo kijana nashindwa kumuweka kwenye kundi gani.

Muacheni afanye atakavyo, ndio maisha aliyoyachagua. Endeleeni kumuombea atambue kosa analotaka kulifanya kabla hajachelewa.

Huyo binti aliyefunga nae ndoa aondoke tu akaanze kivyake. Asilazimishe ndoa, hakuna cha maana atakachokipata huko.
 
Back
Top Bottom