Hii inasikitisha, yaani kiwanda kikubwa kama hiki kinalipa Watanzania Tshs. 3800 kwa siku!

Elfu moja mia tano nalipwa kibaruani,haitoshi kodi ya mezani,halafu mnasema tuidumishe amani,amani itatoka wapi wakati mwenzenu unyumba haupatikani...Song by Nash Mc...Kaka Suma.

Kwa wasio elewa ni kwamba kazi za viwandani ni kuiba kila siku ili u survive, unaangalia gape unapiga chochote na kwenda kuuza mara nyingi mnashirikiana, la sivyo hata kupanga hautoweza utafukuzwa kwenye chumba/nyumba ya watu...na kupata hicho kibarua ni lazima uhonge.

Juzi kati kuna madogo walienda sehemu kuomba kazi ya zege wakaambiwa 7000 hawataki waache,halafu wakalipwa kwenye simu sasa bila kupewa na ya kutolea.
 
Serikali yenyewe inalipaje watumishi wake kwanza.....!
Serikali inamlipa mbunge milioni 11 kwa mwezi.
Mkuu wa wilaya milioni nyingi na Viieite juu.
Waziri milioni nyingi na allowance kibao ndio maana wanajitoa ufahamu.
Wakurugenzi milioni nyingi na Viieite.
Walimu milioni mbili.
Madereva laki sita na posho kibao.
Ki ufupi hakuna mfanyakazi wa serikali anayepata chini ya laki tano
 
Huwa nikimuona mzee baba anapromoti wawekezaji waje wajenge viwanda wana wapate ajira huwa najisemea tu khee!
 
40 in thirty days. Kweli ataoa mke huyu?
Hivi Kuna siku anaeasimulia wenzie kwamba ali enjoy, yaani Kama kwenda kunywa soda na girlfriend sehemu au kula ice cream au hata kutoka kwenda muziki na washkaki?
I cant imagine dah
 
Serikali inamlipa mbunge milioni 11 kwa mwezi.
Mkuu wa wilaya milioni nyingi na Viieite juu.
Waziri milioni nyingi na allowance kibao ndio maana wanajitoa ufahamu.
Wakurugenzi milioni nyingi na Viieite.
Walimu milioni mbili.
Madereva laki sita na posho kibao.
Ki ufupi hakuna mfanyakazi wa serikali anayepata chini ya laki tano
Milioni 2 walimu wa kufundisha nini?
 
Wakuu ukoloni bado upo, hawa wahindi sio watu kabisa. Hivi kweli mfanyakazi anafanya kazi masaa 12 halafu unamlipa 3800 sasa hiyo pesa atafanyia nini.

Kwa kweli mtaani hali ni mbaya kama kweli tungekuwa uchumi wa kati hakuna mtanzania angeenda kufanya kazi kwa hao mashetani.

Chakushangaza kampuni yenyewe ni kubwa(sayona) huwezi hata ifikiria, kila siku inapigiwa promo/vinywaji na msanii mkubwa/Yuda

Serikali ya wanyonge iko wapi, hivi imeshindwa kuweka watu wa kumonitor na kuregulate mishahara ya wafanyakazi wasio rasmi. Kama ilivyoweka kwenye kitengo maalum cha kukusanya mapato

Mishahara mizuri mizuri wanalipana wao na ndugu zao lakini ngozi nyeusi unakula 3800 na ukikaa hata siku moja utoro/ukiugua wanakukata mwisho wa mwezi.
HR wengi ni wanafiki wala musiwaraumu hao Wahindi. Mchawi ni mweusi mwenzio
 
Kwakweli ni heri nikalime miti kijijini kuliko kutumikishwa na Wahindi na Wachina.
Idiots.
Ni heri ungetaja jina la kiwanda ili kama kuna ufuatiliaji iwe simple.
Unanishauri nini mimi ninayefanya kazi kwa mhindi?
 
Hivi viwanda vingekua vinafikisha efu 10 kwa siku vijana wasio na kazi wangepungua sana kitaa ila haya mambo ya 3800 yanafanya watu waone ufala bora wa bet....
 
Kama ni Per Day dhahiri ni Unyonyaji

Lakini sasa tutafanye kuepuka huko , mwananchi anaona bora ajipatie hiyo 3800 kuliko kusubiri kisichosubirika

Hamna cha Uchumi wa kati wala Tantariraa nyingi
 
Kuna bwana mmoja pale kariakoo alikuwa analipwa na mhindi 50,000/= kwa mwezi lakini sikuwahi kumsikia akilalamika....kumbe yule bwana kwa siku alikuwa na uhakika wa kuondoka na 50,000/= mpaka 100,000/= kwa njia anazozijua mwenyewe........hapo ndio nikajifunza jambo kubwa sana kwenye ajira za wahindi na wachina........
 
Two different environment
 
Hivi viwanda vingekua vinafikisha efu 10 kwa siku vijana wasio na kazi wangepungua sana kitaa ila haya mambo ya 3800 yanafanya watu waone ufala bora wa bet....
Hivi unajua hata kwa malipo hayo kuna watu wengi huko na hamna gape?
Kupata kwenyewe mpaka uhonge kwa nyapara(mbongo).
 
Back
Top Bottom