Hii inamuhusu kila mwanaJF, ni muhimu...

Manselly

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
456
130
Habari wana jf.
Kumekua na mkanganyiko sana katika lugha tunazotumia wana jf hasa kuhusiana na watu wenye ulemavu. Kwa kutumia taaluma yangu nimeona bora nitoe darasa na yeyote mwenye swali au maoni awe huru kuuliza. Ni ufafanuzi wa majina sahihi ya watu wenye ulemavu
1. Albino
Huyu ni mtu mwenye ulemavu wa ngozi na anatambulika sana kwa muonekano tu. Tafadhali usimuite ZERUZERU, dili, mzungu au majina mengine yanayodhalilisha utu wake. Jina sahihi ni albino au mwenye ulemavu wa ngozi.
2. Kiziwi
Huyu ni mtu mwenye upungufu wa usikivu either hasikii kabisa au ana usikivu kidogo (residual hearing). Hawa wanatambulika hasa kwa kutembea makundi makundi na wanatumia lugha ya alama (nyie mnaita lugha ya ishara au mikono). Ni mara chache sana kumkuta kiziwi anatembea peke ake .Usimuite BUBU au ASIYESIKIA (huyu ni kiburi). Tafadhali muite kiziwi ndo jina lenye heshima kwake.( nahitaji maswali mengi sana kuhusu kundi hili maana nalifahamu kuliko makundi yote hapa).
3. Asiyeona
Usithubutu kumuita KIPOFU maana kipofu ni mjinga wa jambo fulani ndo mana tuna vipofu wa mapenzi nk. Muite asiyeona tu lina heshima na hadhi na hawa wanatambulika sana kwa fimbo nyeupe maalum wanayotumia kutembelea au wanakua na muongozaji.
4. Mwenye ulemavu wa akili
Usimuite taahira, ndondocha, au chizi. Hakupenda kuwa ivo ila jina sahihi ni mwenye ulemavu wa akili na hawa wako makundi tofauti kama wale wenye autisim na mental retardation ni watu wawili tofauti japo wote ni wenye ulemavu wa akili.
N.B. Kuna aina nyingi sana za ulemavu siwezi kuzianisha hapa ila tuwe waangalifu kwa majina tunayotumia kuwaita hawa wenzetu wenye ulemavu manake wenyewe wanasema kila mtu ni mlemavu mtarajiwa so take care. Nakaribisha maswali na maoni
 
Ahsante sana mkuu lakini thread kama hizi huwa zinakosa wachangiaji yaani siasa imeingia kila sehemu.
 
yes shukrani sana kwa kuisoma ni vyema kutumia taaluma zetu kuifundisha jamii manake tv zetu zinaonyesha bongofleva tu na vingine eti bibi bomba wakati kuna mambo kibao ya kujifunza
 
Tunashukuru kwa Taarifa Ila kunakitabu nilimnunulia Mtoto cha kiswahili kinaitwa TAKADINI hili jina vipi kwenye ili la Namba Moja.
 
Ahsante sana mkuu lakini thread kama hizi huwa zinakosa wachangiaji yaani siasa imeingia kila sehemu.

naelewa mkuu ndo tz yetu hii ingekua thread ya kugegedana au ufisadi ungeshangaa watu ambavyo wangejaa humu hata ivo nikielimisha hata wachache inatosha watakua mabalozi kwa wengine
 
Habari wana jf.
Kumekua na mkanganyiko sana katika lugha tunazotumia wana jf hasa kuhusiana na watu wenye ulemavu. Kwa kutumia taaluma yangu nimeona bora nitoe darasa na yeyote mwenye swali au maoni awe huru kuuliza. Ni ufafanuzi wa majina sahihi ya watu wenye ulemavu
1. Albino
Huyu ni mtu mwenye ulemavu wa ngozi na anatambulika sana kwa muonekano tu. Tafadhali usimuite ZERUZERU, dili, mzungu au majina mengine yanayodhalilisha utu wake. Jina sahihi ni albino au mwenye ulemavu wa ngozi.
2. Kiziwi
Huyu ni mtu mwenye upungufu wa usikivu either hasikii kabisa au ana usikivu kidogo (residual hearing). Hawa wanatambulika hasa kwa kutembea makundi makundi na wanatumia lugha ya alama (nyie mnaita lugha ya ishara au mikono). Ni mara chache sana kumkuta kiziwi anatembea peke ake .Usimuite BUBU au ASIYESIKIA (huyu ni kiburi). Tafadhali muite kiziwi ndo jina lenye heshima kwake.( nahitaji maswali mengi sana kuhusu kundi hili maana nalifahamu kuliko makundi yote hapa).
3. Asiyeona
Usithubutu kumuita KIPOFU maana kipofu ni mjinga wa jambo fulani ndo mana tuna vipofu wa mapenzi nk. Muite asiyeona tu lina heshima na hadhi na hawa wanatambulika sana kwa fimbo nyeupe maalum wanayotumia kutembelea au wanakua na muongozaji.
4. Mwenye ulemavu wa akili
Usimuite taahira, ndondocha, au chizi. Hakupenda kuwa ivo ila jina sahihi ni mwenye ulemavu wa akili na hawa wako makundi tofauti kama wale wenye autisim na mental retardation ni watu wawili tofauti japo wote ni wenye ulemavu wa akili.
N.B. Kuna aina nyingi sana za ulemavu siwezi kuzianisha hapa ila tuwe waangalifu kwa majina tunayotumia kuwaita hawa wenzetu wenye ulemavu manake wenyewe wanasema kila mtu ni mlemavu mtarajiwa so take care. Nakaribisha maswali na maoni

Nakubaliana nawe lakini hapo kwenye RED nimewahi kuongea nao,
wao wenyewe ndani ya chama wanapingana, wapo wanaoona kuwa
jina hili ni tatizo lakini wengine hawaoni kama lina ubaya wowote...
 
Mkuu Manselly hapo kwenye namba 2 naomba nikukosoe, umesema kiziwi ni mtu asiyesikia kabisa au asiyesikia vizuri.
Kwa kukuelewesha tu kiziwi ni mtu asiyesikia kabisa(hata kidogo) sawa na kusema Kipofu ukimaanisha mtu asiyeweza kuona kabisa.
 
Last edited by a moderator:

Kwa kukuelewesha tu kiziwi ni mtu asiyesikia kabisa(hata kidogo) sawa na kusema Kipofu ukimaanisha mtu asiyeweza kuona kabisa.Nafikiri umenielewa.
 
Last edited by a moderator:
Tunashukuru kwa Taarifa Ila kunakitabu nilimnunulia Mtoto cha kiswahili kinaitwa TAKADINI hili jina vipi kwenye ili la Namba Moja.

naelewa mkuu. Kwa kipindi kirefu watu wenye ulemavu walikua hawajui haki zao na elimu inayowahusu hawa watu ilikua haijulikani lakini kwa sasa wameamka na wanatetea haki zao so huyo muandishi alikua hajui hili na ndo mana hata bible inasema bathimayo kipofu. Hatuwez kufuta na kubadili yaliyokwishwa andikwa ila habari ndo hiyo lugha ni lazma ibadilike kulinda hadhi ya watu
 
Mkuu Manselly hapo kwenye namba 2 naomba nikukosoe, umesema kiziwi ni mtu asiyesikia kabisa au asiyesikia vizuri.
Kwa kukuelewesha tu kiziwi ni mtu asiyesikia kabisa(hata kidogo) sawa na kusema Kipofu ukimaanisha mtu asiyeweza kuona kabisa.Nafikiri umenielewa.

sasa zeruzeru tumuite kwa jina gani la mkato kwa kiswahili? maana albino ni jina la kizungu. Jamani tuache mawazo mgando km mtu anaulemavu ni vyema akakubali mapungufu Allah aliyomjaalia badala ya kuanza kuhangaika na watu
 
Nakubaliana nawe lakini hapo kwenye RED nimewahi kuongea nao,
wao wenyewe ndani ya chama wanapingana, wapo wanaoona kuwa
jina hili ni tatizo lakini wengine hawaoni kama lina ubaya wowote...

walivyopinga neno kiziwi walikupa jina gani mbadala mkuu?sio kila kiziwi anajielewa mimi huwa nafanya kazi na chama cha viziwi makao makuu pia so ndo mana kinaitwa chama cha viziwi hilo ndo jina rasmi wanalotumia
 
Mkuu Manselly hapo kwenye namba 2 naomba nikukosoe, umesema kiziwi ni mtu asiyesikia kabisa au asiyesikia vizuri.
Kwa kukuelewesha tu kiziwi ni mtu asiyesikia kabisa(hata kidogo) sawa na kusema Kipofu ukimaanisha mtu asiyeweza kuona kabisa.

sio kweli kaka. Kiziwi kwa kiingereza anaitwa Deaf na uziwi unapimwa kwa mashine inaitwa aodiometer na kurekodiwa kwenye chat inayoitwa aodiogram. Uwezo wa kusikia unapimwa kwa decibels na mtu akifikisha decbels 90 anakua total deaf na viziwi hawa wapo kwenye makundi ya mild, modreate na profound lakn wote ni viziwi. Ukisha kua na upungufu wa kusikia tu unasajiliwa kwenye shule za viziwi ukibisha nenda shule ya viziwi buguruni ingia darasani kimya kimya wasikuone then dondosha chupa wapo watakaosikia japo wapo kwenye darasa la viziwi na ni viziwi japo wapo kwenye mild au moderate sio profound
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Manselly hapo kwenye namba 2 naomba nikukosoe, umesema kiziwi ni mtu asiyesikia kabisa au asiyesikia vizuri.
Kwa kukuelewesha tu kiziwi ni mtu asiyesikia kabisa(hata kidogo) sawa na kusema Kipofu ukimaanisha mtu asiyeweza kuona kabisa.Nafikiri umenielewa.

ukibisha ingia google search for types of deafness utathibitisha kuwa kiziwi sio lazma awe total deaf
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom