Habari wana jf.
Kumekua na mkanganyiko sana katika lugha tunazotumia wana jf hasa kuhusiana na watu wenye ulemavu. Kwa kutumia taaluma yangu nimeona bora nitoe darasa na yeyote mwenye swali au maoni awe huru kuuliza. Ni ufafanuzi wa majina sahihi ya watu wenye ulemavu
1. Albino
Huyu ni mtu mwenye ulemavu wa ngozi na anatambulika sana kwa muonekano tu. Tafadhali usimuite ZERUZERU, dili, mzungu au majina mengine yanayodhalilisha utu wake. Jina sahihi ni albino au mwenye ulemavu wa ngozi.
2. Kiziwi
Huyu ni mtu mwenye upungufu wa usikivu either hasikii kabisa au ana usikivu kidogo (residual hearing). Hawa wanatambulika hasa kwa kutembea makundi makundi na wanatumia lugha ya alama (nyie mnaita lugha ya ishara au mikono). Ni mara chache sana kumkuta kiziwi anatembea peke ake .Usimuite BUBU au ASIYESIKIA (huyu ni kiburi). Tafadhali muite kiziwi ndo jina lenye heshima kwake.( nahitaji maswali mengi sana kuhusu kundi hili maana nalifahamu kuliko makundi yote hapa).
3. Asiyeona
Usithubutu kumuita KIPOFU maana kipofu ni mjinga wa jambo fulani ndo mana tuna vipofu wa mapenzi nk. Muite asiyeona tu lina heshima na hadhi na hawa wanatambulika sana kwa fimbo nyeupe maalum wanayotumia kutembelea au wanakua na muongozaji.
4. Mwenye ulemavu wa akili
Usimuite taahira, ndondocha, au chizi. Hakupenda kuwa ivo ila jina sahihi ni mwenye ulemavu wa akili na hawa wako makundi tofauti kama wale wenye autisim na mental retardation ni watu wawili tofauti japo wote ni wenye ulemavu wa akili.
N.B. Kuna aina nyingi sana za ulemavu siwezi kuzianisha hapa ila tuwe waangalifu kwa majina tunayotumia kuwaita hawa wenzetu wenye ulemavu manake wenyewe wanasema kila mtu ni mlemavu mtarajiwa so take care. Nakaribisha maswali na maoni