Hii inamaanisha nini kwa serikali kutangaza bajeti kubwa Bungeni wakati hizo fedha hazitolewi zote?

Nteko Vano

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
434
111
Hali hii imejitokeza mwaka wa fedha huu unaoisha na ule wa 2010/11. Je, na mwaka huu tutegemee hali hiyo hiyo maana waziri wa fedha ametangaza kutenga tri.15.
 
nadhan wabunge wanachotakiwa kukifanya ni kuikataa bajet mpya mpaka hazina watoe pesa zote za bajet iliyopita
 
Serikali ya ajabu sana hii iliyojaa usanii kila sehemu! Kuna baadhi ya mafungu hayakupata hata senti kwenye halmashauri mbali mbali kwa bajeti ilnayokwisha na hivyo miradi michache sana ya maendeleo ilitekelezwa, au haikutekelezwa kabisa. Sasa wanakuja na matrilioni mengine, watayatoa wapi? Kama ilivyo kawaida ya bunge linaloongozwa na magamba watapitisha bajeti hii, wala hawatahoji yatokanayo na bajeti ya mwaka unaoisha kabla ya kuipitisha hii. Wananchi tunazidi kuwaangalia wanavyobehave! Hukumu yao itakuwa kali kwa huu usanii wanaoufanya.
 
Back
Top Bottom