Hii imekaaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii imekaaje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kindafu, Jun 30, 2011.

 1. k

  kindafu JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,114
  Likes Received: 866
  Trophy Points: 280
  Nawasalimu wana JF!

  Jana tarehe 29.06.11, nilisoma kwa mshangao habari iliyoandikwa kwenye gazeti la Tanzania Daima kwamba serikali inamlipia waziri mmoja hotelini zaidi ya Tsh. Hamsini millioni (50,000,000.00) kwa mwezi kwa ajili ya malazi na chakula.Na pengine huyo ni mmoja tu kati ya wengi wanaotanua maeneo mbali mbali nchini na nje ya nchi.

  Cha kusitisha zaidi swala hilo lilipoibuliwa bungeni mtendaji mkuu wa serikali yaani waziri mkuu Mizengo Pinda alijifanya kushtuka kwamba hana habari hizo!!! Na mpaka leo sijasikia mtu yeyote aliyewajibishwa kuhusu swala hilo.

  Binafsi nashangaa wanaharakati bado hawachukua hatua za kutuhamasisha tuandamane mpaka Ikulu kuidai serikali iwajibike kwani tuliichagua ili isimamie rasilimali zetu kwa manufaa yetu sote, na sio kwa ajili ya wachache kujitanua kiasi hicho!! Hizi pesa sio za Kikwete,wala Serikali yake,wala chama chake cha CCM bali ni kodi zetu wananchi.

  Yaani sisi tuendelee kukamuliwa kodi kwa kila kitu ili wao wapate za kutanua wajameni?? Wana JF, Great Thinkers hii imekaaje???? Na tufanye nini ili serikali isiendeleze haya masihara?
   
Loading...