Hii imekaaje! Waziri Ghasia kuwashtaki kwa Rais wabadhirifu ambao yeye anawaongoza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii imekaaje! Waziri Ghasia kuwashtaki kwa Rais wabadhirifu ambao yeye anawaongoza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkeshaji, Mar 23, 2011.

 1. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wakuu Salaam,
  Katika ratiba yake ya kutembelea wizara mbalimbali, jana Rais Kikwete alikutana na Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Mh. Hawa Ghasia na watendaji wa wizara yake.

  Kama ilivyokuwa kwenye wizara nyingine alizotembelea, Mh. Rais alipewa taarifa mbalimbali kuhusu wizara hiyo. Mojawapo ya mambo aliyoelezwa Rais Kikwete ni kuhusu Ufisadi wa fedha za serikali zaidi ya bilioni tisa kulikofanywa na watumishi wa wizara hiyo kwa kuajiri watumishi hewa na kulipa mishahara hewa kwa miaka kadhaa.

  Kilichonitatiza mimi ni jinsi Mh. Hawa Ghasia alivyokuwa akilalamika mbele ya Mh. Rais kuhusu ufisadi huo ambao kiukweli umefanywa na watendaji ambao wako chini yake na ambao yeye anawaongoza.

  Kutokana na hicho nilichokiona/kukisikia nimetatizwa na maswali yafuatayo:
  1. Je Mh. Hawa Ghasia ameshindwa kuwaadabisha/kuwachukulia hatua za kisheria watendaji wake hadi aende kulalama kwa Mh. Rais? Au hilo halimo ndani ya majukumu yake? Au na yeye ni sehemu ya huo ufisadi?
  2. Kama yeye ameshindwa anadhani ni nani anapaswa kuwawajibisha?
  3. Kama hilo lilikuwa ndani ya majukumu yake, je kuna haja gani ya yeye Ghasia kuendelea kuwepo kwenye hiyo nafasi?
  4. Kama Mh. Rais asingetembelea wizara, je Mh. Ghasia angelifumbia macho ufisadi huo. Au angelifanya nini?

  Yote kwa yote inajengeka picha kuwa viongozi wetu hawana "DNA" ya uwajibikaji mpaka pale kutakapokuwa na nguvu ya kuwafuata nyuma.
  Je hali hii itaendelea hadi lini?
  Je tunahitaji kuwa na viongozi ambao wanashindwa kuchukua maamuzi ya kuwaadabisha/kuwawajibisha watendaji wao hadi wakaombe ruhusa kwa mtu fulani?

  Viongozi badilikeni,...la sivyo!

  Wasalaam.
   
 2. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #2
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Huyu Hawa ni ndugu wa Salma....
   
 3. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2011
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ... ni jinsi JK alivyoiponda TAKUKURU kwamba wakipewa jukumu la kufwatilia wizi wa BILIONI tisa za wafanyakazi hewa WATATUMIA zaidi ya miezi nane kuchokonoa makaratasi tu bila kuonesha matokeo!!

  Source: taarifa ya habari kuhusu ziara ya Prezdaa
   
 4. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,071
  Trophy Points: 280
  Kweli na mimi kuna sehemu nimeisoma, na nikawa kama naota vile! Kikubwa hapa hata ukiangalia Kikwete na waziri wake unaona wazi kuwa ni MAIGIZO na wote wanajua kinachoendelea. Ni dhahiri inahitajika nguvu zaidi ya hii tuliyonayo sasa kuleta mabadiliko la sivyo tutakuwa taifa la mwisho kutambulika.
   
 5. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  kwani sheria za wizi serikalini hazijui, huyo kazi imemshinda, ana behave kama class monitor kusemea wenzake kwa mwalimu na wakati vyombo vya sheria vipo....

  kwani rais yeye ananguvu gani dhidi ya wezi serikalini ambayo yeye kama waziri hana?

  yeye achukue hatua, rais JK akiamua am-Magufuli (kumzuia) basi ...lakini kama kila kitu anakimbilia kwa rais , si bora atolewe tu rais afanye kazi mwenyewe...
   
 6. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,717
  Likes Received: 1,627
  Trophy Points: 280
  kilichonifurahisha jana ni kushushuriwa kwa HG kuwa kama JK asingefika hapo wizarani bil 9 za watumishi hewa angezitaja nani au angeacha mambo yakaenda kimya, yeye kajibu kawapa kazi takukuru, Rais kajibu hii takukuru kimeo ambayo hukaa na na fail moja wanazunguka nalo miaka nane na hizo bil 9 si zitakuwa zimetumika na kuisha bila wahusika kuchukuliwa hatua, JK alionyesha ni Jinsi gani Hwa Ghasia ni Ghasia tupu katika wizara hii, inaonekana haiwezi kama hawezi kuchukua hatua muhimu wakati anajua TAKUKRU Yetu ni KIMEO ORIGINAL na kichaka cha kutetea UFISADI, hivyo JK hana Imani na Waziri Ghasia wala Imani na TAKUKUKURU
   
 7. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ja-Kaya nae aache kuzingua watu.......kama TAKUKURU anajua ni wazembe kwa nini hadi leo kawaacha

  Haoni kuwa anajidai kuonesha ungangari wakati ndio anafunua udhaifu wake hata ambao hawauoni sasa waanze kuuona?

  TAKUKURU yeye ndie anaewateua na kama wanaboronga anawaacha nini sasa si angewabadilisha basi tujue moja?

  Kwa tafsiri yangu ni kuwa TAKUKURU wana nafuu kuliko yeye, maana yeye ndie anaewafuga
  ....
   
 8. m

  mang'ang'a JF-Expert Member

  #8
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Nadhani haya ndiyo matokeo ya kupewa kazi kwa ngono, sasa anataka nani afanye kazi yake? na ikifanywa na mtu mwingine atakua na sababu ya yeye juwepo hapo au lupango kwa uchunguzi.KAMAUNAFANYIKAGA LAKINI.
   
 9. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hii script imejaa ghasia tupu, waziri anashitaki wakora waloko ndani ya wizara yake kwa Raisi. Amesahau majukumu yake kama waziri; zigo amewasukumia Takukuru. Raisi anaponda Takukuru inayolipoti kwake na yeye mwenyewe ndiye anayeteua watendakazi ktk hiyo Takukuru. Nina smel ghasia tupu ktk hili. Kuna haja ya kuwa na Wizara 5 tu zinatutosha sana, hizi wizara utitili na mambo yenyewe ki-ghasia ghasia; na wote hao wanahitaji VX V8
   
 10. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  bunge lilitaka bosi takukuru awajibishwe sakata la richmond; jk akakauka. Leo hawa takukuru anawaona hawafanyi kazi haraka/vizuri????!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Siamini kuwa haya yanatoka mdomoni mwake.
   
 11. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hivi haya malipo hewa si ni wizi tu wa kawaida? Kama hivyo ndivyo kwanini husiripotiwe polisi badala ya TAKUKURU? Mimi naona hapa hakunadhamira ya kweli ya kulishughulikia tatizo hilo, kinachofanyika ni kupoteza lengo tu.
   
 12. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Sasa wanafanya kazi gani hao akina ghasia na takukuru. Wanakula pesa ya bure. Nchi hii, we acha tu.
   
 13. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Mnapoambiwa kuwa watu wanapewa madaraka lakini hawana uwezo mnafikiri ni majungu?

  Ktk hili kuna vitu viwili. Moja mfumo wa uteuzi ulipo pili ni uwezo binafsi wa watendaji hususani mawaziri. Kwa utaratibu uliopo mwanachama yeyote wa chama tawala anaweza kuteuliwa kuwa waziri. Ndio maana unaona leo mtu yuko mifugo kesho ulinzi mtondogoo fedha. Ktk ulimwengu wa leo hapo hakuna kitu.

  Mambo muhimu kama people conceptual and technical skills huwa haviangaliwa kabisa.
   
 14. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nadhani pia kuna suala la kujuana. huyu ni mtoto wa mjomba, huyu ni shemeji, huyu sijui mchumba....! Tutafika?
   
 15. Margwe

  Margwe JF-Expert Member

  #15
  Mar 28, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hivi wikileaks walisemaje vile kuhusu JK na hosea?
   
Loading...