Hii imekaaje wanawake wenzangu? Eti the early you accept polygam is better!

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
15,354
2,000
mamad.

Ni hivi, wanawake wengi wamejingewa au wamejijengea woga kuhusu mitaala kutokana na uchoyo na ubinafsi tabia ambayo ni asili ya binadamu, mfano ni asili ya binadamu kuogopa kifo huku anatamani kuingia peponi, utapataje pepo bila kufa??!!.

Katika Uisilamu ndoa ya mitaala inalo sharti moja la UADILIFU, mume anapokuwa na HAJA au ulazima wa kuongeza mke ni lazima ahakikishe kwamba atawatendea mahitaji yao kwa uadilifu kama hatoweza uadifu Qur'an inasema; Ni BORA abaki na mmoja vinginevyo kwake mitaala itakuwa ni kiwanda cha kujitengenezea madhambi.

Ni Zipi Haja na faida za kuoa mke zaidi ya mmoj:-

1-----Wanawake ni wengi duniani kuliko wanaume, Mungu hakuumba hivyo kwa makosa bali makusudio maalumu kuendeleza uzao wa watu duniani inabidi uwiano uwe hivyo na hata kwa wafugaji wa ng'ombe, kuku nk, ili kuendeleza uzao kwa mifugo yao utakuta Madume mawili kwa majike wengi au jogoo mmoja kwa makoo wengi nk.

2------Kulinda heshima na hadhi ya jamii; ni hivi heshima ya jamii ni pamoja na maisha ya staha ya watu wake, sio staha wanawake wawe wengi mitaani wakirandaranda bila kuolewa, hatari yake ndiyo vyangudoa na ukahaba na madanguro kuongezeka na watoto wasiokuwa na baba kuongezeka na hao watoto wakikosa malezi wanakuwa vibaka na wavuta unga nk, katika ukahaba ndimo magonjwa ya zinaa yatapatikana na kumbuka wateja wa hao makahaba ndio hao waume zenu mnaowatisha wasioe mke mwingine zaidi yako, unakataa mke mwenza unapokea Ukimwi na Hepatitis nk.

3----- Kumbuka wanawake wanaoranda mitaani kwa kukosa kuolewa hao ni ama mdogo wako, mtoto wa ndugu yako, mama yako mdogo, shangazi yako na hata anaweza kuwa ni mwanao, je unaweza kuwa ni mtu mwenye furaha kuona mwanao au nduguyo yeyote anaranda mitaani kutafuta wanaume wa kukidhi haja zake za kimwili kwakuwa tu hakuolewa???

4----Wanaobomoa ndoa za mke/mme mmoja ni nyumba ndogo, ushahidi uliopo ni kwamba ndoa za mke/mume mmoja zimekuwa zikibomoka kutokana na nyumba ndogo, mume ananogewa na nyumba ndogo mwishowe anatelekeza nyumba kubwa, yote hii isingekuwepo kama nyumba ndogo "zingehalalishwa" kupitia mitaala.

5-----Maradhi kwa Mke, inaweza kutokea mtu kaoa mke baada ya muda fulani mke akashikwa na maradhi ya kudumu kama ya kigenetic nk, na akashindwa kabisa kumuhudumia mumewe hapo mitaala inaswihi ili huyo mke mwenza aje kuwahudumia wote mume na mwenzake aliyekuwa mgonjwa, haitakuwa ubinadamu kumpa talaka huyo mgonjwa na kuoa mke mwingine.

6----- Kukuza uzao, mara nyingi inatokea watu wanaoa wanawake tasa na inapogundulika hivyo basi mitala inaswihi ili kuendeleza uzao, mke tasa sio ubinadamu kumpa talaka.

7-----Kukuza uzao wenye vipaji vingi, mbali na malezi kuna vipawa watu huwanavyo kutokana na vinasaba hivyo mitala ni njia mmoja ya kukuza uzao wenye vipaji kadhaa.

8--- Kukidhi haja za mume, lazima tukubaliane kwamba kuna wanaume wengine wana nguvu kubwa sana katika tendo wameumbwa hivyo na Mungu, watu wa aina hiyo wanapoweza kutimiza like sharti ya mitala basi ni ruksa kuongeza mke ili kumpunguzia "mzigo" mke mmoja na ili asiwe na nyumba ndogo.

NB: Wanawake wenye khofu na Mungu na wanaojua faida ya mitala hao ndio wanaoweza kuolewa na amani ikapatikana ndani ya nyumba na sio wale wanawake wenye tamaa ya matumbo yao na tamaa za watoto wao, wanawake wa aina hiyo ya tamaa katika nyumba ni kama jehanamu ndogo, hawafai katika mitala.

Mokaze umetoa maelezo mazuri sana lakini ukweli ni kwamba siku hizi wenye sababu za msingi na uwezo wa kumudu kuoa mke zaidi ya mmoja yaani mitala hata hawafanyi hivyo

Ila wale wasiokua na uwezo hata wa kukamilisha mahitaji muhimu kwa familia zao na watoto zao ndio wenye tamaa ya kuongeza wanawake.

Na hapa ndio sisi wanawake tunapochachamaaa na famila kupoteza muelekeo
 

Vishu Mtata

JF-Expert Member
Dec 15, 2019
2,205
2,000
Ila kwa sasa kua na wake wengi ni tamaa tu za wanaume, japo baadhi wanasingizia dini inaruhusu na nn lakin main point ni kucontrol tamaa.

Na wanawake wa sasa wana wivu mkali tofauti na zamani, anakua na malengo yake makubwa tu, anakua anatamni awe sehemu fulani kimaisha sasa kumuongezea mke mwenza ni kama unazizima ndoto zake na wewe.
 

Mokaze

JF-Expert Member
Aug 3, 2018
10,756
2,000
Mokaze umetoa maelezo mazuri sana lakini ukweli ni kwamba siku hizi wenye sababu za msingi na uwezo wa kumudu kuoa mke zaidi ya mmoja yaani mitala hata hawafanyi hivyo

Ila wale wasiokua na uwezo hata wa kukamilisha mahitaji muhimu kwa familia zao na watoto zao ndio wenye tamaa ya kuongeza wanawake.

Na hapa ndio sisi wanawake tunapochachamaaa na famila kupoteza muelekeo


Hicho usemacho ni kweli kabisa MamaD, na watu wa aina hiyo ndio wanaoharibu maana na nia njema ya mitala.
 

Nyalotsi

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
6,524
2,000
Ila kwa sasa kua na wake wengi ni tamaa tu za wanaume, japo baadhi wanasingizia dini inaruhusu na nn lakin main point ni kucontrol tamaa.

Na wanawake wa sasa wana wivu mkali tofauti na zamani, anakua na malengo yake makubwa tu, anakua anatamni awe sehemu fulani kimaisha sasa kumuongezea mke mwenza ni kama unazizima ndoto zake na wewe.
Mwanaume mwenye mke zaidi ya mmoja anaongeza zaidi utafutaji kuliko mwenye mke mmoja.
Mind you, anayetakiwa kuoa mke zaidi ya mmoja ni mwenye uwezo. Hivyo ataongeza uwezo zaidi.
Mke kuwa mmoja haimfanyi kupata vingi kwa kuwa yuko peke yake. Mwanaume atatafuta kulingana na familia iliyopo.
Ubinafsi wa wanawake huwa unawafanya wawaze kuwa ninachopeleka kule kingekuwa Cha kwake.
Kumbe hata nisingekitafuta. Angeendelea kupata anachopata Sasa hivi
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
15,354
2,000
kwako dr.mwaka tupe uzoefu
Kwanza nitake radhi kwa kunipa jina lisilokua langu. Mimi sio dr. mwaka

Turudi kwenye maada
Uzoefu ni kwamba ukiwa vizuri kabisa kiuchumi ukamtosheleza mkeo kwa kila anachotakiwa kupata wivu unaweza kuwepo mwanzoni ila atakuelewa na kuendelea kukuheshimu nawe utampenda zaidi

Sio maisha ya kuungaunga halafu unatamani kuongeza wanawake, utajuta na utakufa siku sio zako
☺☺☺☺☺
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom