mwanawao
JF-Expert Member
- Aug 18, 2010
- 3,142
- 5,634
Nimesikiliza taarifa ya habari kutoka T.B.C leo kuna research imefanyika Tanzania ikihusisha MIFUKO YA JAMII na matokeo yanaonyesha kuwa kuna baadhi ya mashirika yatafilisika ifikapo mwaka 2015 kutokana na uwekezaji wa kiholela ambao haukufanyiwa tathmini ya kutosha. Utafiti huo umeonyesha kuwa kuna mashirika matatu yapo kwenye risk kubwa zaidi ya kufilisika.
Maswali yangu ni haya:
1. Kuna sheria yoyote inayomlinda mwanachama kwamba shirika likifilisika aweze kulipwa hela yake kwa njia mbadala? Mfano mashirika mengi yanajenga nyumba za makazi ya kuishi, inawezekana hali kama hiyo ikitokea sheria ikakulinda ulipwe angalau apartment badala ya hela?
2.Wanachama wenye hela zao kwenye haya mashirika itakuwaje? Kweli mtu atafanya kazi afikishe miaka 60 umwambie hela yake ya mafao haipo?