Hii imekaaje WADAU: Baadhi ya MIFUKO YA JAMII KUFILISIKA ifikapo 2015

mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
2,861
4,924
Nimesikiliza taarifa ya habari kutoka T.B.C leo kuna research imefanyika Tanzania ikihusisha MIFUKO YA JAMII na matokeo yanaonyesha kuwa kuna baadhi ya mashirika yatafilisika ifikapo mwaka 2015 kutokana na uwekezaji wa kiholela ambao haukufanyiwa tathmini ya kutosha. Utafiti huo umeonyesha kuwa kuna mashirika matatu yapo kwenye risk kubwa zaidi ya kufilisika.

Maswali yangu ni haya:
1. Kuna sheria yoyote inayomlinda mwanachama kwamba shirika likifilisika aweze kulipwa hela yake kwa njia mbadala? Mfano mashirika mengi yanajenga nyumba za makazi ya kuishi, inawezekana hali kama hiyo ikitokea sheria ikakulinda ulipwe angalau apartment badala ya hela?
2.Wanachama wenye hela zao kwenye haya mashirika itakuwaje? Kweli mtu atafanya kazi afikishe miaka 60 umwambie hela yake ya mafao haipo?
 
King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
44,447
51,162
Mkuu ebu achana na hyo mifuko ukianza kuwastua kwamba wanafilisika watazuia hela zetu tena ebu acha kuongelea hayo makitu yalituumiza kichwa mwezi wa 8 mpaka Nov.
 
mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
2,861
4,924
Mkuu ebu achana na hyo mifuko ukianza kuwastua kwamba wanafilisika watazuia hela zetu tena ebu acha kuongelea hayo makitu yalituumiza kichwa mwezi wa 8 mpaka Nov.

MKUU, ni utafiti umefanyika na kama umeshatolewa mpaka kwenye vyombo vya habari hamna cha kuficha hapo taarifa ni kwamba tayari wanazo. Je wanachama wao wanalijua hilo?
 
LUS0MYA

JF-Expert Member
Aug 4, 2011
640
718
  • Nathubutu kukubaliana na report hiyo kwani sasa mambo ni dhahiri kabisa taasisi hizi zitakufa.nimeingia kidogo kwa undani kuangalia moja ya taasisi kubwa ya hifadhi ya jamii(NSSF) inavyofanya kazi basi unaweza kusema mambo hayaendi yanavyohitajika.Hebu angalia; NSSF walitoa kadi mpya za kietroniki kwa wanachama wake ili waweze kutumia katiak kuangalia michango nk hadi leo hii kadi yangu imechakaa sijawahi kuitumia hata mara moja.nyuma ya pazia wakuu waje watueleze shirika lilitumia kiasi gani kutayarisha na kusambaza hizi kadi?
  • Michango ya wanachama kutokuwa allocated kwa wahusika.ukijaribu kupata statement ya NSSF unaweza kuchanganyikiwa!aghalabu ni mara chache sana akaunti ya mwanachama inakuwa uptodate.Waajiri wanalipa michango yao kwa muda muafaka lakini ukiangalia akaunti yako utashangaa kuona wakati mwingine michango inayoonekana haifikii hata nusu ya kiwango kinachotakiwa kuonekana.Swali hapa ni kuwa hayo mabilioni ambayo hayajawa posted kwenye akaunti ya mwanachama yako wapi?nani anayatunza?
  • Wafanyakazi wake bado hawajakwewnda na hali ya sasa ya utendaji kazi.huduma zao n i mbovu na hata uwezo wa kusimamia uwekezaji unaoendelea hawana.NSSF ni moja ya taasisi ambayo hadi katika dunia ya leo.wanafunga ofisi mchana kwenda kula!Baada ya saa 7 mchana hawahudumii tena wanachama....this is bunch of foolery!
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
98,352
170,234

Mimi siiamini TBC , ila kutokana na uchunguzi wako basi nakuamini wewe , hadi nahisi wewe ni bora kuliko TBC, maana umesema hadi yale ya chumbani , kufunga ofisi kubwa namna hiyo kisa chipsi kuku !
 
mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
2,861
4,924
Mimi siiamini TBC , ila kutokana na uchunguzi wako basi nakuamini wewe , hadi nahisi wewe ni bora kuliko TBC, maana umesema hadi yale ya chumbani , kufunga ofisi kubwa namna hiyo kisa chipsi kuku !

MKUU, unaweza usiiamini TBC kama wangekuwa wao ndo wamefanya huo utafiti lakini utafiti umefanywa na watu wengine, wao wamefanya tu kutangaza baada ya kuipata.
 
CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,364
6,404
Nimesikiliza taarifa ya habari kutoka T.B.C leo kuna research imefanyika Tanzania ikihusisha MIFUKO YA JAMII na matokeo yanaonyesha kuwa kuna baadhi ya mashirika yatafilisika ifikapo mwaka 2015 kutokana na uwekezaji wa kiholela ambao haukufanyiwa tathmini ya kutosha. Utafiti huo umeonyesha kuwa kuna mashirika matatu yapo kwenye risk kubwa zaidi ya kufilisika.

Maswali yangu ni haya:
1. Kuna sheria yoyote inayomlinda mwanachama kwamba shirika likifilisika aweze kulipwa hela yake kwa njia mbadala? Mfano mashirika mengi yanajenga nyumba za makazi ya kuishi, inawezekana hali kama hiyo ikitokea sheria ikakulinda ulipwe angalau apartment badala ya hela?
2.Wanachama wenye hela zao kwenye haya mashirika itakuwaje? Kweli mtu atafanya kazi afikishe miaka 60 umwambie hela yake ya mafao haipo?

Walaaniwe wote, watembee na shetani maishani mwao kama watafilisis hela zetu
 
mwanawao

JF-Expert Member
Aug 18, 2010
2,861
4,924
NSSF haikosi humu.....lazima ni mojawapo ya mifuko inayoelekea kuzimu

NSSF lazima wawepo maana ndo wenye miradi mikubwa sana inayoendelea kufanyika kwa sasa, wanajenga hotels na apartments sehemu nyingi tu sahivi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom