Hii Imekaaje? Mwenye Kujua anisaidie.......

mujemaso

Senior Member
Apr 26, 2012
112
225
Habari za leo wanajamvi,

Kuna kitu kinanifanya nitafakari sana nikiangalia mataifa haya tunayoyaita yameendelea na yale yanayoendelea. Ukifuatilia vizuri utakuta mataifa haya kama si yote basi baadhi yana sifa zifuatazo:

1. Lugha ya kwao wenyewe ya asili (na ndo inatumika kufundishia)
2. Maandishi ya kwao wenyewe
3. Dini za kwao wenyewe (japo na za kigeni zipo)
4. Utamaduni wao wanaulinda sana
.
.
.
Mengine mnaweza kuongeza.

Nchi kama Korea, Malaysia, Indonesia, India, China, Japan, nchi za Kiarabu, Urusi n.k zote hizi zina sifa nilizotaja hapo juu na ni nchi ambazo zinakuja juu kiuchumi. Nabaki kujiuliza dini, lugha, maandishi vina uhusiano gani na maendeleo kiuchumi ? Nikiangalia kwa upande mwingine nchi zetu kina sie ambazo hazina sifa za hapo juu ziko hohehahe kiuchumi.

Japo nchi kama Afrika Kusini imepiga hatua lakini unakuta kuna Ngozi nyeupe iko pale ! Hii Imekaaje ?
 

BUGE

Senior Member
Sep 22, 2013
163
195
Nionavyo mimi pamoja na kulinda tamaduni zao kubwa zaidi ni weledi ktk kazi, kujituma na uwadilifu wa vingozi wao ktk kusimamia vyema mali za taifa pia uwelewa wa wananchi wao upo juu ktk swala zima la kujua haki na wajibu wao mmoja mmoja au kama taifa kwa ujumla
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom