Hii imekaaje kwa mpenzi anayekupa kiasi fulani cha pesa halafu ndani ya siku mbili anaomba 75% ya pesa aliyokupa

Uchoyo huo, hata haukupendezei!
Hahhaha.mkuu nyie mmezid uchoyo..yan unakuta nakupa hela leo..kesho tunaeza kuwa ndan nakuomba buku mbili uniwekee bando unagoma unasema nakuwekea ila utanilipa
 
Kwa ufupi kuna huyu mpenzi wangu, yaani juzi aliniwezesha kiasi kidogo cha pesa kama 2.5M hata hazijapita siku mbili, jana kanipigia simu anataka nimuazimie kama 1.5M kuna dharula amepata nyumbani kwao, moyo umekuwa mgumu kumuamini nahisi ni ubahili unamsumbua huyu mwenzagu hivyo nimekuja kwenu nimsaidie ama na mimi nikae kimya tu kama sijaona huo ujumbe wake.

Kwa ufupi tu hiyo pesa kwa sasa sina maana nilituma nyumbani kuna ujenzi unaendelea kule.

Nahitaji ushauri wako wa kujenga na si kubomoa.
Ushauri ni mgumu bila kujua mko muda gani kwenye mahusiano. Kama muda ni mrefu je hiyo ni mara ya kwanza? Kama huwa anafanyaga hivyo huna haja ya kuwa na wasiwasi. Kama ni muda mfupi unayo sababu ya kushutuka maana huenda alikupa pesa ila baade akili yake ikamtuma alikosea kukupatia. Kwahiyo ni kama njia ya kupunguza maumivu na huyo hamutaweza kudumu kwenye mahusiano.
 
Hahhaha.mkuu nyie mmezid uchoyo..yan unakuta nakupa hela leo..kesho tunaeza kuwa ndan nakuomba buku mbili uniwekee bando unagoma unasema nakuwekea ila utanilipa
Sasa si nakuwa nishaitumia jamani, nakupa nini tena
 
Na hiz ndo true colors za jinsia hii pendwa..tutafanyaje sasa...

Jana tu hapo nmetoka kumuahidi x wangu wa kitambo sana kuwa aje achukue television akaweke kwenye liquor store yake mpya kakubal ila hatak kuja kuichkulia nyumban...wakat yeye ndo kalia shida...kupokea mnataka kutoa hamtak.hahhah
 
Wanaume wana mitego, na mitego yao kwetu ni kwa kutumia pesa,ungempa aliyoomba ungejiongezea nafasi kubwa ya kula mara mia ya hiyo 2.5,, nakumbuka x-mas ya mwaka jana alinitumia 50k kwa ajili ya sikukuu hapo hapo bintize walitumia karibia 1m kwa ajili ya sikukuu,mama yake 300k na hizo zote akanijulisha, sikubadilika wala kujaa kinyongo nilikuwa normal tu nikamshukuru km kipofu aliyeona mwezi, guess what nimeambiwa nichague nchi nzuri kwa utalii ndani ya Afrika kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu mwaka huu
Wacha wee, unajua kutumia fursa.
 
Kwa ufupi kuna huyu mpenzi wangu, yaani juzi aliniwezesha kiasi kidogo cha pesa kama 2.5M hata hazijapita siku mbili, jana kanipigia simu anataka nimuazimie kama 1.5M kuna dharula amepata nyumbani kwao, moyo umekuwa mgumu kumuamini nahisi ni ubahili unamsumbua huyu mwenzagu hivyo nimekuja kwenu nimsaidie ama na mimi nikae kimya tu kama sijaona huo ujumbe wake.

Kwa ufupi tu hiyo pesa kwa sasa sina maana nilituma nyumbani kuna ujenzi unaendelea kule.

Nahitaji ushauri wako wa kujenga na si kubomoa.

Sijajua wengine wamekushauri vipi ila hata kama huna tafuta mpe, hata ingekua mimi ningempa ila roho ingeniuma niwe mkweli maana nisingeweza kuja kumdai!!

Inawezekana anakupima au kabanwa kweli....
 
Kwa ufupi kuna huyu mpenzi wangu, yaani juzi aliniwezesha kiasi kidogo cha pesa kama 2.5M hata hazijapita siku mbili, jana kanipigia simu anataka nimuazimie kama 1.5M kuna dharula amepata nyumbani kwao, moyo umekuwa mgumu kumuamini nahisi ni ubahili unamsumbua huyu mwenzagu hivyo nimekuja kwenu nimsaidie ama na mimi nikae kimya tu kama sijaona huo ujumbe wake.

Kwa ufupi tu hiyo pesa kwa sasa sina maana nilituma nyumbani kuna ujenzi unaendelea kule.

Nahitaji ushauri wako wa kujenga na si kubomoa.
Hapo anakupima kama wewe ni wife material au ni bwege tu, na hamuwez fanya kitu chochote katika maisha wewe leo kakupa kesho huna mwanamke gani sasa et unasema ubahiri. Mwanaume anapenda mwanamke mwenye nidham ya pesa na anaejitambua utaachwa f@la ww.
 
Wacha wee, unajua kutumia fursa.
😂😂😂Ni kutumia ubongo kwa usahihi,, lengo la kunijulisha yote hayo ilikuwa ni nini, ilhali anafanyaga miamala yake mingine pasipo mimi kujua nikajiongeza tu ulikuwa mtego,, mitego ni mingi mno na hata leo naweza kutegwa😂😂😂😂
 
Kwa ufupi kuna huyu mpenzi wangu, yaani juzi aliniwezesha kiasi kidogo cha pesa kama 2.5M hata hazijapita siku mbili, jana kanipigia simu anataka nimuazimie kama 1.5M kuna dharula amepata nyumbani kwao, moyo umekuwa mgumu kumuamini nahisi ni ubahili unamsumbua huyu mwenzagu hivyo nimekuja kwenu nimsaidie ama na mimi nikae kimya tu kama sijaona huo ujumbe wake.

Kwa ufupi tu hiyo pesa kwa sasa sina maana nilituma nyumbani kuna ujenzi unaendelea kule.

Nahitaji ushauri wako wa kujenga na si kubomoa.
inaitwa both teams to score hiyo..
 
Mwakuliwa in the context! Pesa kidogo 2.5M tone ya sms yako na attitude haifanani na majidai yaliyo kwenye maudhui.

Mwakuliwa anataka project ndefu ila wewe ni Mwakulakula tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom