Hii imekaaje et!!!!!

ex's walozaa wanafungamana kama zito alivyofungamana na chadema.

Huwezi athiri kimoja bila kuathiri kingine.
 
sio wote, wengine walizalishana wakatelekezana, usitegemee wawe na mahusiano mazuri.

Waloachana kwa nginjanginja huwa hawako karibu.

Tatizo linakuja kama ex alobaki yuko singo, kama naye kaoa ama kuolewa hawawi karibu sana.

Ila lazima wahusiane sababu ya mtoto

kwisha habari angu.....!
 
mimi nijuavyo mara nyingi wanaozaa huwa hawaachani kama yule mwanamke hakuolewa baada ya kuachwa na huyo mwanaume, kwa sababu yule mwanaume atakuwa anakwenda pale kumuona mtoto, mara utasikia kazaa naye mtoto wa pili. Ila kwa wengine ili kuvunja kabisa hiyo hali wanachukuwa watoto na kukaa nao , hiyo inamfanya yule mwanaume asiwe na kisingizio cha kwenda kwa yule mzazi mwenzie.

Pia muwekane sawa jinsi atakavyokuwa anakuja kumtembelea mtoto ama aje home kwako au apelekewe amsalimu au aende shule .

Fanya hayo utakata mzizi wa fitina. Lakini ukiona mwanaume anakataa hayo , fikiria halafu chukua hatua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom