Hii Imekaaje Bandugu? ;WANACHAMA SIMBA KUTINGA BUNGENI JUMANNE.

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,141
13,215
[h=3][/h]

WANACHAMA wa klabu ya Simba wanaompinga Mwenyekiti wa klabu hiyo, Ismail Aden Rage wataelekea mjini Dodoma Jumanne kwa ajili ya kuonana na Spika wa Bunge hilo, Anna Makinda kuelezea namna Mwenyekiti huyo anavyovunja Katiba ya klabu hiyo.
Awali wanachama hao walipanga kuondoka leo kwenda Dodoma ili kesho Jumatatu waonane na spika lakini wamehairisha kutokana na kesho kuangukia siku ya Uhuru ambapo watu awaendi makazini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam kwa niaba ya wanachama wenzake, Katibu wa tawi la mzambalauni, Daniel Kamna mwenye kadi ya uwanachama wa klabu hiyo namba 100, alisema kuwa lengo lao wanataka kufikisha matatizo ya Rage kwenye klabu hiyo kwa wabunge hili wamshauri kuachia madaraka klabuni hapo.
"juzi tulimpa siku mbili awe amejiuzulu..., lakini ameonekana kuwa mkaidi na kiburi, sasa sisi msimamo wetu uko pale pale tumeshajipanga na tumewasiliana na wabunge wanachama wa klabu yetuambao wametualika bungeni na tutaondoka hapa Jumanne ili siku inayofuata asubuhi tuingine bungeni," alisema Kamna.
Alisema kuwa mwenyekiti wao huyo ameonyesha jeuri na kutowasikiliza wanachama waliomuweka madarakani na badala yake amekuwa na maamuzi ya peke yake yasiyokuwa na faida kwa klabu hiyo.
Kamna alisema moja ya jambo ambalo limewashangaza ni kitendo cha Mwenyekiti huyo alipokutana na mmiliki wa klabu ya Sunderland ya Uingereza mapema mwaka huu ambapo badala ya kuomba msaada kwa ajili ya klabu (Rage) aliomba msaada kwa jili ya jimbo lake la Tabora mjini.
"Sasa mtu kama huyo klabuni kwetu wa nini, ameonyesha kuweka masrai yake binafsi mbele badala ya Simba kwanza," aliongezea kusema Kamna.
Alisema kuwa Simba inawanachama na mashabiki wabunge ambao aliwataja baadhi yao kuwa ni Makongoro Mahanga, Zitto Kabwe, Iddi Azan na Mussa Azan Zungu ambao watafanikisha wao wanachama kuingia bungeni siku hiyo ya Jumatano.
"Unajua uwezi kuingia bungeni bila kuwa na mwaliko maalum kutoka kwa aidha mbunge au kiongozi mwingine pale bungeni, tayari tumepata mwaliko na tunajiandaa na safari," aliongezea kusema Kamna.
Alisema kuwa hawana ugomvi na Rage ila wanapingana naye baada ya kuonyesha vitenda vya wazi vya kuvunja katiba ya klabu hiyo hivyo wanataka ajiuzulu na kuwaachia Simba yao.
Hata hivyo alipotafutwa Rage kwa njia ya simu kuzungumzia kauri hiyo ya wanachama, simu yake ya mkononi haikuwa ikipatikana.
Klabu ya Simba ipo kwenye mvutano mkubwa wa kiuongozi katika kipindi hiki ambacho timu nyingi zipo kwenye maandalizi kwa ajili mzunguko wa pili wa ligi kuu.
Wanachama na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji wa klabu hiyo wanamtaka Mwenyekiti wao Rage ajiuzulu kwa madai ya kushindwa kufuata katiba ya klabu hiyo.
 
pamoja na kwamba mimi ni Mwanachama wa Simba lakn hii sijaielewa kabisa
 
nawashauri wafuate Katiba ya Simba tu, si kwenda kumaliza nauli na posho zao Dodoma
 
[h=3]HATUMTAKI RAGE AJIONDOE MWENYEWE IFIKAPO JUMAMOSI DEC 7 [/h]
[h=3][/h]

blogger-image--1577598344.jpg

Wanachama wa Simba wamemtaka Mwenyekiti wa Simba, Aden Rage kujiudhuru ifikapo jumamosi baada ya hapo wao wanakwenda mjini Dodoma ili kumshinikiza ajihudhuru
 
usipopendeza arusini huwezi kupendeza msibani
 
blogger-image-395004746.jpg

Wakizungumza katika ukumbi wa idara ya Habari Maelezo mchana wa leo, Alhamis Desemba 5, 2013 walisema wamechoka na vituko vya mwenyekiti wao maana kila wakimtaka aitishe mkutano mkuu amekuwa akikiuka
 
pamoja na kwamba naungana nao kumpinga rage njia wanayotumia si sahihi watumie njia sahihi kumuondoa kama kuitisha mkutano ikishindika kuhamasisha washabiki wote wa simba wasihudhurie mechi mpaka rage ameondoka
 
pamoja na kwamba naungana nao kumpinga rage njia wanayotumia si sahihi watumie njia sahihi kumuondoa kama kuitisha mkutano ikishindika kuhamasisha washabiki wote wa simba wasihudhurie mechi mpaka rage ameondoka

huenda kuna mtu kawalipia per diem
 
ninyi ndio wanachama, timu ni yakwenu, kwanini musifunge mlango wa chumba cha mwenyekiti na kumtangazia asikanyage kwenye jengo lenu? timu ya kwenu alafu muka
mtwike mzigo spika!!! acheni ubwenyenye chukueni hatua wavulana nyinyi.

na wasicjana tumo umetusahau
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom