Hii imekaaje Balozi wa China kufanya mazungumzo ya kitaifa kwenye ofisi za chama cha siasa!?

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
20,385
24,939
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akizungumza na Balozi wa China hapa nchini Dk. Lu Young, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba Dar es Salaam.

My take : Hii imekaaje wanajamvi!? balozi anayewakilisha maslahi ya china kwa Tanzania kwenda kufanya mazungumzo ya kitaifa kwenye ofisi za chama cha siasa??

full_size_20170118191640.jpeg



Chanzo : ITV
 
The problem huyu jamaa kule kwao bado kuna mambo ya chama kushika hatamu sasa anadhani kila mahali ni chama kushika hatamu! Kule kwao, ni kawaida kuona kiongozi wa nje aliyefanya ziara ya kiserikali anaenda pia kukutana hadi na viongozi wa chama!!!

Sasa hawa akina Kinana wana-take advantage ya uzumbukuku wa jamaa asiyejua kutofautisha kati ya serikali na chama!!!
 
Mbona ni kawaida yao kuwakaribisha hata kwenye mikutano yao ya kisiasa mbele za wananchi. Kuna balozi wa nchi fulani nchini (wenye kumbukumbu sahihi watatujuza) alishiriki kwenye mkutano wa CCM mwaka jana
 
Kabla ya uchaguzi,Kinana,Kikwete na hata Mwigulu walienda China kwa interval mbali mbali,hao ndio Baba walezi wa CCMmadarakani!!
 
Unawezaje kuchora mstari kati ya Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China na Communist Party of China (CPC)?
 
kwa huo ukaribu sio wa kawaida na inawezekana ccm wakawa wameshikwa masikio na wachina. chochote watakacho ambiwa na wachina kwao ni sawa.
hata bila kujiuliza.
 
Back
Top Bottom