Hii huduma ya pesa inayotolewa na makampuni ya cm ni wizi mtupu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii huduma ya pesa inayotolewa na makampuni ya cm ni wizi mtupu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiumbe duni, Feb 16, 2012.

 1. K

  Kiumbe duni Senior Member

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huduma hii baada ya kupapatikiwa na watu wengi imeshaanza kuwa kero. Kama ukitaka kutuma pesa mkoa mwingine tofauti na unaoishi wakala atakuambia hairuhusiwi mpaka akurushie wewe na wewe ndio umrushie huyo wa mkoani. Huu ni wizi kwa sababu wakala akikurushia wewe halafu wewe ukamrushia wa mkoani ni lazima ukatwe hela, na wamkoani akienda kwa wakala kutoa pesa ni lazima akatwe. Kwa hiyo wanakula mara mbili kwako na kwa wa mkoani, tofauti kama wakala angeruhusiwa kurusha moja kwa moja mkoani angekatwa mtu mmoja tu. Wadai wakirusha moja kwa moja hela inaweza kupotelea njiani utetezi ambao hauna mashiko.
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wepi hao Tigo au Voda?
   
 3. c

  chooser New Member

  #3
  Feb 16, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  @kiumbe duni hizo ni taratibu zilizokekwa na voddacom wenyewe na sio wakala
   
 4. K

  Kiumbe duni Senior Member

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wote wanahusika
   
 5. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Huu ni utaratibu uliowekwa na makampuni yenyewe ili kuhakiki yenyewe ndio yanayonufaika zaidi kuliko wakala. kumbuka unaporusha wewe kwenda kwa mjomba ako wakala hausiki na makato yanaenda 1kwa1 kwenye kampuni
   
 6. K

  Kiumbe duni Senior Member

  #6
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakala ahusiki, ila kinacholalamikiwa ni kwa nini hizi kampuni haziruhusu kutuma pesa moja kwa moja mikoani kupitia kwa wakala mpaka wakala amrushie mteja na mteja amrushie anayetaka kumtumia?
   
 7. E

  ENGINE CONTROL Senior Member

  #7
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 20, 2011
  Messages: 139
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kweli sababu haina mashiko kwani ukilusha wew huko mkoani haiwezi kupotea???.

  Ok!! Kwani wakala akirusha yeye moja kwa moja mkoani au akikurushia wewe na wew ndiyo umrushie wa mkoani ni njia ipi ni sahihi na salama zaidi.

  Hawaoni kama zikipita mikonon mwao (mawakala) ndiyo zitakuwa salama zaidi??.

  Kwani wao kazi yao ni nini hasa??
   
 8. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  wanachojali ni transaction interest na sio usalama
   
 9. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,655
  Trophy Points: 280

  Wakuu, huo utaratibu ni muhimu na salama sana kwa mteja kutokana na ukweli kwamba mara kwa mara kunakuwa na matatizo ya network, iwe Tigo Pesa au M-Pesa!! Assume unafika kwa wakala halafu unampatia pesa kisha anatuma yeye moja kwa moja. Halafu hapo hapo unakuta network inasumbua....hapo kuna uwezekano mkubwa huyo unayemtumia wakati huo akashindwa kupata hiyo pesa...!!! Sasa hapo utalazimika kuondoka huku ukiwa hufahamu endapo pesa still ipo kwenye akaunti ya wakala au kwa uliyemtumia. Na vyovyote iwavyo, huwezi kupiga kambi kwa wakala hadi upate uhakike kwamba pesa yako imefika....ni lazima uondoke huku ukiwa kwenye dilema! Itafika siku ya pili, pesa haijafika...na hapo itabidi kufuatilia kwenye kampuni ya simu....hakuna wakala atakayekubali kuacha duka lake aende kwenye kampuni ya simu hasa kwavile kwake itaonekana imeshatoka...!!! Mbaya zaidi, ni pale unayemtumia kama hajajisajili......kwa utaratibu wa tigo kama umetuma after one week, itabidi irudi kwa mtumaji. So, tell me....utakuwa tayari pesa yako irudi kwa wakala halafu uanze tena kumfuatilia?!

  That is one. Wakati mwingine, unakuta unatuma lakini kutokana na matatizo ya network, pesa inashindwa kuhama toka kwenye akaunti ya mtumaji. So, kama amekutumia wewe mwenyewe, unaweza kusepa zako na kujaribu mara kwa mara hadi pale network itakapokua poa na kutuma. So, assume pesa ipo kwenye akaunti ya wakala....je, utapiga kambi kwa wakala na kumwambia awe anajaribu mara kwa mara bila kujua network itakua poa mida gani?!

  Ushauri wa bure ni kwamba, hata kama wakala ata-opt kukutumia moja kwa moja....KATAAA na mwambie akutumie wewe kisha mwenyewe utaituma kwa mwenyewe. Gharama za wakala kukutumia wewe ni ndogo sana kuliko usumbufu utakaopata kutoakana na kumwabia atume moja kwa moja!!!! Hapa kama kuna cha kulalamikia ni poor network lakini sio hatua ya wakala kukuingizia wewe kwanza...hiyo ni safe zaidi kwako kuliko vinginevo!
   
 10. m

  mariavictima Senior Member

  #10
  Feb 17, 2012
  Joined: Jul 8, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mbona ni rahisi sana. Wewe weka pesa kwenye account yako, kisha mtumie mtu unayetaka kumtumia. Kuweka pesa kwenye account yako ni bure. Kutuma pesa unakotaka utakatwa shilingi 200 tu kama umesajiliwa. Yule unayemtumia atakatwa wakati wa kupokea kufuatana na kiwango atakachochukua.
  mfano (kama amesajiliwa) atakatwa kama ifuatavyo:
  1,000 mpaka 9,999 atakatwa shs 500/=
  10,000 mpaka 49,999 atakatwa shs 1,000/=
  50,000 mpaka 99,999 atakatwa shs 1,500/=
  100,000 mpaka 199,999 atakatwa shs 2,000/=
  200,000 mpaka 299,999 atakatwa shs 3,000/=
  300,000 mpaka 399,999 atakatwa shs 4,000/=
  400,000 mpaka 1,00,000 atakatwa shs 5,000/=
  Kama unayemtumia hajasajiliwa, atapokea pesa ulizomtumia bure.

  Kama wewe hujasajiliwa utatuma pesa kwa gharama zifuatazo:
  1,000 mpaka 9,999 atakatwa shs 700/=
  10,000 mpaka 49,999 atakatwa shs 1,200/=
  50,000 mpaka 99,999 atakatwa shs 1,700/=
  100,000 mpaka 199,999 atakatwa shs 2,200/=
  200,000 mpaka 299,999 atakatwa shs 3,200/=
  300,000 mpaka 399,999 atakatwa shs 4,200/=
  400,000 mpaka 1,00,000 atakatwa shs 5,200/=
  Kama unayemtumia hajasajiliwa, atapokea pesa ulizomtumia bure.

  Hii ni kwa wateja wa vodacom.
  Lakini pia kwa makampuni mengine (Tigo) hayatofautiani sana. Gharama ni kama hizo hizo. Ili usiibiwe na wakala omba kipeperushi cha bei kwenye ofisi/maduka ya hizo kampuni za simu. Pia ukihisi umeibiwa na wakala piga simu kwa kampuni husika na taja namba ya wakala, watamfungia mara moja. Ni muhimu unapotuma au kupokea pesa kuchukua namba ya wakala. Nadhani nimesaidia kwa kiasi fulani japo mimi si mfanyakazi wa hayo makampuni. Niliwahi kupata shida kama yako na nilipokwenda kwao walinielekeza hivi.
   
 11. Wa Kwilondo

  Wa Kwilondo JF-Expert Member

  #11
  Feb 18, 2012
  Joined: Sep 15, 2007
  Messages: 1,083
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  Tunashukuru Wakala!! please assist me on this;wakala anapata faida yoyote akikuhamishia fedha kwenye simu? i mean kuweka hela kwa simu
   
Loading...