Hii hapa Siri ya ulinzi mkali wa Rais Magufuli

thetallest

JF-Expert Member
Oct 21, 2017
8,256
9,085
Huwa nafuatilia komenti za wanajukwaa mbalimbali kuhusu ulinzi wa Rais Magufuli,wengi hushangaa kwanini Rais Magufuli ana ulinzi mkali kiasi hicho,na wengi hujaribu kuulinganisha na wa awamu ya kwanza ya JK Nyerere,

kwamba mwalimu Nyerere alitembelea 109 landrover,hakua na msafara ,alikua sehemu zingine anakwenda na gari tatu tu,au moja.

Ni 34yrs sasa imepita,

kulinganisha hicho kipindi na cha sasa ni kituko kabisa!,teknolojia ime advance sana.

Enzi za mwalimu Tv aliangalia peke yake hapo Ikulu, mpaka ilipokuja zile sinema za magari ,za kina Yombayomba,na zilihimiza kilimo tu,watu walilima mashamba ya mfumaki,watanzania kwa ujumla walikua watiifu sana ,hakukua na ujambazi,wizi uliokithiri,ilikua rahisi kuwabaini wahalifu ,teknolojia ilikua duni sana.computers hazikuwepo,radio ilikua moja tu" RTD",mgambo mmoja na rungu aliweza kufanya kazi kijiji kizima ,na aliwatuliza .

Nakumbuka kuna Dada mmoja aliwahi kuvaa suruali mchana ,alizomewa mtaa mzima huku akisindikizwa na mawe, aliokolewa baada ya kuingia nyumba moja ,alikaa humo hadi usiku,akapewa khanga na kwenda kwao,hali hiyo ndio ilikua enzi za Mwalimu Nyerere,

Ni mengi ya kuelezea zama hizo za ujima za kufulia gwanji na tope .


Vijana wengi mnaolalamikia ulinzi wa Magufuli mlikua hamjazaliwa na hivyo hamkuyaishi hayo Maisha,ni simulizi tu kwenu.
Kipindi kilibadilika wakati wa awamu ya pili ya Mzee Mwinyi,"trade liberization".

Kwasasa watu wame advance katika elimu,teknolojia ,habari na ufundi,mambo yapo kisasa zaidi,maadui wa taifa wenye uchu na raslimali zetu wameongezeka na wana uwezo mkubwa ki raslimali zote.

Sasa kutaka Rais Magufuli ulinzi wake uwe kama wa JK Nyerere zama hizi za kisasa ni wehu mkubwa, ikizingatiwa kazi afanyayo ni ngumu,ya ku deal na drug dealers ,mafisadi papa,mabeberu,waliokua wanasomba watakavyo maliasili zetu kawadhibiti kwa asilimia kadhaa.
, halafu atembelee V8 mbili ina sense kweli?,
Nikiangalia gharama anayotumia kwa ulinzi kama Amiri jeshi mkuu ni ndogo sana kulinganisha na majukumu yake kwa taifa,kwa dunia ya leo.

Nashauri kila chombo cha kisasa kitumike kumlinda rais dhidi ya kundi lolote halifu kwa nchi yetu.na si aibu hata kidogo.

Nafahamu Mungu ndio mwenye nafasi katika kila nafsi ya mwanadamu,lakini shetani nae ana nguvu zake hapa duniani,hivyo ni haki binadamu kujisaidia mwenyewe dhidi ya hila za shetani.
 
Uko sahihi kabisa, hata huyu anayelalamikia Ulinzi Wa Rais Lazima tujiulize nini maneno yake,,kwanini akahoji Ulinzi huu, umemkwamisha kutenda jambo gani dhidi ya Rais hadi analalamika? Serikali kupitia Cyber Crime Act na TCRA fanyeni uchunguzi dhidi ya Mtu huyu na wenzake
 
hata angekuwa anatembea na baiskeli angekuwa salama tu watu kama kina trump ndio wanasakwa
 
Mleta baada ya rais huyu kutoka madarakani technology itakuwa imeongezeka zaidi lakini kama rais mwingine ataingia madarakani kihalali hatahitaji ulinzi mkali usioendana na kura zake. Hatupingi ulinzi, lakini kama kweli umeingia madarakani kwa kura halali na sio wizi au kupindua nchi, ulinzi wa hivyo ni matumizi mabaya ya pesa za umma kwa kisingizio chochote kile.
 
Mleta baada ya rais huyu kutoka madarakani technology itakuwa imeongezeka zaidi lakini kama rais mwingine ataingia madarakani kihalali hatahitaji ulinzi mkali usioendana na kura zake. Hatupingi ulinzi, lakini kama kweli umeingia madarakani kwa kura halali na sio wizi au kupindua nchi, ulinzi wa hivyo ni matumizi mabaya ya pesa za umma kwa kisingizio chochote kile.
Rais akikubali nchi ipolwe ulinzi wa nini?
 
Back
Top Bottom