Hii hapa ni List ya Mapedeshee/Papaa wa Tanzania na Kazi zao

Hawa jamaa huwa wanafaidi watoto wakali mpaka napata hasira.

VIDEO Queen mwenye taito kubwa Bongo, Rehema Fabian, juzikati alinaswa akifanya mambo ya chumbani hadharani na pedeshee anayefahamika kwa jina la Jacob Best, kitendo kilichozua maswali kibao kutoka kwa wadau walioshuhudia uchafu huo na kutafsiri kuwa ni ufuska, Ijumaa Wikienda linakudondoshea.

Ishu hiyo ilinaswa live na paparazi wetu Oktoba 18, mwaka huu ndani ya New Maisha Club, Masaki jijini Dar es Salaam. Rehema na pedeshee huyo walitinga kiwanjani hapo wakiwa ameshikana mikono, wakajiweka mahali na kuanza kuchapa ‘matingas’ kwa kasi.

Kilevi kilipokolea vichwani mwao, walianza kudendeka hadharani, bila kujali umati wa watu uliokuwa ukiwashuhudia.

“Sikutegemea kama bado Rehema ana tabia za kifuska kiasi hicho. Walichokuwa wanakifanya hakipaswi kufanywa eneo kama hili bali chumbani, ama kweli dunia imekwisha,” alisema mmoja wa shuhuda wa tukio hilo.

Rehema alipotafutwa na kuwekwa mtu kati ili aeleze sababu za kufanya uchafu ule, alifunguka kuwa pedeshee huyo ndiyo mumewe mtarajiwa hivyohaoni ubaya kufanya chochote mahali popote.
 
soma hapa chini upate maana ya mapedegee!

Irene Uwoya awabwatukia mapedeshee - Global Publishers

"MUIGIZAJI ‘hot' katika tasnia ya filamu Bongo, Irene Uwoya (pichani) amewabwatukia baadhi ya wanaume wenye nazo ‘mapedeshee' kwa maelezo kuwa, baadhi yao wana tabia za kike.

Akizungumza na Ijumaa juzikati kwa njia ya simu Uwoya alisema kuwa, amefikia hatua ya kufunguka hayo kutokana na namna ambavyo wamekuwa wakimpa wakati mgumu kwenye maisha yake.

Alisema kuwa, wapo baadhi ya wanaume hao wakimtongoza mwanamke kisha wakakataliwa hutengeneza skendo ili kumchafua kwa makusudi.

"Kwa mfano kuna mapedeshee ambao huja kushinda pale Leaders Club kuwinda wasichana, ukiwachunguza sana utabaini ni mijike dume.

"We angalia kuna jamaa mmoja alikuwa akinitongoza, sijui alidhani mimi mshamba au limbukeni wa magari, baada ya kumkatalia si akaanza kunizushia mambo ya kijinga, yaani sijui wakoje hawa," alisema Uwoya.

Siku za hivi karibuni kumekuwa na utitiri wa baadhi ya wanaume wanaojiita mapedeshee ambao wamekuwa wakitumia fedha zao kuwashawishi mastaa wawape penzi, kitendo kinacholalamikiwa na wasanii wanaojiheshimu"
 
PDG..kwa kifaransa..PRESIDENT DIRECTOR GENERAL..walianzia kongo,kukua kwa muziki wa dansi kukawabatiza watu maarufu hasa vijana wenye mafanikio(wamepataje hatujui) jina hilo...wanaimbwa kwa sababu hutoa sapoti kwa wanaowaimba katika kitu ambacho wazaire hukiita MABANGA(unalitaja jina la mtu ana biashara ama shughuli yake katika tungo zako) na baadaye anakupatia malipo...na wanawake huitwa MASHEBEDEE....NAWASILISHA...

We bwana wewee unatuambia kifaransa halafu unaandika kiingereza maana yake nini???? ama hujui kutofautisha kiingereza na kifaransa??
 
Pedeshee Juma Banatozi mzee wa bwawa la kitaji huyu aliuwawa kwa ujambazi kule Morogoro
 
wengi wao hawajabahatika kwenda shule,kwenda ughaibuni kusaka maisha,hawajoka katika familia za kitajiri,si wakulima ila wanatumia ujanja wa kimjini kuendesha maisha yao!nawakubali sana hawa jamaa kwani kama watoto wazuri wanachukua na kuwahudumia na wanaendesha magari makali!.........piga pesa kwa kumliza mmoja ili watukumi wafurahi!
 
PDG..kwa kifaransa..PRESIDENT DIRECTOR GENERAL..walianzia kongo,kukua kwa muziki wa dansi kukawabatiza watu maarufu hasa vijana wenye mafanikio(wamepataje hatujui) jina hilo...wanaimbwa kwa sababu hutoa sapoti kwa wanaowaimba katika kitu ambacho wazaire hukiita MABANGA(unalitaja jina la mtu ana biashara ama shughuli yake katika tungo zako) na baadaye anakupatia malipo...na wanawake huitwa MASHEBEDEE....NAWASILISHA...

Umenipa shule sikujua kuwa wanaawake nao wanajina lao la kipedeshee
 
wengi wao hawajabahatika kwenda shule,kwenda ughaibuni kusaka maisha,hawajoka katika familia za kitajiri,si wakulima ila wanatumia ujanja wa kimjini kuendesha maisha yao!nawakubali sana hawa jamaa kwani kama watoto wazuri wanachukua na kuwahudumia na wanaendesha magari makali!.........piga pesa kwa kumliza mmoja ili watukumi wafurahi!

Hapo kwenye Red ndio kanuni ya upedeshee si ndio mkuu?Manake ilivyokaa ni kama kanuni vile.
 
Pedeshee simply means "Tapeli",
Yaani ili kutumia tafsida, badala ya kuita Tapeli Shark, ndio unaweza kutumia Pedeshee Shark!!!
 
Pedeshee Ndama, papa msofe, Muzamil Katunzi,Juma nyato, Tom diamond, Charles Mtawali(muzee wa magari), Juma kizaizai, Abdul Mteketa MB,
 
Back
Top Bottom