Hii hapa ndio Kauli Thabiti aliyotuachia Kamanda Alphonce Mawazo

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,627
218,056
Kwamba MTU PEKEE WA KUMUAMINI KATIKA STRUGGLE NI WEWE MWENYEWE , hii ni kwa vile wengi tuliowaamini Wametusaliti .

Hii kauli ingetolewa enzi za mitume basi bila shaka huyu kijana leo tungekuwa tunamsoma kwenye vitabu vya Mungu.

Alphonce Mawazo alikuwa miongoni mwa Wahanga wa mwanzo kabisa kuteketezwa katika Utawala wa awamu ya 5 , aliuawa Kikatili kwa kukatwa na mashoka mithili ya Simba Mla watu na wauaji WALIOTUMWA KUMUUA .Mazishi yake yalizuiwa kwa muda mrefu na Serikali ya Tanzania kwa kutumia Jeshi la Polisi hadi pale Chadema ilipofungua shauri Mahakamani.

Bado mpaka leo tunaendelea kutafuta sababu zilizopelekea serikali ile kuzuia kwa nguvu sana Mazishi Halali ya Alphonce Mawazo , leo Shujaa huyu ametimiza miaka 6 tangu kuuawa kwake .

TUNAMUOMBA MWENYEZI MUNGU AIPOKEE ROHO YA ALPHONCE MAWAZO NA AIWEKE MAHALI PEMA PEPONI , AMINA .

 
Amina Amina Amina Amina Amina Amina Amina.

Lkn elewa kabisa kuwa Mungu daima hamfichi muuwaji maana ukiua nawe utakufa tu.

Leo hii karibia nusu ya walio husika na huo unyama tayari wamesha hukumiwa na mamlaka kuu kutoka juu mbinguni.
 
li ingetolewa enzi za mitume basi bila shaka huyu kijana leo tungekuwa tunamsoma kwenye vitabu vya Mungu.
Lakini si tunaweza kumsoma katika kumbukumbu ya chama!

Hawa ndio mashujaa wa chama mnaotakiwa kuwaweka kwenye historia ya chama. Ni kama wale watakatifu, wafia dini, kama wale wa Uganda, akina Lwanga, Kizito ambao majina yao hadi leo yamo kwenye vitabu vya dini zao kwa kumbukumbu zao.

Hakika Kamanda Mawazo kamwe hawezi kusahaulika katika kumbukumbu za CHADEMA.

Wapo wengi waliojitoa mhanga kukipigania chama wakati mgumu sana. Hawa wanatakiwa kuwekwa katika kumbukumbu zenu na michango yao waliyokifanyia chama.
Hili siyo jambo dogo, ni jambo la heshima sana, na linatoa motisha kwa vijana wengine.
 
Back
Top Bottom