Hii hapa Katiba ya Zanzibar ya 1984 (Toleo la 2010)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,797
11,959
Heshima kwenu wakuu,

KWA KUWA Mkutano wa Baraza la Wawakilishi wa tarehe 9 Oktoba, 1984 kwa niaba ya wananchi wa Zanzibar ulielewa na kukubali kwamba jukumu letu katika historia yaWatu wa Zanzibar kuimarisha Umoja, kuendeleza Mapinduzi ya Kijamaa katika Zanzibar na kusukuma Mapambano ya Ukombozi na harakati za Mapinduzi nchini, katikaAfrika na duniani kote;


NAKWAKUWA tunatambua kwamba Umoja wa Wananchi wa Zanzibar unatokana na ushirikiano wa miaka mingi tangu wakati wa mapambano ya kupigania Uhuru hadi kufikia daraja hii ya mafanikio, na unatokana na siasa yetu ya Ujamaa na Kujitegemea;


NA KWA KUWA tunazingatia na kuthamini kazi nzuri ya Kimapinduzi iliyofanywa naViongozi wa Mapinduzi, wakiongozwa na Mwasisi wa Chama cha ASP na Mapinduzi ya Zanzibar ya 1964, Marehemu Mzee Abeid Amani Karume, ambaye fikra zake zitaendelezwa na kudumishwa daima, kizazi baada ya kizazi katika kupambana na Ukoloni, Ubepari, Unyonge, Uonevu na Dharau, na badala yake kudumisha Uhuru na Umoja, Haki na Usawa, Heshima na Utu;


NA KWA KUWA tunatambua kwamba mafundisho na mawazo ya Kimapinduzi yatalindwa, yataendelezwa na kudumishwa kwa misingi ya Kidemokrasia;


NA KWA KUWA tunatambua kuwa mapambano ya kujenga Ujamaa katika Zanzibar na kushiriki kwetu kikamilifu katika harakati za Mapinduzi ya Zanzibar kunahitaji SHERIA madhubuti itakayowaongoza watu Ki-Katiba, kutokana na fikra za Wafanyakazi na Wakulima;



NA KWAKUWA SISI, Wananchi wa Zanzibar tumeamua rasmi na kwa dhati kujenga katika nchi yetu jamii inayozingatia misingi ya uhuru, haki, udugu na amani;


NA KWAKUWA misingi hiyo yaweza tu kutekelezwa katika jamii yenye demokrasia ambayo Serikali yake husimamiwa na Baraza la Wawakilishi lenye Wajumbe waliochaguliwa na linalowakilisha wananchi, na pia yenye Mahkama huru zinazotekeleza wajibu wa kutoa haki bila woga wala upendeleo wowote, na hivyo kuhakikisha kwamba haki zote za binadamu zinadumishwa na kulindwa na wajibu wa kila mtu unatekelezwa kwa ukamilifu;


KWA HIYO BASI, KATIBA HII IMETUNGWA NA BARAZA LA WAWAKILISHI KATIKAKIKAO CHAKE CHATAREHE 9 OKTOBA,
1984 kwa niaba ya Wananchi, kwa madhumuni ya kujenga jamii kama hiyo, na pia kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Zanzibar inaongozwa na Serikali yenye kufuata misingi ya demokrasia na ya kijamaa.

Habari zaidi soma Kiambatanisho.
 

Attachments

  • Katiba_ya_Zanzibar_ya_1984_(Toleo_la_2010)_en.pdf.pdf
    18.5 KB · Views: 230
Hamna kitu hapo wewe weka katiba tusome, acha utoto wewe, yaani unatuwekea kitu gani hiki sasa, Yaani hamna kitu
 
Katiba za nchi hii ni kwa ajili ya wananchi tu , viongozi wanaisigina kila siku .
 
Back
Top Bottom