Hii hapa hukumu ya Kiswahili iliyotolewa na aliyekuwa Jaji wa Mahakama kuu ya Tanzania Mh. Galeba

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,211
5,937
Nimeisoma hukumu hii na kwa maoni yangu JPM ametenda haki kumpandisha cheo.

Aidha nitoe rai kwa vyuo vyetu vikuu vione namna ya kutambua mchango wa Jaji Galeba wafikirie kumpa Udaktari wa heshima.
 

Attachments

  • Galeba.pdf
    595.8 KB · Views: 74
Ningeshauri wapewe udaktari wa heshima raia wote wanaohangaika kutengeneza dawa za Corona asilia, wao ndio wanamchango mkubwa zaidi kwa jamii kuliko huyo alieandika hukumu kiswahili.

Sasa hivi tanzania kuna ufumbuzi wa zaidi ya dawa asilia 1,000 za Covid 19 zinazopigiwa Promo. So unaweza kushangaa zikatakiwa kutolewa "DOCTORATE ZA HESHIMA" kwa raia 3,500 nchi nzima. Mpaka Corona iishe raia wanaweza kufika 5,000 wenye Doctorate Za Heshima. Alievumbuwa "NYUNGU" apewe u "PROFESSOR" kabisa.

Ila chonde chonde kuna siku tutakuja kunyweshana sumu.
 
Hebu tuwekee hapa mkuu
1694536_IMG-20180227-WA0007.jpg
 
Mkuu nimeipitia niyakawaida tofauti ni Lugha tu ila kumpa Ujaji niswala la utashi wa ksiasa.
 
mimi pia napongezs watooe hukum kwa kiswahil.kwa yale maneno ambayo yahitaji ufafanuz unayatafsir tu.kuna ishu ilitokea kwamba kesi isiklizwe upya.ila ilo neno sasa la kilatin balaaa.
 
Jaji alikua na bahati tu maana hiyo siyo hukumu ya kwanza ya mahakama ya juu kwa kiswahili .

Ipo hukumu ya mahakama ya rufani iliyoandikwa kwa Kiswahili ilikua inahusiana na ule mvutano wa kama YESU ni Mungu ama la?

Nadhani mnakumbuka ishu ya DIBAGULA.

Kwahiyo bahati ilimuangukia kama dodo.
 
Back
Top Bottom