Hii Hali ya Umeme kutouwepo siku nzima maeneo mbalimbali ya nchi, tatizo nini

ubarinolutu

JF-Expert Member
Oct 22, 2012
1,964
3,895
Umeme kwa huu mwezi unakatika Sana siku nzima, ukiuliza emergency wanajibu matengenezo, nimetembea mikoa Saba mwezi huu shida Ni hiyo hiyo, huku wengine wanasema mitambo imechakaa , huku wengine wanasema stigler, wengine wanasema mgao wa kimya kimya, embu serikali itoe kauli Kama Kuna mgao tukanunue mishumaa, mficha malazi kifo umumbua
 
Kahama huku imekuwa Kama jadi yani.kila siku umeme hakuna.Tanesco kama kazi imewashinda semeni mapema
 
Morogoro imekuwa ni kawaida saana hata Jana huku nilipo wamekata kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 1 usiku na hata uliporud bdo ni baadhi ya maeneo
 
Umeme kwa huu mwezi unakatika Sana siku nzima, ukiuliza emergency wanajibu matengenezo, nimetembea mikoa Saba mwezi huu shida Ni hiyo hiyo, huku wengine wanasema mitambo imechakaa , huku wengine wanasema stigler, wengine wanasema mgao wa kimya kimya, embu serikali itoe kauli Kama Kuna mgao tukanunue mishumaa, mficha malazi kifo umumbua
Tanesco wameshashindwa kuhudumia! Dawa ni kuruhusu makampuni mengine yaanze kusambaza umeme!!
 
Morogoro imekuwa ni kawaida saana hata Jana huku nilipo wamekata kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 1 usiku na hata uliporud bdo ni baadhi ya maeneo
Duuh!! Moro nilikuwa naisifia, kumbe nako shida!! nimekaa sana hapo mkuu!!
 
Kumbe ni tatizo la nchi nzima. Hii Nchi huwa inaahidi uongo tu sometimes

Umeme kukatika imekuwa ni jambo la kawaida.
 
Kuna tatizo kubwa sana ambalo serikali inaoogopa kulisema maana iko kwenye sifa mode, hivyo inaona itadharauliwa. Tatizo hili lilianza toka mwezi wa tisa na kuendelea kukua kidogo kidogo. Walijikaza hapo katikati kwani ilikuwa tunaingia kwenye uchaguzi. Kwasasa ni kama mambo ya mficha maradhi kifo humuumbua. Niliposikia tangazo kuwa taasisi za umma ambazo hazijalipwa umeme zitakatiwa, nikajua muda wa ukweli kukaa wazi umewadia.
 
Umeme kwa huu mwezi unakatika Sana siku nzima, ukiuliza emergency wanajibu matengenezo, nimetembea mikoa Saba mwezi huu shida Ni hiyo hiyo, huku wengine wanasema mitambo imechakaa , huku wengine wanasema stigler, wengine wanasema mgao wa kimya kimya, embu serikali itoe kauli Kama Kuna mgao tukanunue mishumaa, mficha malazi kifo umumbua

Tumetoa tangazo la matengenezo katika mashine zetu za kuzalisha umeme

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

DESEMBA 17, 2020

TAARIFA YA MATENGENEZO KATIKA VITUO VYA KUZALISHA UMEME VYA KIDATU, KINYEREZI II NA SONGAS.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa kuna matengenezo katika Kituo cha Kufua Umeme kwa maji cha Kidatu na Vituo vya Kufua Umeme kwa Gesi Asilia vya Kinyerezi II na Songas.

Kutokana na matengenezo hayo, baadhi ya maeneo nchini yataathirika kwa kukosa huduma ya umeme kwa nyakati tofauti.

Wataalamu wetu na mafundi wanaendelea na kazi kuhakikisha mashine zinatengemaa haraka.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza

Tafadhali usiguse wala kukanyaga waya uliokatika au kudondoka chini.

Toa taarifa Ofisi za TANESCO zilizo karibu nawe, au wasiliana nasi kupitia namba za simu zifuatazo: - Kitengo cha Miito ya Simu 0222194400 na 0768 985100

Mitandao ya Kijamii :
Website:

www.tanesco.co.tz

Instagram: tanescoyetu

Barua pepe: customer.service@tanesco.co.tz,

Twitter: www.twitter.com/tanescoyetu

Facebook: Tanesco Yetu

Imetolewa na;
OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO MAKAO MAKUU.
 
Hao wengine huo umeme wanautoa wapi?.
Mkuu, maisha ya tz kila kitu tumeingiza siasa!! sikana kwamba vyavyo vya umeme havipo!!

Lakini watu hawajawa serious na kazi!! Sasa utakapo muwekea ushindani. atajirekebisha!!
 
Tumetoa tangazo la matengenezo katika mashine zetu za kuzalisha umeme

SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

DESEMBA 17, 2020

TAARIFA YA MATENGENEZO KATIKA VITUO VYA KUZALISHA UMEME VYA KIDATU, KINYEREZI II NA SONGAS.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa kuna matengenezo katika Kituo cha Kufua Umeme kwa maji cha Kidatu na Vituo vya Kufua Umeme kwa Gesi Asilia vya Kinyerezi II na Songas.

Kutokana na matengenezo hayo, baadhi ya maeneo nchini yataathirika kwa kukosa huduma ya umeme kwa nyakati tofauti.

Wataalamu wetu na mafundi wanaendelea na kazi kuhakikisha mashine zinatengemaa haraka.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza

Tafadhali usiguse wala kukanyaga waya uliokatika au kudondoka chini.

Toa taarifa Ofisi za TANESCO zilizo karibu nawe, au wasiliana nasi kupitia namba za simu zifuatazo: - Kitengo cha Miito ya Simu 0222194400 na 0768 985100

Mitandao ya Kijamii :
Website:

www.tanesco.co.tz

Instagram: tanescoyetu

Barua pepe: customer.service@tanesco.co.tz,

Twitter: www.twitter.com/tanescoyetu

Facebook: Tanesco Yetu

Imetolewa na;
OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO MAKAO MAKUU.
Hivi matangazo yenu kama haya huwa mnayaweka wapi hasa? Maana katika hizo social network ulizotaja sijaona tangazo la katazo la umeme.... Muwe update katika hizo social network zenu, kama mnataka kukata umeme mahali bas mtoe taarifa watu wajue.
 
Matengenezo sio hoja, hoja Ni mgao, uzalishaji haukizi mahitaji, hiyo ziada kila Mara ambayo serikali imesema ipo iko wapi, ndo ilipaswa kutumika wakati huu, hakuna Cha ziada Wala Nini huu Ni mgao wa umeme Tena Ni mgao mkali sana
 
Back
Top Bottom