Uta Uta
JF-Expert Member
- Feb 2, 2016
- 3,739
- 8,736
Habari wanajamvi?
Teklojia ya mawasiliano imekuwa kiasi ambacho unaweza kufanya mambo mengi kupitia simu yako ya mkononi. Zamani kidogo tulianza kwa kutumia miche ya sabuni, ikaja kichwa cha kambale, baadae dole gumba ikafuatiwa na kitochi. Ila tumeenda mbali zaidi mpaka leo tupo katika android. Nikirudi katika mada yangu kuna hii tabia iliyozuka miaka ya karibuni ya watu kupiga picha ya matukio mbali mbali na kuyarusha katika mitandao ya kijamii. Tena watu hawajali hata utu wakifika eneo la tukio msaada mkubwa wanaoutoa wao ni kupiga picha tu. Kibaya zaidi hawa wapiga picha hawana mipaka wala tafsida, wao wanapiga tu iwe jeshini, ikulu, kituo cha polisi chumbani na kwingineko bila kujali madhara ya picha hizo kwa familia na jamii kwa ujumla. Kilichonisikitisha zaidi ni hili tukio la Mh Malima, polisi walikuwa wanatekeleza majukumu yao ya kawaida, ila kuna mdada amekaa pembeni anawapiga picha huku akishabikia analikoki, mtatuua, we kaka pisha unaniziba nk, sijui kama taratibu za jeshi la polisi linaruhusu kupigwa picha katika utekelezaji wa majukumu yake bila utaratibu maalum (kibali), kama sheria haziruhusu mi nashauri yule dada atafutwe na jeshi la polisi na ashughulikiwe ipasavyo. Vyombo vyetu vya ulinzi viheshimike ipasavyo, Pia nashauri serikali iandae sheria maalum ili wote wanaopiga picha kiholela kwa matukio yasio stahili wachukuliwe sheria, pia mamlaka ya mawasiliano utusaidie kutuelimisha ni utaratibu gani niufuate pindi nitakapo kuta picha yangu katika mtandao bila ya idhini yangu.