Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,258
- 20,707
Najua ukikutana na wanawake 10 barabarani kati yao 9 au wote kumi wametengeneza nywele,yaani wameziondoa kwenye uhalisi wake na wanataka zifanane na za wazungu,waarabu wachina n.k,ukiwauliza sababu hasa ya kufanya hivyo watakuambia "ili wapendeze" kwao kua na nyele ndefu ndo kupendeza!Hili ni tatizo na pia ni maradhi,ni tatizo la kujikataa.Unafikia mahali unadhani hukustahili kuwa na nywele hizo,hili nalo halina tofauti na wale wanaojichubua ngozi zao ili wawe weupe,wanaona weusi ni ubaya,wanajikataa!Watu weusi tumekua na maradhi haya kwa muda sasa,tunaona tumekosewa kuumbwa what a shame!!Hebu fikiria unafikia mahali unabadili ngozi na nywele za asili ukidai eti unataka "kupendeza"!Shame on us black people!Nani kakuambia kua na rangi nyeupe na nywele ndefu ndo kupendeza?Hii ni kwa jinsia zote.Cha kushangaza utamkuta mdada kaenda saloon "kutengeneza" nywele halafu anamzodoa na kumkejeli mwenzie aliechubua ngozi utadhani wanatofauti!WATU WEUSI,TUJITAMBUE NA KUIONA THAMANI YETU!