Hii habari ya Jumatano ya Majivu asili yake ni nini!?

Yesu hakuacha kanisa wala hakuwahi kuanzisha kanisa, hivyo ni uwongo uliokithiri kudai kwamba Roma ndio kanisa mama aliloacha Yesu, in short Waroma/Wakatoliki ni mwendelezo wa dini ya Mafalsayo na masadukayo ,dini zile za mapokeo ya asili ambayo ndio waliokuwa wakimpinga saana Yesu hadi wakamuua na wakatunga uwongo kwamba hakufufuka bali aliibiwa mwili wake kabirini. Ukatoliki ni ka mfumo tu kaliko kinyume na Yesu / Mungu Ila kamejificha ficha ktk baadhi ya maandiko
Mathayo 16:13-20
Nimenukuu mstari wa 18-19
18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
19 Nami nitakupa wewe funguo za ufalme wa mbinguni; na lo lote utakalolifunga duniani, litakuwa limefungwa mbinguni; na lo lote utakalolifungua duniani, litakuwa limefunguliwa mbinguni.
 
Mnahangaika na kupiga mikelele humu sisi Wakatoliki tuko pouwa kwa saana na Ibada zetu toka lini kelele za mlango zikamzuiya mwenye nyumba kupata usingizi
 
dogo walahi una ilimu hii ulio post kakufundisha quran, hadith, au miratul rasul
Unataka kula BAN tena? Yaani juzi ulikua kifungoni. Ile kuachiwa tu tayari umeshatafuta uzi wa mambo ya dini! Utarudi jela muda mfupi sana....!
 
Unataka kula BAN tena? Yaani juzi ulikua kifungoni. Ile kuachiwa tu tayari umeshatafuta uzi wa mambo ya dini! Utarudi jela muda mfupi sana....!
mimi napata thawab... jibu basi dogo hiyo ilimu ya majivu kakufundisha nani?
 
Ila nlichogundua Watu wanajua kuunga Dotts vizuri sanaaaaa.,Suala la majivu origin yake ni km "DERIVATION OF FORMULA",.Maana imepelekwa mpk mzizini.,Anyway
Safii
 
Hoja zimekata unatafuta kampani we pambana tu kama vipi mpe namba ya paroko amsimulie.... nacheka saana.
Kama Yesu aliwatimua waliokuwa wakifanya bness kwenye sinagogi sidhani kama alikuwa anakubali masanamu hadi iwe sunna
 
Kwa uelewa wangu mdogo ..

Ukisoma biblia kwa umakini utajua kuwa kujipaka majivu (kama ishara ya toba ) ,kufunga na kuomba ilikuwa ni kitu kimoja ambacho mojawapo kilichotumika kuomba toba na huruma ya Mungu..

Kaangalie katika kitabu cha ester pale waraka wa amani ulipotoka wa kuwaangamiza wana wa israel..mordekai na waIsrael walivaa magunia na kujipaka majivu

Kaangalie katika kitabu cha Ayoub pale alipofikwa na mabaya ..

Kaangalie pia katika kitabu cha Yona pale watu wa mji wa ninawi walipopata taarifa ya mji wao kuangamizwa na Mungu ..walifanyaje pia katika kuomba huruma ya Mungu

Mimi sio mzuri wa kukariri mistari hivyo utaniwia radhi
kwa nn wakatoriki mnabibila yenu yenye vitabu kadhaa na halikadharika walutheran wao wana idadi tofauti ya ya kwenu. Waprotesant wanayakwao tofauti ya vitabu vya Waroma na walutherani kwa idadi
 
Samahanini.
Hapa naona kuna majadiliano yanayotofautiana kimtazamo wa tendo la Majivu.
Hapa kuna nadharia mbili zinazo kinzana na kuchanganywa.

1. Iko nadharia ya Dini au Dhehebu au Imani flani.

2. Iko nadharia ya Imani ya Kikristo.

Nianze na nadharia ya pili.

UKRISTO ni kufuata maagizo yote yaliyoa amriwa na Yesu Kristo kuyatekeleza.
Ni kujifunza na kufanya maagizo ya Yesu Kristo.
Wanaofuata hayo maagizo wanaitwa Wanafunzi wa Yesu Kristo, ambao wanajenga mahusiano mema na Yesu kama kiongozi wao.
Yesu ndiye Kristo.

Note.
Wafuasi wa Musa, au Nuhu, au Ibrahimu, au Ellen G. White, au Gullam, sio Wakristo.

DINI ni dhehebu la Kiimani lenye matendo ya kuabudu.
Ziko dini zinabudu Sanamu, Miti, ng'ombe, Jua, Mwezi, Watu, Miungu, Mungu nk.

Kama nilivyoeleza hapo juu.
Bwana Yesu alishasema wazi kwa kuwaagiza wanafunzi wake
kwamba ;

"Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi..............na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi"
Mathayo 28: 18-20.

Anayeyashika yote aliyoyaamuru Yesu Kristo, huyo ndiye ni Mkristo, na imani yake ni Ukristo, kwa lugha nyepesi "U-yesu" "U-kristo"

Je Yesu Kristo, aliwaamuru wanafunzi wake kufundisha kupaka Majivu ?

Kama ndiyo, basi ibada ya Majivu ni ibada ya Kikristo.

Kama sio, basi Ibada ya Majivu ni ya Dini au Dhehebu flani, na sio ya Imani ya Kikristo.

Kristo ndiye NJIA, KWELI na UZIMA.
Kweli na iwe Kweli nayo Kweli itatuweka Huru.

Alleluya.
 
Aliye anzisha haya matatizo ni shetani japo siyo jina lake kitu chochote ukitaka kukijua ni lzm uanzie mwanzo kwanza nitoe msisitizo tupende kusoma sana
 
Wakatoliki ndio wanaweza kuwa na majibu.

Hakuna mahali popote katika Biblia panapozungumzia J5 ya Majivu.

Hakuna mahali popote katika Biblia panapozungumzia Kwaresima.

Wanadai wanafunga siku 40 jambo ambalo kimahesabu haliji, unafunga asbh mpk saa 12 jioni halafu unadai umefunga siku nzima!

Haya yote ni mapokeo ya wanadamu yaliyotokana na Mitaguso ya Papa gani huko kwao, pamoja na hayo unaweza kuongezea:

Sala ya Rozari
Ibada za wafu
Masanamu yaliyojazana kwenye majengo yao ya ibada
Mapadri kutofunga ndoa ilihali tamaa zinawawaka
Ulevi

Na mengineyo yaliyo nje ya muongozo wa Biblia
Kila kanisa lina mapungufu yake hakuna ambalo halina, kukosoa usichokijua na kutokua na mamlaka ya kukosoa ni ulimbukeni na dalili ya kutangatanga kidhehebu, Mungu kakuumba na busara ya kuchuja na kuyafuata yaliyo mema hapohapo ulipo, mimi naamini ya kuwa sina mamlaka ya kukosoa dhehebu lolote lile hapa duniani ndio sababu kwa busara kabisa ninafocus kwenye imani niliyobatizwa na kuyafuata yale mema ambayo roho mtakatifu ananiongoza. Jifunze kutofautisha amri za kanisa na maandiko matakatifu, kila kanisa lina amri na sheria zake ila sisi waumini wa haya makanisa twaongozwa na imani zetu na busara tulizozaliwa nazo, tuheshimiane, kwa mfano napita eneo fulani nakuta waumini wanasali kwa kulia machozi na kujigalagaza chini kila jumapili, hata kama siwaelewi siwezi kuwacheka, kuwakosoa wala kuwanyooshea kidole. Ubarikiwe!
 
Samahanini.
Hapa naona kuna majadiliano yanayotofautiana kimtazamo wa tendo la Majivu.
Hapa kuna nadharia mbili zinazo kinzana na kuchanganywa.

1. Iko nadharia ya Dini au Dhehebu au Imani flani.

2. Iko nadharia ya Imani ya Kikristo.

Nianze na nadharia ya pili.

UKRISTO ni kufuata maagizo yote yaliyoa amriwa na Yesu Kristo kuyatekeleza.
Ni kujifunza na kufanya maagizo ya Yesu Kristo.
Wanaofuata hayo maagizo wanaitwa Wanafunzi wa Yesu Kristo, ambao wanajenga mahusiano mema na Yesu kama kiongozi wao.
Yesu ndiye Kristo.

Note.
Wafuasi wa Musa, au Nuhu, au Ibrahimu, au Ellen G. White, au Gullam, sio Wakristo.

DINI ni dhehebu la Kiimani lenye matendo ya kuabudu.
Ziko dini zinabudu Sanamu, Miti, ng'ombe, Jua, Mwezi, Watu, Miungu, Mungu nk.

Kama nilivyoeleza hapo juu.
Bwana Yesu alishasema wazi kwa kuwaagiza wanafunzi wake
kwamba ;

"Basi enendeni mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi..............na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi"
Mathayo 28: 18-20.

Anayeyashika yote aliyoyaamuru Yesu Kristo, huyo ndiye ni Mkristo, na imani yake ni Ukristo, kwa lugha nyepesi "U-yesu" "U-kristo"

Je Yesu Kristo, aliwaamuru wanafunzi wake kufundisha kupaka Majivu ?

Kama ndiyo, basi ibada ya Majivu ni ibada ya Kikristo.

Kama sio, basi Ibada ya Majivu ni ya Dini au Dhehebu flani, na sio ya Imani ya Kikristo.

Kristo ndiye NJIA, KWELI na UZIMA.
Kweli na iwe Kweli nayo Kweli itatuweka Huru.

Alleluya.

mkuu unaisomaje Biblia Takatifu? hebu soma hii mistari mimili halafu ikatae jumatano ya majivu kwa hasara yako
john2031.jpg
Matthew16_19.jpg
 
mkuu unaisomaje Biblia Takatifu? hebu soma hii mistari mimili halafu ikatae jumatano ya majivu kwa hasara yako View attachment 700441 View attachment 700442
Mkuu mimi katu sijaikataa Jumatano ya majivu.
Kwani kupaka majivu ni dhambi ?
Nina uhakika sio dhambi.
Nimesema ni aina ya Ibada ya dhehebu flani.
Kwani sio wakristo wote wanaopaka majivu.
Kama kupaka majivu kutaongeza imani ya Kristo kwa waumini basi haina tatizo mkuu.
Imani ya Kristo ipo kiroho zaidi, mambo kama ya kunawa uso na maji ya baraka, kupaka majivu, kukomnika nk, ni ya kimwili zaidi na ndio matendo ya ibada hayo.
 
Back
Top Bottom