Hii habari ni kweli na huyu Miss ni nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hii habari ni kweli na huyu Miss ni nani?

Discussion in 'Celebrities Forum' started by FairPlayer, Mar 25, 2010.

 1. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #1
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Jamani nimeona hii habari wala sijaielewa:


  Gazeti ‘The Biggest IQ' Ijumaa Wikienda, halina cha kupoteza kwa kuthubutu kuondoa wingu hilo na kueleza kinagaubaga kuhusu tukio zima kwa kuweka hadharani maelezo ya pande zote mbili na jinsi Jeshi la Polisi Kanda ya Dar chini ya Kamanda Suleiman Kova, lilivyo hoi kiasi cha kuchelewa kupata hatma.

  Gazeti ndugu na hili la Ijumaa lilikuwa la kwanza kuripoti habari ya Miss Tanzania Top 10 mwaka 2008 – 09 (jina linaendelea kuhifadhiwa kwa sababu za kimaadili) kubakwa baada ya kuleweshwa na Patrick.


  Ijumaa Wikienda linakwenda mbele zaidi kwa kuchambua utata mkubwa ambao unalizingira tukio zima kiasi cha kulipa msukosuko Jeshi la Polisi ambalo mpaka leo limeshindwa kuchukua uamuzi wa kuifikisha kesi hiyo kwa Pilato a.k.a mahakamani.


  Tukio hilo la Miss kubakwa, linadaiwa kuchukua nafasi Machi 13, 2010 (Jumapili) lakini mpaka leo Machi 22, 2010 ikiwa ni siku tisa baadaye, kesi hiyo haijafikishwa mahakamani na inaendelea kuzungushwa polisi.


  Kitendo cha kuzungushwa polisi bila kufikishwa mahakamani, kumekuwa na taswira yenye shaka kwamba huenda zinafanyika jitihada za kulimaliza shauri hilo kabla ya kufika mahakamani.


  Endapo hilo litafanikiwa, bila shaka Jeshi la Polisi litakuwa limetenda dhambi kwa sababu sheria inakataza kwa kesi za ubakaji na mauaji kuzungumzwa achilia mbali kumalizwa nje ya Mahakama.


  Uchunguzi wa Ijumaa Wikienda umebaini kauli tata zinazopishana kutoka pande mbili yaani kwa mlalamikaji na mtuhumiwa, pia mazingira ya kitendawili kigumu kuteguka yanayoelezwa na mlalamikaji ambaye ni Miss Tz.


  MAELEZO KUTOKA KWA MISS TZ

  Kauli za Miss Tz kama alivyosimulia na maelezo yake kuhifadhiwa kwenye kitabu cha Ripoti za Polisi (Report Book au kwa kifupi RB) na katika faili la mpelelezi wa kesi ni kwamba mrembo huyo alibakwa baada ya kuleweshwa.

  Mrembo huyo ambaye alipitia kitongoji cha Dar City Centre na Kanda ya Ilala, akiwa na kampani ya ‘mashosti' zake watatu, siku ya tukio, walikuwa ‘wakipombeka' kwa vileo vya bei mbaya ndani ya Hoteli ya Sea Cliff, Oysterbay, Dar es Salaam.


  Wakiwa wanapombeka, Patrick aliungana nao huku naye akiwa ameshika pombe yake na baada ya muda, mrembo mwingine mwenye asili ya Bara la Ulaya alijumuika nao, hivyo kutimiza timu ya watu sita.


  Baada ya kugida kinywaji huku wakiongea stori za hapa na pale, likaja wazo la wao kwenda Club Bilicanas ‘Billz' ambapo wote waliingia kwenye gari la Patrick na safari ya kuelekea klabu hiyo iliyopo Posta Mpya, Dar ikaanza.


  Alieleza kwamba walipofika Billz, warembo hao walishuka na kuingia klabu huku Patrick akibaki kwenye gari lakini baada ya muda naye aliteremka, akafunga ‘motokaa' lake na kuingia ‘mjengoni'.

  Miss huyo alieleza polisi kuwa baada ya Patrick kuingia ndani ya klabu, aliwafuata na kuwauliza kama wapo tayari kwa ofa yake ya vinywaji lakini warembo hao wakadai bado wanayo ‘stoko' waliyotoka nayo Sea Cliff, hivyo zikiisha ataruhusiwa kuwanunulia.


  Inaelezwa kuwa baada ya kauli hiyo, Patrick aliondoka lakini aliporudi alikuwa na kinywaji kingine kinachoingiza kilevi mwilini (jina tunaliminya) kikiwa ndani ya glasi ambacho alimkabidhi mrembo huyo ambapo baada ya kupiga funda kadhaa alianza kulegea.


  Mrembo huyo alieleza kuwa palipopambazuka, alijikuta akiwa amelala kitandani kwenye chumba asichokijua kabla ya kukutanisha macho na Patrick ambaye bila kuficha alijisifu kwamba alimuingilia kimapenzi tena akishirikiana na vijana wengine watatu.


  Miss Tz huyo ambaye yupo ‘sexy' kimuonekano, alisema kuwa baada ya majibu hayo ya Patrick, ilibidi amlaghai kwa maelezo kuwa amemkubalia waendelee kuwa wapenzi kwa dhati badala ya kubakana, hivyo akamuomba waongozane hadi nyumbani kwao, Upanga, akamtambulishe kwa wazazi wake.


  Aliongeza, nyumba aliyobakwa ipo Mbezi Beach, hivyo walisafiri hadi Upanga ambako alimkaribisha Patrick sebuleni, kisha yeye akaenda kuteta na ndugu zake kuhusu unyama aliotendewa.


  Alisema, baada ya kuwaeleza ndugu zake, walimkamata Patrick hadi Kituo Kidogo cha Polisi Upanga kabla ya kurushwa Kituo cha Selander Bridge ambako kesi hiyo ilipokelewa na kupewa nambari SBR/RB/470/2010 KUBAKWA.


  Baada ya kufika Selander Bridge, mrembo huyo alitoa maelezo kwamba alitendewa ubakaji Mbezi Beach, hivyo kesi hiyo ilihamishiwa Kituo cha Polisi Kawe na kuripotiwa kwa nambari KW/RB/2325/2010.


  MAELEZO YA PATRICK

  Katika kufuatilia mbivu na mbichi, gazeti hili lilizungumza na Patrick ambaye alisema kuwa yeye hakumbaka mrembo huyo, isipokuwa kesi imetengenezwa kwa lengo la kujinufaisha kimaslahi.

  Patrick alisema: "Stori ipo hivi, nilikutana na … (anamtaja jina mrembo huyo) Sea Cliff Hotel baadaye tukaenda Bilicanas. Mimi nafahamiana naye kwa muda na nimekuwa nikimsaidia mambo mengi kwa sababu sisi wote ni wanamitindo.


  "Tuliachana Bills mimi nikarudi nyumbani kwangu, asubuhi kwenye saa tano nilipokea simu ya … (anataja tena jina la mrembo) akiniomba niende nyumbani kwao kwa sababu ana shida na mimi.


  "Kwa sababu tunafahamiana sikuwa na tatizo, nilikwenda na nilipofika nyumbani kwao ilikuwa ni majira ya saa saba mchana. Alinikaribisha vizuri nikaketi lakini nikiwa sebuleni aliingia mwanamke mmoja ambaye nilikuja kugundua ni mama yake.


  "Yule mwanamke aliniambia kuwa yeye ni mwanamke wa kirashia, kwahiyo ni lazima atanionesha kazi kwa kitendo cha mimi kumbaka mwanaye, nikashangaa, nikauliza kumbaka nani? Akaniambia nimembaka … (anataja tena jina la mrembo).


  "Hapo hapo … (jina la miss) akanigeuka, wakaingia watu wengine, wanawake wawili na mabaunsa wawili ambao walianza kunipiga na kunilazimisha nikubali kuwa nimembaka … (jina), vinginevyo wangeniua.


  "Kutokana na ukweli kwamba walikuwa wamenipiga sana ilibidi nikubali, baada ya hapo wakaniambia ni lazima niandike maelezo ya kukiri na ni lazima nitoe faini.


  "Waliniambia nikubali kulipa dola 5,000 (kama shilingi 6,700,000) lakini mimi nikasema naweza kulipa 1,000,000. Wakasema nilipe pale pale ‘keshi', mimi nikawaambia kwa pale pesa niliyokuwa nayo ni shilingi 500,000, wakachukua.


  "Huku wakinipiga, walinilazimisha nisaini kwamba nitalipa hizo pesa kwa kosa la kumbaka … (jina), kwahiyo nilisaini kwa kuona hiyo ndiyo njia pekee ya kujiokoa na kipigo.


  "Hata hivyo haikusaidia, wakaendelea kunipiga mpaka jioni, fikiria tangu saa saba mpaka saa moja jioni napigwa, wakatishia kunifanyia kitu kibaya zaidi, hapo nikapiga kelele nyingi za kuomba msaada.


  "Unajua mazingira ya Upanga na ile nyumba, ilikuwa ngumu kwa majirani kusikia lakini baadaye walisikia, hivyo wakatoa taarifa polisi ambapo askari walifika, wakaingia ndani na kunibeba hadi kituoni.


  "Pale Selander nilieleza kila kitu lakini nashangaa polisi walinigeuka, mara tukapelekwa Kawe. Tangu wakati huo nimekuwa nikiomba kesi hii iende mahakamani ili ukweli ujulikane kwa sababu mimi sijambaka… (jina).


  "Na hizo picha za … (jina), walimpiga ndugu zake pale pale nyumbani kwao ili kutengeneza mazingira ili ionekane nilimpiga baada ya kumbaka. Walivunja simu zangu, wakachukua laptop kwenye gari.


  "Nashangaa tangu tufike polisi, ndugu zake wamekuwa waking'ang'ania niwalipe shilingi 500,000 ili kesi iishe, hawataki iende mahakamani. Mimi nataka kesi iende mahakamani ili ukweli ujulikane. Nimenyanyswa sana, nimepigwa na nimedhalilishwa.


  "Badala ya kupelekwa mahakamani, kesi yetu imepelekwa Oysterbay Polisi huko nako tumeambiwa kuna watu wawili waliwahi kupelekwa na … (jina) kwa nyakati tofauti kwa madai kwamba walimbaka lakini badala ya kwenda mahakamani, akaomba alipwe fidia, wakamalizana. Hii ni kutengeneza, sijabaka na wala sina sababu ya kubaka."


  MASWALI TATA

  Kwanini mrembo huyo atake fidia ya pesa kwa kubakwa? Je, kitendo cha yeye kubakwa anakilinganisha na shilingi 1,000,000 ndiyo maana ‘anakomalia' shilingi 500,000 iliyobaki?

  Ndugu wa mrembo huyo walimsainisha Patrick kama ushahidi, je, ushahidi wa Kipolisi na Kimahakama, unaweza kuthibitisha tendo la ubakaji kwa sahihi badala ya vipimo vya daktari?


  HEKA HEKA POLISI

  Kwa ufuatiliaji wa tukio hilo wiki iliyopita, tuliweza kugundua kwamba shauri hilo limekuwa likihamishwa vituo mara kwa mara.

  Lilianzia Kituo kidogo cha Polisi, Upanga, likapelekwa Selander, baadaye Kawe, likahamishiwa Oysterbay na Ijumaa iliyopita lilipelekwa Kituo cha Wazo Hill lakini baadaye Patrick na Mrembo waliitwa Kituo Kikuu cha Dar (Central).


  Central, kikao kikuu kilifanyika kwa vigogo wenye nyota zao kuzungumza na mrembo huyo pamoja na Patrick hasa baada ya gazeti ndugu na hili la Ijumaa, kuripoti habari hii kwa mara ya kwanza.


  Kikao kilichukua muda mrefu na ilipofika machweo, Patrick alibanwa nyuma ya nondo (mahabusu) ili kurahisisha upelelezi wa kesi kuchukua nafasi ya mafanikio.


  KUTOKA IJUMAA WIKIENDA

  Hapa kuna utata na ili haki itendeke, shauri hili ni vema likafika mahakamani. Kama mrembo huyo katendwa basi Patrick ashughulikiwe kulingana na sheria za nchi zinavyoongoza.

  Ikiwa mrembo huyo na familia yake walifanya mtego kwa lengo la kujipatia fedha, basi naye alipie gharama ya kitendo alichofanya mbele sheria. Ieleweke kuwa hii ni Dar yenye mambo na hila nyingi. MHARIRI.


  Source:http://www.globalpublisherstz.com/ijumaawikienda
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Mar 25, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Mtu aliyebakwa asingedai fidia harakaharaka namna hiyo na sidhani km kuna ripoti ya dr kuthibitisha hilo
   
 3. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #3
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Issue nzima inaendeshwa ki ajabu ajabu sana. Polisi wa bongo bwana!!
   
 4. m

  mnyakyusa JF-Expert Member

  #4
  Mar 25, 2010
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 248
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Aliyebakwa angetembea mpaka kwao jamani?? msicheze na kubakwa labda kama ndio dili zake huyo miss
   
 5. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #5
  Mar 25, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  pengine hakudai fidia yeye .....tusimhukumu
  labda hao kaka zake ndo walodai pesa

  yote yanawezekana kwa tanzania hii, acha ende mahakamani tujue ukweli
   
 6. Sal

  Sal JF-Expert Member

  #6
  Mar 25, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 500
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  hebu tuambieni jina lake huyu miss uchwara maana tayari ni tapeli, hakuna sababu ya kuficha jina hapa, ili wengine nao wakimuona wamuogope kama ukoma.
   
 7. Mgeninani

  Mgeninani Senior Member

  #7
  Mar 25, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Njaa kali!
   
 8. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2010
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Jamani wana JF hatumjui huyo miss anayeishi UPANGA dar?
   
 9. Mgosi wa Sui

  Mgosi wa Sui Member

  #9
  Mar 26, 2010
  Joined: Aug 22, 2009
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Gazeti moja lilimtaja nakumbuka jina la kwanza tu ni Nelly
   
 10. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2010
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Yule mdada mwenye blog ya Uturn , yeye kamtoa na jina na picha kabisa..
   
 11. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #11
  Mar 26, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 819
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Dah nilisha msahau Nelly, kweli Nelly mama yake ni Mrussia na ina wezekan ni huyo, ila dah sikujua kama ni njaa kali kihivyo ya $5,000 ,kubakwa tena mtungo na watu watatu halafu jiulize mtu kkulewesha je wataku dhalilisha kiasi agani kwa kukuingilia kila sehemu, tuombe huyo Alexawe hana ukimwi au hao jamaa zake walio fanya mtungo hawana ukimwi,
   
 12. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,427
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  Rushwa tupu vituo vya polisi. Kwa ujumla kesi ni ya kupanga.
   
 13. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #13
  Mar 26, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  sHIGONGO=nELLY=pARTIC=pOLICE, WOTE WAMOJA BONGO KWELI NI TABU NI BALAA
   
 14. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #14
  Mar 26, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,427
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  Rushwa tupu vituo vya polisi. Kwa ujumla kesi ni ya kupangwa.
   
 15. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #15
  Mar 26, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,427
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  Rushwa tupu vituo vya polisi. Kwa ujumla mazingira ya kesi yanaonyesha niya kupangwa.
   
 16. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,427
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  Rushwa tupu vituo vyetu vya polisi. Kwa ujumla mazingira ya kesi yanaonyesha niya kupangwa.
   
 17. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #17
  Mar 26, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,435
  Likes Received: 2,307
  Trophy Points: 280
  Ondoa porojo zako za kijinga hapa. Unataka kutupotezea malengo ....
   
 18. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #18
  Mar 26, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  MISS TANZANIA 2ND RUNNER UP 2008 - NELLY KAMWELU ABAKWA.....

  Written by Mange Tuesday, 23 March 2010

  MENEJA masoko wa kampuni ya Dolly Wood and Konic Ltd, Patrick Mbasha (21), jana alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, akikabiliwa na kesi ya kumbaka Miss Ilala mwaka 2008 Nelly Kamweru.

  Wakili wa serikali, Misonge, alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mirumbe kuwa mnamo Machi 14 mwaka huu majira ya saa tano usiku eneo la Mbezi Beach, jijini, alimbaka Kamweru.

  Mshtakiwa huyo alikana shtaka hilo na Hakimu Mirumbe aliiarisha kesi hiyo hadi Aprili 5 mwaka huu, ndipo atakapokuja kutoa masharti ya dhamana na akaamuru mshtakiwa arejeshwe rumande.

  www.mohammeddewji.com/blog

  [​IMG]
  Pichani, Vodacom miss Tanzania 2nd runner up 2008 and Miss Ilala 1st Runner up 2008 Nelly kamweru


  Haya ndio maelezo ya Nelly Polisi


  Nelly anadai kwamba siku ya tukio alikuwa na shoga zake wawili wakipata a few drinks, baadae huyo patric anaedaiwa kumbaka aliwajoin hapo mezani.

  Baada ya muda walikubaliana wote wanne hawamie Club Bilicanas, kufika huko Nelly anadai Patric Mbasha alimpa kinywaji na alipokinywa tu kaanza kulegea na hakumbuki kilichotekea tena kesho yake akajikuta kaamka guest house akiwa na huyo patric huku huyo patric akidai kwamba keshamfanya mchezo mbaya tena akishirikiana na rafiki zake na pia kampiga picha za uchi,

  Hii ndio part ambayo inaleta utata.

  Nelly anadai baada ya jamaa kumwambia kambaka basin a yeye akajidai yupo in love na jamaa akamwambia sawa kwa vile keshamfanya basi waendelee kuwa wapenzi, akamwambie waende wote nyumbani kwa kina nelly akamuiintrode kwa wazazi wake kama mchumba kufika kwa kina Nelly , Nelly akawaamabia ndugu zake kwamba Patric kambaka na baada ya hapo All hell broke lose, na jamaa alijikuta akipigwa na ndugu za demu na kupelekwa na polisi na kushtakiwa na kubaka.

  Haya ndio maelezo ya patric

  Patric anadai kwamba , yeye ni kweli alikuwa sea cliff na Nelly na shoga zake, na pia alienda nae bilicanas lakini aliondoka Bilicanas peke yake akawaacha mademu hapo Bills,

  Kesho yake asubuhi akapigiwa simu na Nelly akimuomba kwamba aende nyumbani kwao ana maongenzi nae, jamaa kufika huko kwa kina Nelly ndio akakutwa na Balaa na kubaka.

  MMMMH…I don’t know what to think kwa kweli, but if it were me, nimejikuta nimebakwa nakupigwa picha za uchi sidhani kama ningekuwa na nguvu ya kuanza kumdanganya huyo alienibaka kwamba nampenda niende nae home kwetu, cos nimtu ambae namfahamu ningewahi polisi na polisi wangeenda kumtafuta,,

  MDAU WHAT DO U THINK??

  SWALI JE KAFANYIWA UCHUNGUZI NA MADAKTARI?JE KAKUKUTWA NA MICHUBUKO YOYOTE SEHEMU ZA SIRI???KUNA MTU ALIEONE HIYO VIDEO? ITABIDI TUMTAFUTE NELLY ATUHADISIE VIZURI…NA KAMA KWELI JAMAA KAMBAKA NAE APATE KIFUNGO CHA MAISHA KAMA KINA BABU SEYA..
   
 19. Mkereketwa

  Mkereketwa JF-Expert Member

  #19
  Mar 27, 2010
  Joined: May 19, 2007
  Messages: 202
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu dada alikuwa ni Miss Ilala 2008 na Miss Tanzania Second Run-Up 2008 anaitwa Nelly Kamweru.

  Ciaoo
   
 20. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #20
  Mar 28, 2010
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Imeandikwa: "Ficha upumbavu wako usifiche hekima yako".
   
Loading...